Sijavutiwa na Toyota Harrier a.k.a Tako la Nyani

Huyu jamaa muongomuongo tu gari yenyewe kapewa test drive tu tayari anajifanya analijuaaa sasa utalinganisha vp saloon car na SUV offcoz saloon cars zilitengenezwa luxurious zaidi ya SUV lakini upande wa design tako la nyani ni zuri na heshima pia. Sasa speed120 ulikua unakimbilia wapi hatuko kwenye mashindano.
 
Harrier engine nyepesi sana haitoboi hata kwa crown wakikutana kwenye open runway. Crown iko more stable 😂😂 kwa kifupi harrier mbio zake ni zakwendea coco, kidombwi na morogoro.
 
Uzuri wa tako la nyani ni upi ukilinganisha na salon cars zaidi ya road clearance? Tena kwa mwonekano iko hivi C class w204 > BMW 320i >Crown >Harrier
 
Uzuri wa tako la nyani ni upi ukilinganisha na salon cars zaidi ya road clearance? Tena kwa mwonekano iko hivi C class w204 > BMW 320i >Crown >Harrier
Sijabisha kuhusu luxurious, crown ni luxury car ila harrier hiyo ni SUV maanake ni confortable kwaajili ya kubeba watu,mizigo na offroad. So kuzicompare hizi gari ni kosa kubwa inatakiwa ulinganishe bmw 320I na crown au benz c class na crown. Harrier linganisha na cluger au other SUV cars.
 
Gari inaweza kuwa SUV na ikawa luxurious pia mkuu mfano LX570 and the likes. Tatizo la Harrier ni kwamba sio proper SUV(ni crossover), sio luxurious, haina performance, sio fuel economical, haina balance barabarani, haina mwonekano mzuri ‘kihivo’ n.k . Harrier ni kwa watu wafuata mkumbo otherwise ni gari average sana na haikupi value for your money
 
We jamaa
 
Wewe ndio unafata mkumbo wa ubishi, tako la nyani ni gari luxury sana tu kulingana na bei yake, tatizo lake ni nyepesi zinapata ajari sana hasa kwa walevi, engine haina nguvu kiukweli inazidiwa kila kitu na vanguard ila ni nzuri kwa mwonekano na ndiomaana imeuza sana sio bongo tu harrier inauza mpaka marekani na uingereza , ila chuma imesimama na inamwonekano wa kishua bro kila mtu anapenda vitu vizuri hayo mambo ya engine na ulaji wa mafuta ni minor kitu cha kwanza mvuto, usipoielewa harrier demu wako ataielewa.
 
Popote ulipo nunua korosho nakuja kulipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…