17th Portion:
.... Mzee Dingi alimtumia msg Mzee KY kumtaarifu kuwa ndio wanakaribia, so tujiandae.
Plan ilivyokuwa ni kwamba, wakishafika pale center, Mzee Dingi alitakiwa kumpigia simu Mzee KY ili aje awapeleke kwenye eneo lake analouza. Wakishafika kwenye hiyo eneo, Mzee KY anatakiwa kuwaita majirani zake aliopakana nao kwenye ilo eneo analouza, ili waje kutambua na kuthibitisha mipaka.
Wakishaoneshana mipaka, na kuelewana katika kila kitu, hapo ndio wanatakiwa kuniita mwenyekiti, niende mpaka pale site, ili kuona eneo linalouzwa na mipaka yake. Nikishajiridhisha kuwa kila kitu kipo sawa, hapo wote kwa pamoja tunatakiwa kwenda ofisini ili kuandikishiana na kukabidhiana hela.
Kuhusu ofisi, Mzee KY angeshauri twende tukaandikishiane nyumbani kwake. Nyumba hii ambayo tulikuwa tumefikia, na ilikuwa na muonekano kuwa inakaliwa na familia so ni rahisi kuaminika. Pia mihuri yote muhimu nilikuwa nimeshapewa, hadi nyalaka za mauziano zilizoandaliwa na Mzee KY nilikuwa nimekabidhiwa. Kiufupi, nyalaka zote sahihi zilikuwepo na baada ya mauziano, yule mstaafu angepewa. Kasoro pekee iliyokuwepo, ni kwamba eneo linalouzwa sio letu.
Takribani nusu saa tokea atume ile msg, Mzee Dingi akapiga simu. Baada ya salamu na maongezi kidogo, Mzee KY akaenda kuwapokea. Kisha akaenda nao hadi eneo linalotakiwa kuuzwa.
Wakiwa pale, majirani wakapigiwa simu. Akaanza kwenda yule mwanasheria feki, robo saa mbele, huyu Mzee Kidevu nae akaenda. Nikabaki mwenyewe, mwenyekiti ndani ya ile nyumba.
Baada ya kama dakika 45 tokea yule Mzee Kidevu aniache kwenye ile nyumba, Mzee KY akanipigia simu niende. Moyo ulikuwa unadunda kuliko kawaida, ila kila nikifikiria mgao wangu nitakaopata, nikajipa moyo. Nikawafata walipo.
Wale wengine wote, hakuna aliyekuwa kabeba begi lake pale site, ni Mimi peke yangu ndio nilienda na kibriefcase changu pale site. Nilivyofika tu site, nikapatwa na mshangao baada ya kumuona mtu tunayetakiwa kumliza.
Unajua katika maisha, coincidences zipo, lakini kuna baadhi ya coincidences hata ujielezee vipi, ni ngumu watu wengine kukuamini.
Alivyogeuka yule mama tunayetaka kumuuzia eneo, nikajikuta nipo uso kwa uso na Mama mwenye nyumba niliyohama siku iliyopita. Binafsi kutokea moyoni, sikuwa nafahamu kama mlengwa ni yeye. Na hata sababu iliyonifanya nihame pale kwake, wala haikuhusiana na yeye kuwa target yetu.
Ila unadhani ni nani angeweza kuamini maelezo yangu?. Yani leo nimehama, then kesho tunaenda kumpiga tukio, alaf niseme nilikuwa sijui kitu? Mtu yeyote mwenye akili timamu na reasoning capacity ya kawaida tu, asingekubali.
Yule mama alivyoniona kwa mbali, akanitambua. Nikawasogelea mpaka pale. Akanipokea kwa bashasha sana.
"Mwanangu ni wewe? Siamini macho yangu, kumbe ndio umepata kazi huku?". Nikamjibu ndio. Akanichangamkia sana, "Mungu mkubwa, na wakati wa Mungu ndio wakati sahihi, angalia ulivyoinuliwa mwanangu". Muda huo anaongea yote, wale washirika wangu wote wapo kimya, kila mmoja kapigwa butwaa kivyake, kasoro Mzee KY, yeye alikuwa neutral.
Yule mama akaendelea, "Unaona mwanangu kuishi na watu vizuri ilivyo ni jambo jema? Mfano ungeondoka kwa ugomvi, leo hii tungetizamana usoni? Nadhan hata jambo langu leo lingekuwa gumu". Mzee Dingi ikabidi aingilie yale maongezi yetu, "Kwani nyie mnafahamiana?". Mstaafu akamjibu, "Ndio, huyu ni kijana wangu kabisa, nimefahamiana nae miaka mingi, na leo ona Mungu amenikutanisha nae tena, ili aweze kuwa msaada wangu kwenye huu ununuzi"
Mzee Dingi: "Ni jambo jema, basi hapa shughuli yetu itaenda kwa urahisi sana"
Mstaafu: "Yani hapa Sina mashaka kabisa, nipo kwenye mikono salama ya kijana wangu"
Yule mstaafu akanigeukia Mimi na kuniambia "Tena tukitoka hapa unikumbushe nikurudishie Kodi yako iliyokuwa imebaki, maana ulivyotoka tu, dalali akaleta mtu mwingine atakayeingia leo. Ilikuwa halali yako kuhama pale. Huku ni mbali mwanangu."
Akili ikaanza kunizunguka kuliko kawaida, hapa nisimame upande wa nani?, wa huyu mama, au wa ile timu?. Upande wowote ambao ningechagua lazima kuna consequences ningekutana nazo. Nikisema nisimame na kina Mzee Dingi, basi uhaminifu kwa huyu mama ningekuwa nimeuvunja. Nikisema nisimame na huyu mama, basi nijiandae kuingia kwenye vita na kina Mzee Dingi, maana nitakuwa nimewaingiza kwenye hasara kubwa sana. Dili za hela ndefu kama hizi, huwa zinamaandalizi mengi, na gharama kubwa inatumika, mfano ile nyumba ambayo tungeenda kuandikishiana, ilikuwa imekodiwa, na iliwekwa vitu vyote vya ndani ili ionekane kama ni makazi halisi.
Kufanikiwa Kwa Ili dili, ndio hela ya kucover hizi gharama zote ingepatikana. Kufeli Kwa Ili dili ni hasara, hasara ambayo hakuna aliyekuwa anataka itokee, na ndio maana maandalizi yake yalikuwa deep. Mpaka kufikia muda ule, hatma ya kufanikiwa au kufeli Kwa lile dili zilikuwa mikononi mwangu. Nikawa najiuliza, hawa watu watanielewa kweli??. Wote nikiwaangalia, they mean business, hakuna aliyekuwa na mzaha. Katika ile timu yote, nilikuwa namuhofia sana yule Mzee KY, ukiachana na yeye kuwa kiongozi, ila pia ni mtu fulani aliye serious sana muda wote. Macho yake yameingia kwa ndani, alafu makali sana. Akikuangalia sana unaweza hisi anachuki na wewe.
Wakati naendelea kuwaza hayo. Mzee KY akaamua kuchukua nafasi yake kama muuzaji wa ile ardhi, akamgeukia Mzee Dingi na kumwambia:
"Hebu tumalize ili swala, kuna sehemu natakiwa kuwahi"
Mzee Dingi: "Haya mama, twende mkaandikishiane, ila tufunge ili swala"
Mstaafu: "Sawa hakuna shida"
Mwanasheria feki na yule Mzee Kidevu kama wanaweza kuondoka, maana kazi yao ya kutambua mipaka wameshaifanya. Mzee KY akawazuia kuondoka, kwamba wao kama majirani na mashahidi, watatakiwa kuweka Saini zao kwenye zile nyalaka za mauziano.
Baada ya kuwaambia hivyo, akashauri twende nyumbani kwake tukasainishane. Nikamkatisha, kwamba kuna shida kidogo imejitokeza.
Wote wanne kasoro yule mama mstaafu, walinigeukia kwa mshangao, maana nilienda nje ya script. Yule Mzee KY alinikata jicho, ambalo lilinipa tafsiri kwamba nikizingua nimekufa.
Akili ikaanza kunizunguka kwa haraka, maana nilitakiwa kufanya maamuzi ndani ya muda mfupi, uhamuzi ambao ungeweza kuwa na impact kwangu, kwa muda mrefu ujao...
Baada ya kufikiria kwa haraka, kuna wazo likanijia kichwani. Wazo ambalo niliona lingesaidia kudelay ile process kwa siku chache. Nikawashirikisha nilichokuwa nawaza
Analyse: "Wazo la kwenda kuandikishiana kwako muuzaji, ni zuri, ila sio sahihi. Kiofisi zaidi, inatakiwa kila kitu kikafanyikie ofisini, ili baada ya hapo niweze kuacha nakala za haya mauziano pale, sitakiwi kuzunguka nazo"
Aisee wale jamaa walinikata macho ya chuki, hadi nikaingia ubaridi. Unajua nature ya hii kazi, maandalizi yake hayakutakiwa kuhusisha ofisi. Ndio maana hata ofisi feki haikuwa imeandaliwa. Kitendo cha kusema tuandikishiane ofisini, maana yake hizo ni gharama zingine za haraka ambazo tutaziingia.
Ajabu ni kwamba, Mimi wakati najaribu kitengua lile zoezi lisifanyike siku ile, yule Maza ambaye tunataka tumpige hela akaanza kunibembeleza nifanikishe mauziano siku ile ile.
Mstaafu: "Mwanangu hebu nisaidie Mama ako, nipate ili eneo siku ya leo, nimelisumbukia sana"
Analyse: "Naelewa mama, lakini haya ni maswala ya kiofisi, leo mkiuziana alaf nikapoteza nyalaka. Inaweza kuniweka hatiani huko mbeleni"
Kesho Yetu: " Kwanini upoteze nyalaka, serikali imekuamini kukupa hiyo nafasi, mbona unashindwa kujiamini?"
Mstaafu: "Wewe mbona ni kijana smart sana, acha kuniangusha bhana"
Mzee Dingi: "Kama wasiwasi ni huo, basi tukishaandikishiana, tutaenda kuzipitisha chini ya mlango wa ofisi. Jumatatu utawahi mapema ili uziweke kwenye mafaili"
Mstaafu: "Hela ya soda ipo kijana wangu, naomba sana unisaidie"
Huyu mama ndio alikuwa anazidi kunipa ugumu. Najaribu kutaka kumsaidia. Lakini yeye anazidi kuniwekea ugumu. Baada ya majadiliano ya dakika kadhaa, Mzee KY ikabidi aingilie kati;
Mzee KY: "Nakubaliana na mwenyekiti, yupo sahihi kwa anachokisema. Ili ni jambo nyeti sana, halitakiwi kupelekwa kiholela."
Wote tukabaki tunamwangalia kwa mshangao, sikutarajia kama angeniunga mkono. Inamaana huruma imemuingia au kuna kitu kingine anafikiria?
Akaendelea:
Mzee KY: "Nashauri tufanye mambo kiofisi zaidi, Jumatatu mpaka Jumatano sitokuwa na nafasi, ila naomba wote kwa pamoja tukutane ofisini siku ya Alhamisi ili tumalize ili swala. Na kuhusu gharama zenu za usumbufu nitazirudisha, wala msiwe na hofu"
Tukawa tumekubaliana hivyo, lakini sisi wengine wote tulibaki na maswali kichwani, Mzee KY anawaza nini?. Mbona tumeenda nje ya plan lakini hajapanick?
Kiukweli nilishindwa kabisa kumuelewa. Ikabidi nimwambie yule mstaafu anipe lift mpaka Dar, maana kuna mambo yangu nilitakiwa kuyaweka sawa kule. Mzee KY akaniangalia jicho lenye kuuliza "Huondoki na sisi?". Nikampotezea.
Kwenye gari ya yule mstaafu, nikapanda na Mzee Dingi. Wale wengine wakarudi kivyao. Tukiwa njiani yule mstaafu alinibembeleza sana nisimamie swala lake lifanikiwe ile. Nikamwambia asijali. Mzee Dingi akawa anachombeza hapa na pale, lakini tukikutanisha macho yake yananiambia "ntakuua apostle". Pamoja na jicho la chuki alilokuwa ananiangalia nalo, lakini alikuwa haruhusu nimguse hata kidogo. Kiufupi alikuwa ananitisha, lakini at the same time ananiogopa.
Baada ya kufika mjini, kila mmoja alienda na njia yake. Yule mama mstaafu alitaka kunipa lift ila nikahofia Mzee Dingi anaweza kutufatilia nyuma nyuma alafu apajue ninapoishi, so nikakataa. Wote akatushushia sehemu moja. Kabla hatujaachana Mzee Dingi akaanza kunipa makavu;
Mzee Dingi: "Apostle Unazingua sana ujue? Dili ilikuwa imeshaisha hii"
Analyse: "Ila kumbuka huyu mama Mimi ananifahamu vizuri tu, dili likiisha msala unabaki kwangu"
Mzee Dingi: "Msala ubaki kwako, kwani bado unaishi kwake? Tanzania mapori mengi sana, nenda hata Mtwara huko, sio lazima wote tuendelee kuishi mjini".
Analyse: "Nirahisi kwa wewe kusema hivyo, lakini pia tambua yule mama.....". Kabla sijamalizia kauli yangu, akanikatisha.
"Acha useng* apostle, kwani Mama ako yule?". Aliongea kwa nguvu na jazba kiasi kwamba watu waliokuwa karibu wote wakatugeuzia sisi macho. Ukimuona Mzee Dingi alivyokuwa kavaa na yale maneno aliyoongea, ilikuwa halali wapita njia kutushangaa.
Nikaamua kuondoka, nikachukua uelekeo wangu, Mzee Dingi nae akaeleka upande wake.
**************
Kuna jambo moja ngoja niliongelee japo wakati naanza kusimulia, sikuplan kabisa kuweka details zake.
Nilivyokuja kuzinguana na kina Mzee Dingi hadi ikafikia kuachana nao (nitasimulia mbeleni) niliendelea kuwa na mawasiliano na Mzee KY kwa muda kidogo. Katika huo muda, ndio alikuja kuniambia vitu ambavyo hata kwangu havikuwa clear. Tokea mwanzo nimekuwa nikisema tu, tukapiga dili ili au lile, lakini sikuwahi kusema how. Ngoja walau nielezee dili la huyu mstaafu ilikuwaje mpaka ikafikia hatua ya kwenda kuuziana ardhi kule vigwaza.
Mzee KY anawatu anaofahamiana nao sehemu kadhaa, kuna mtu alimpa tip kuhusu huyu mama mstaafu na mafao yake. Yeye siku zote huwa anahitaji info hiyo tu, kwamba pale kuna hela kiasi kadhaa inaweza kupatikana, then mengine yote anafanya mwenyewe.
Alivyopewa hiyo info, akaja kuoneshwa muhusika mwenyewe alivyo. Baada ya hapo akaandaliwa mtu wa kumfatilia na kukusanya taarifa zake za kutosha. Zikishapatika, analetwa mtu wa kuja kukuvuta kwenye himaya yao. Kama unayetaka kutapeliwa ni mtu mzima sana, basi katatumwa katoto, kama wewe ni kijana, atatumwa mtu mzima au mzee nk. Kwa huyu mstaafu, kalitumwa katoto kakiwa na sare za shule ya msingi. Mtoto alipewa namba ya simu imeandikwa kwenye kikaratasi, akaambiwa amfate yule mama mstaafu kisha amuombe simu ili ampigie mama yake, maana amechanganya magari (just imagine unakutana na mtoto wa primary maeneo ya kkoo, alafu anakuomba umpigie mama yake, huwezi chomoa. In reality hako katoto kanakuwa sio mwanafunzi, au hata kama ni mwanafunzi basi anakuwa planned).
Sasa ile namba ukiipiga, haitokaa ipokelewe. Itaita sana mpaka ukate tamaa wewe. Kinachofatia, utamsaidia yule mtoto kupanda gari za kumfikisha kwao. Itakapofika mida ya usiku, mwenye ile namba itakupigia na kusema amekuta missed call yako. Ukikumbuka tukio na kumuelezea, atakushukuru, Kisha atakwambia nilikuwa sehemu fulani ndio maana sikuweza kupokea. Hii sehemu fulani atakayoitaja, lazima iwe inaendana na wewe maana taarifa zako za kutosha zinakuwepo. Anaweza kusema nilikuwa kwenye ibada kwa Mwakasege, Kakobe au Mwamposa, or chochote ambacho ukikisikia kitaendana na wewe. Hapo ndio utamwambia "Ooh kumbe na wewe unapata huduma kwa huyo mtumishi?".
So kutokea hapo, hamtojadili habari za mtoto tena. Next mtajikuta mnaanza kukutana physically huko kwenye huduma za kiroho. Atazidi kuwa karibu na kujenga uhaminifu, mpaka kuna siku utaongea kitu kitakacho kuja kukuliza. Haya yote yanachukua muda mrefu sana, na ndio maana Mzee KY kwa mwaka alikuwa hafanyagi dili nyingi.
Sasa kwa huyu mstaafu ilikuwa kama hivi. Alikuja akaongea habari zake za kuhitaji kufanya mradi wa greenhouse na kilimo cha umwagiliaji katika mtindo wa kisasa. Hii ndio taarifa aliyokuwa anaisubiria Mzee KY. Alivyoipata, ndio akaanza kuweka plan ni kwa namna gani akamilishe plan. Wakati anaendelea na kuweka mipango yake sawa, ndio kuna siku aliniona na yule mama mstaafu kabla sijahama kwenye nyumba yake. Na kwavile alishawahi kuniona na kina Mzee Dingi, basi akapendekeza Mimi niwe included ili ku-smoothen the process.
So, kwenye lile dili sikujumuishwa kwavile waliniona smart na mchangamfu, bali ukaribu wangu na yule mama. It was not a coincidence, everything was planned. Na Mzee KY alikuwa ahead of time.
Pamoja na hayo yote, Kunishirikisha Mimi ilikuwa ni plan A, lakini haikuwa plan pekee. Na kitendo cha Mimi kuonekana na yule mstaafu pale site, dili lilikuwa tayari limeshafanikiwa kwa 80%, either niendelee nao au nikatae.
So muda ule nilipoachana na Mzee Dingi baada ya kushushwa kwenye gari na mstaafu, Mimi nilianza kufikiria ni jinsi gani naweza kumsaidia yule mstaafu bila kuingia kwenye utata na kina Mzee Dingi.
Wakati Mimi nafikiria hayo, Mzee KY kwa upande wake alikuwa ashanitoa kichwani kwake. By the moment tumeachana kule site, yeye tayari alisha-execute plan B. Plan ambayo timu nzima hatukuwa tunaifahamu, isipokuwa yeye. Kama ushawahi kuangalia movie, huwa kuna wale extra characters, wanaonekana kwenye vipande kadhaa ili kukamilisha matukio, baada ya hapo hawaonekani tena hadi movie inaisha. Hivyo ndivyo Mzee KY alivyotufanya timu nzima. Yani kipindi Mimi na Mzee Dingi tunatukanana barabarani kisa dili limedelay, kumbe kwenye dili lenyewe wote tumeshatolewa.
Kwa ufupi Mzee KY aliamua kuwa Solo.......
Endelea hapa
Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu, mpaka siku niliyokutana na yule Mzee