Sijashangaa wala kushtuka Mbowe kukamatwa kwa tuhuma za ugaidi

Sijashangaa wala kushtuka Mbowe kukamatwa kwa tuhuma za ugaidi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
TUHUMA ZA UGAIDI ZA MBOWE ZINAWEZA KUWA NA UKWELI WOWOTE?

Mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu yangu Freeman Mbowe ametiwa hatiani na polisi kwa tuhuma za ugaidi na kupanga njama za kutaka kuua na kudhuru viongozi wa Serikali. Mbowe alitiwa mbaroni akiwa Jijini Mwanza.

Toka namfahamu Mbowe amekuwa na siasa za aina hiyo, siasa za zilizojaa ukakasi mkubwa, siasa za kuwajaza upepo wanachama wake huku akiwadhuru wote wanaoenda kinyume na matakwa yake na wale wanaohatarisha uenyekiti wake ndani ya CHADEMA.

Tunakumbuka jinsi Chacha Wangwe, mwanasiasa kijana aliyechipukia miaka ya 2005 alivyofariki kwenye kifo chenye utata mzito baada tu ya mwanasiasa huyo kuonyesha nia ya kutaka kugombea Uenyekiti wa CHADEMA ili kumuondoa Mbowe. Alipitia nyakati nzito mpaka kufikia kifo chake cha ajari ya gari ambacho kilihusishwa moja kwa moja na nia yake ya kutaka kumng'oa madarakani Bwana Mbowe.

Baada ya Chacha Wangwe, ikafuata zamu ya Zitto Kabwe ambaye nae pia licha ya kuwa mwanasiasa kijana machachari ndani ya nchi na CHADEMA na ushawishi wake wa kutaka kumng'oa Mbowe, pia akakutana na masaibu ya kutosha ndani ya Chama hicho huku akizushiwa kashfa nzito na viongozi ndani ya CHADEMA mpaka kufika hatua ya kufukuzwa ndani ya CHADEMA na kutishiwa mara kadhaa kuuawa kwasababu tu ya nia yake ya kutaka kugombea kwenye nafasi ya Uenyekiti. Naye Zitto Kabwe akapata matatizo mazito kwa dhamira yake hiyo ya kutaka kugombea na mwisho akafukuzwa CHADEMA.

Mwisho ikawa kwa Mbunge wa Ndanda Mhe Cecil Mwambe ambaye naye baada ya kuonyesha nia ya kutaka kugombea Uenyekiti wa CHADEMA akaanza kutukanwa na kutishiwa maisha yake na viongozi na wanachama wa CHADEMA kwa sababu tu ya kufuata utaratibu wa kidemokrasia ndani ya Chama hicho kutaka kumng'oa Mbowe. Akabananishwa mpaka akaamua kukikimbia Chama hicho kwenda CCM. Alipitia masaibu yote hayo kisa tu kutaka kugombea Uenyekiti wa CCM.

Huyo ndiyo Mbowe ninayemfahamu Mimi na siasa zake.

Zaidi sikushangaa tuhuma za Mbowe kuhusika na ugaidi na njama za kutaka kuua na kudhuru viongozi kwa kuangalia mfululizo wa kauli zake zilizojaa uchochezi, uvunjifu wa amani, uhaini na uchonganishi mzito zilizowahi kutoka kwenye kinywa chake.

Mwaka 2016, Mbowe na wenzake wakaja na operesheni waliyoiita UKUTA ambayo Mbowe alitoa kauli nzito na chonganishi za kutaka kuchochea vurugu ambapo Mbowe mwenyewe alikubali kuitwa mchochezi huku akiwa na mfululizo wa kauli zilizojaa siasa za chuki, kichochezi na zinazohamasisha vurugu ndani ya nchi.

Unakumbuka jinsi Mbowe alivyosimama kule Mbeya na kuwaambia wanachama wake kwamba kwasasa ni lazima waunganishe nguvu ya umma kwa staili ya Libya na Misri? Na kudai wakubali kubeba majeneza kwa kusema "mapambano nchi hii hata kama Watanzania 100 watakufa lakini lazima tukubali kubeba majeneza." Hiyo ilikuwa Januari mwaka 2018.

Na mfululizo wa kauli zake za vitisho kwa vyombo vya ulinzi na usalama?

Kwahiyo kwa haya tu machache ninayomfahamu Bwana Mbowe, basi nakiri sijashangaa wala kushtuka Mbowe kutiwa hatiana na tuhuma za ugaidi na njama za kuua au kudhuru viongozi kwa sababu hizo ndizo aina za siasa za Bwana Mbowe. Anyway, tusubili mahakama itoe maamuzi yake.
 
Polisi hawatii mtu hatiani.

Mtu anakutwa na hatia baada ya mahakama kuendesha kesi na kuthibitisha pasi shaka ushahidi utakaopelekwa mahakamani.
Nimeisha kusoma hapo ulipoandika "polisi kumtia hatiani".
 
Matukio uliyoorodhesha ambayo na qenzako huwa wanayaorodhesha hayana uhusiano wa moja kwa moja na tuhuma unazomtupia Mbowe.

Unadai Chacha Wangwe alipata ajali ya gari kwa sababu ya kuutaka uenyekiti, kwani asingeutaka huo uenyekiti asingepata ajali ya gari? au kuupata uenyekiti wa Chadema siku hizi imekuwa kinga ya kuepuka ajali za magari?

Habari ya Zitto, huyu aliutaka uenyekiti wa Chadema wakati akiwa kwenye mahusiano ya kificho na aliyekuwa Rais wa JMT, Jakaya Kikwete, aliposhtukiwa akaulizwa akadai Kikwete ni sawa na baba yake, ulitaka mtu wa aina hii apewe chama akauze siri kwa aliyekuwa mwenyekiti wa CCM?

Kuhusu Mwambe, huyu alikuja Chadema akakaa muda aliokaa, then akaamua kugombea uenyekiti wa Chadema, alipoukosa akaanza kutoa shutuma kuhusu chama, kwanini zile shutuma asingezitoa mapema akasubiri mpaka alipoukosa uenyekiti? na baada ya hapo akarudi CCM, kama alikuwa mwana mabadiliko wa kweli kwanini asingeanzisha chama chake?

Wengi wenu mnaomshutumu Mbowe hamna hoja za msingi, mna copy & paste hoja za wenzenu halafu mnakuwa mnazirudia rudia kila wakati kujaribu kuwadanganya wasioijua historia vizuri, Mbowe sio gaidi.
 
CCM hawana tofauti na Makaburu au Wakoloni.Huwezi kuwatoa Madarakani kwa kupitia makaratasi /Sanduku la kura.Rejea vita vya ukombozi ; Africa kusini, Angola , Msumbiji, Zimbabwe, Namibia. Sina uhakika kama Mbowe na Chadema wameamua kufuata njia hiyo ,Lakini Ili CCM kutoka lazma itumike nguvu ya ziada!
 
Honestly... CCM mnairudisha nyuma hii nchi kimaendeleo kwa kiwango kikubwa mno,
Kwa kuona kwamba hakuna aliye bora zaidi yenu
Kwa kuona hakuna mwenye jema zaidi yenu
Kwa kudhani kwamba hakuna mkubwa zaidi yenu
Kwa kudhani kwamba hii nchi ni ya kwenu peke yenu
Kwa kuona kwamba mna haki kuliko wengine... Na uroho wenu wa maendeleo binafsi.
 
Kama inavyo semekana Mbowe alikuwa anaajiri/recruits askari na wanajeshi waasi kwa lengo la kuhujumu serikali na kuuwa viongozi wa serikali, basi kwakweli Mbowe alifika pabaya sana, siajabu ange ajiri hata wahamiaji haramu kwa lengo baya zaidi.

Matendo haya hayana tofauti na yale wanayo yafanya Bokoharam. Hata hivyo Jeshi la Polisi wakishirikiana na vyombo vyote vifanye upelelezi wa kina na kwa weledi wa viwango vya juu.
 
Tunakumbuka jinsi Chacha Wangwe, mwanasiasa kijana aliyechipukia miaka ya 2005 alivyofariki kwenye kifo chenye utata mzito baada tu ya mwanasiasa huyo kuonyesha nia ya kutaka kugombea Uenyekiti wa CHADEMA ili kumuondoa Mbowe. Alipitia nyakati nzito mpaka kufikia kifo chake cha ajari ya gari ambacho kilihusishwa moja kwa moja na nia yake ya kutaka kumng'oa madarakani Bwana Mbowe.
Salome mbatia naye aliutaka uenyekiti wa chadema, maana naye alikufa kwa ajali?
 
Kama inavyo semekana Mbowe alikuwa anaajiri/recruits askari na wanajeshi waasi kwa lengo la kuhujumu serikali na kuuwa viongozi wa serikali, basi kwakweli Mbowe alifika pabaya sana, siajabu ange ajiri hata wahamiaji haramu kwa lengo baya zaidi...
Hao wahamiaji haramu wangepitia wapi hadi kumfikia Mbowe na hatimaye kuwa Askari wake? (Ina maanisha kuna uzembe mkubwa kwenye idara ya uhamiaji).

Tumia akili za kawaida tu sio lazima uwe na PhD.
 
JUMA JUMA, tangu lini Polisi wakamtia Mtuhumiwa hatiani??jifunze ujue,na Ile safari ya vijana wa Kawe kwenda Ulaya kama alivyotuahidi Mgombea Ubunge Gwajima tunaenda lini?
 
Back
Top Bottom