14th Portion
... Nilivyofika kwake, nilipokelewa vizuri kama vile hatukuwa na ugomvi. Nikala, Kisha nikala tena. Zikafatiwa story za hapa na pale. Kutokana na mishe niliyotakiwa kuifanya kesho yake, sikuweza kulala pale. Muda ulivyosogea, nikamwambia inabidi niondoke. Hakunizuia, maana alijua muda wowote anaweza kunipata. Kabla sijaondoka, nikaomba ile PS niondoke nayo.
Hapo ndio kama nilimtibua nyongo, maana sio kwa maneno aliyonitolea. Kana kwamba dakika chache zilizopita, sio sisi tuliokuwa tunafurahi. "Yani wewe unapenda kupokea, kutoa hutaki, haya nenda kaiombe ruhusa familia yako kuwa nataka kukupa zawadi, wakikubali, njoo uchukue, maana maamuzi yako wanafanya wao". Kiufupi alisema kama sipo tayari kukubali takwa lake, basi nisahau kuhusu ile PS. Nikakubaliana na hali. Nikaondoka.
Wakati nipo gheto nawaza dili la kesho tu. Mfano tukipata million 60, pale mgao wangu sio chini ya 10m. Nikaanza kuipangia matumizi kabisa, hapo ndio nikaona Mzee Dingi alikuwa sahihi, dili likifanikiwa naweza survive mwaka mzima bila stress. Baada ya mawazo ya hapa na pale, nikaamua kulala nitulize kichwa.
***** ***** ******* ** ** ****
Niliamka mapema sana, asubuhi ya siku iliyofuata. Ili niwahi pale maeneo ya kisutu, ile njia inapandisha kuelekea mtaa wa Lumumba. Lengo la kwenda pale ilikuwa ni kununua begi lenye muundo wa briefcase. Wakati nipo njiani naelekea pale, Mzee Dingi akanipigia, na kunitaarifu yule mstaafu amepata dharura, hivyo zoezi halitoweza fanyika siku hiyo, tutaenda kesho yake.
Baada ya kuongea nae, niliendelea na safari yangu, maana kivyovyote vile. Lile begi lazima niwe nalo. Baada ya kulininunua, nikaendelea na mishe zangu kama kawaida, kisha nikarudi ghetto. Kesho yake pia dili likabuma. Safari hii likasogezwa mbele wiki nzima.
Ikabidi tukutane wote kujadili nini kifanyike katika iki kipindi tunasubiria yule mstaafu mambo yake yakae sawa. Katika yale maongezi wakawa wanasema kuna kitu hakipo sawa ndio maana dili linakuwa gumu. Mzee Dingi akashauri kama timu, inabidi twende tena kwa mtaalam wao tukaangalie tatizo liko wapi (wao walishaendaga na huwa wanaenda sana). Kwavile Mimi nilikuwa ndio mgeni, wakashauri niwepo siku ya kwenda. Ila Mzee Kesho Yetu akakataa lile swala, akawaambia kwa mganga sio sehemu unayoenda enda tu kila ukitaka. Na kwavile wao walishaenda wiki chache zilizopita, basi ni apostle (Mimi) ndio natakiwa niende.
Mzee KY: "Huyu bwana mdogo ndio inabidi kwenda nae kuangalia shida nini, maana kila kitu kilikuwa sawa kabla hajahusishwa"
Mzee Dingi: "Ni wazo zuri pia, kwahiyo anaendaje?"
Mzee KY: "Nitaenda nae Mimi"
Mzee Dingi: "Ungepumzika tu mkuu, acha niende nae"
Mzee KY: "Hapana hakuna haja, nitaenda nae. Maana nataka nimpeleke sehemu tofauti na ile niliyowapeleka last time"
Mzee Dingi: "Sawa hakuna kama ni hvyo"
Nia yao ilikuwa zoezi la kwenda kwa mtaalam lifanyike wik end, ila nikawaomba wik end hiyo waniache nifanye mambo yangu, alafu jumatatu ndio twende huko kwa mtaalam. Baada ya kuelewana, tukasambalatika, kila mtu na uelekeo wake.
Jumapili asubuhi nikawasiliana na yule Mzee wa Kongowe, akaniambia nimsubirie pale pale aliponichukua mtoto wake mara ya mwisho. Mida ya saa nne, tayari nilikuwa pale, alivyofika tukaondoka wote.
Tulivyofika pale shambani, tulizunguka zunguka kwenye mifugo yake huku tunapiga Story. Dhumuni la kwenda kuonana nae safari hii ilikuwa ni kutaka kumuomba kama anaweza kunisaidia kuniunganisha sehemu yoyote ya ajira, maana maisha ya kuunga unga hayanaga dhamana.
Mzee: "Hicho ndicho najaribu kufanya mwanangu, ila sio rahisi kama unavyodhani"
Analyse: "Ila ulikuwa kwenye mfumo wao Mzee, japo ni ngumu, ila huwezi kosa namna"
Mzee: "Mambo hayapo hivyo kijana. Mimi pia nilifanya kuchomekwa tu, kama unavyojua sitokei kwenye familia zenye mashina na mizizi ya kisiasa. Watu wa kupenyezwa wanapigwa vita sana na inner circle. Na kibaya zaidi utawala ni mpya, kila mtu anajaribu kujitengenezea yeye njia, nani atanikumbuka?
Analyse: "Kwahiyo unanisaidiaje kijana wako"
Mzee: "Nitaendelea kuangalia angalia, ukipatikana upenyo, nitakwambia. Ila Sasa hivi wamebana sana mianya yote. Na walengwa tunaobanwa ni sisi, sio wao"
Analyse: "Sawa Mzee"
Mzee: "Mlango mmoja ukifungwa, kuna mwingine mahali fulani utafunguliwa kwa ajili yako, unachotakiwa ni kuwa tayari muda wote maana hujui ni lini, wapi au kutoka Kwa nani mlango wako utafungukia. Kwa umri wako hutakiwi kukata tamaa kabisa, siku zote tumaini ni sauti ya Mungu ndani yetu, bila hiyo huna cha maana utakachofanya".
Analyse: " Nimekuelewa Mzee"
Mzee: "Sawa, nitaendelea kuangalizia upenyo sehemu, ukipatikana nitakwambia, ila am not promising you anything"
Analyse: "Sawa, nashkuru sana"
Tukaendelea na shughuli zingine za hapa na pale, mpaka muda wake wa kuondoka ulivyofika, tukaondoka wote.
Niliendelea kujilaumu mpaka basi, kwa nafasi niliyopoteza. Niliipiga teke njia rahisi, nikachagua kuhangaika kusikokuwa na faida. Kesho jumatatu ilibidi asubuhi ninyonge tai, moka nzuri, unyunyu kisha nielekee ofisini, ila sababu ya uzembe, ntaenda kukutana na wazee wasio na hekima, ili twende kwa mganga. Maisha haya π
π
π
Kesho yake mapema nikakutana na Mzee KY maeneo ya mbezi stand ya gari ndogo, safari ya kuelekea Moro ikaanza. Baada ya kufika Moro, tulitembea kwa dakika kama 30 kisha tukaachana na mji, na kuchukua njia kuingia ndani ndani huko. Safari nzima, mawazo yangu yapo kwenye mazungumzo yangu na yule Mzee kule Kongowe.
Mimi na Mzee KY hatukupiga story nyingi njiani, ni Mzee ambae sio muongeaji, muda mwingi anasikiliza tu. Na hizo story chache tulizopiga, ni kwamba alikuwa ananiuliza kitu, then ananiacha nibwabwaje.
Baada ya mwendo wa kama lisaa na nusu au mawili, tukafika mwisho wa safari yetu, then tukaelekea kwa huyo mtaalam wake.
Inaonekana alishawasiliana na yule mtaalam, kumjulisha ujio wetu. Maana tulivyofika, baada ya salamu hapakuwa tena na mazungumzo mengi, nikaambiwa niingie kwenye chumba kilichokuwa vyumba vya nyuma. Mzee KY akamwambia mtaalam bwana mdogo atoke kaiva, mganga akacheka tu. Nikaingia kupikwa kwa mara ya kwanza.
Niliambiwa vitu vinavyotakiwa kununuliwa mfano nazi, karatasi nyeupe, wembe, unga nk. Hela ilitolewa, vikafatwa. Palifanyika mambo mengi sana na mazito, tena kwa muda mrefu. Nilianza kwa kusuguliwa na mchanganyiko wa unga wa sembe na tui la nazi mwili mzima. Vikafatia visomo, chale kuanzia unyayoni mpaka utosini. Kiufupi zoezi lilikuwa zito. Kimoyo moyo najiuliza "Huyu ni Mimi ndio nafanyiwa hivi au?''. Baada ya hapo nikatakiwa kutoka nje vile vile na boksa yangu, mpaka katikati ya kiwanja alafu nirudi ndani. Nikamuuliza yule mganga, "Natoka hivi, na wale watu waliopo nje je?". Mganga akanikata jicho, kiasi kwamba nikajikuta nanyanyuka.
Aisee ukiona mtu anahela, wewe muheshimu tu, haijalishi kazipata vipi. Watu wanasuffer mazee, kila njia ni tough.
Mida ya jioni ndio tulimaliza. Nikapewa dawa ambazo nilitakiwa kujifukiza kwa siku kadhaa, na zingine ambazo nilitakiwa kuoga, lakini hizi za kuoga, sikutakiwa kuziogea bafuni au chooni. Kuna dawa ilikuwa mchanganyiko wa unga mweusi, na mafuta mafuta, hiyo nilitakiwa kuichanganya kwenye mafuta ya nazi, kisha niwe napaka viganjani na usoni kabla ya kutoka nyumbani na kwenda kwenye mishe mishe zangu. Lakini pia nilipewa kitu mfano wa hirizi, ambayo upana wake unakaribia kucha ya kidole cha shahada. Hiyo niliambiwa niwe nayo muda wote. Hizi dawa mbili (ya kupaka na hirizi) zilifanya mpaka kesho nina bifu na Mzee Dingi.
Kila kitu kilivyokuwa kimekamilika, tukaaga na kuondoka. Njiani Mzee KY ananiambia, "Bwana mdogo ukiwa serious kwenye maisha utafika mbali sana, ila kwa muda mchache ambao nimespend na wewe, tatizo lako kubwa ni moja tu"
Nikamuuliza tatizo gani??. Akanijibu, "You don't smile easily". Nikatatizika kidogo, "Kuto tabasamu nalo ni tatizo?". Akanijibu "Bado una mengi ya kujifunza". Nikabaki namwangalia tu. Katikati ya story zilizoendelea, nikajikuta namwambia "Sikuwahi fikiria kama siku moja ningeangukia huku". Akacheka.
Mzee KY: "Tukiwa wadogo, ni ndoto ya kila mtoto kuwa rubani. Hii Dunia jinsi ilivyo, ukiteleza kidogo tu inakuchagulia njia"
Hapo ndio akaniambia machache kuhusu yeye. Katika hayo maongezi yetu ndio niligundua kuwa ana masters ya uhandisi wa umeme, lakini pia ana CPA, ana uwezo wa kuzungumza lugha 3 za kimataifa kwa ufasaha kabisa. Chuo alisomeaga Uganda. Na ana ofisi mbili town, lakini just for backup, japo zinafanya vizuri.
Nilimshangaa sana kwanini ameamua kuendelea na njia ile wakati ana uwezo wa kutengeneza decent money?
Mzee KY: "Sikia bwana mdogo, hii Dunia inaweza kukuchapa alafu haikupi kabisa muda wa kujutia. Na hata ukiwa kwenye kujutia, inaweza ikakuchapa tena, kiasi kwamba ukiwa kwenye kujutia kwako, ndani yake ukapata majuto mengine".
Wakati najaribu kujiuliza amemaanisha Nini, akaendelea, "Unatakiwa kujutia huku unaenda nayo, maana muda haukusubiri".
"Sema sijui kwanini wewe umeingia huku, ila binafsi kisasi na kinyongo nilichokuwa nacho juu ya mtu fulani ndio kimeniingiza huku. Nilipima kina Cha maji kwa mguu, sasa nimeshazama tayari".
Hakuongea tena mpaka alivyonishusha mbezi mwisho.
. ****** ******** ********** ** ***
Baada ya pale, nikanyoosha mpaka gheto kwangu. Kwavile sikuwa nimejiandaa sehemu ya kuogea, ikabidi nibebe ndoo yangu hadi kwenye kiwanja cha shule ya msingi (nilikuwa jirani na shule), nikaenda kuogea pale chap, then nikarudi ghetto kujifukiza ile dawa nyingine. Baada ya hapo nikalala.
Kabla ya kwenda kwa mganga, kuna vitu vingi sana nilikuwa sivielewagi, na sivipatii majibu. Nilikuwa nikipishana na vijana (wakike kwa wakiume), unakuta mtu smart, lakini macho mekunduu kuliko kawaida, japo sio mlevi wala mvutaji sigara. Au mkipishana unahisi harufu ya moshi tu. Nilikuwa najiuliza, hivi hapa mjini kuna watu wanapikia majiko ya kuni au?. Kumbe hakuna bhana, vijana wanajifukiza sana. Tena wameanza kuoga moshi kabla hata ya Corona.
Hizo siku tatu za kujifukiza, nilikuwa nanuka moshi muda wote. Kibaya zaidi, zile dawa za kuoga hutakiwi kutumia sabuni.
Kipindi naendelea na ile dozi. Mzee Dingi akawa ametupa taarifa kuwa alipigiwa simu na yule mlengwa wetu, wamekubaliana zoezi litafanyika siku 6 tokea hiyo siku. Maana alikuwa anajipanga, akishanunua lile eneo basi mipango yake mingine iende haraka pia.
Nikamaliza masharti, tukabaki tunamsikilizia yule mstaafu, japo tulipiga dili kama mbili, na zote zilitiki vizuri tu.
Kile kihirizi alichonipaga yule mtaalam, aliniambia kwavile natakiwa niwe nacho muda wote mwilini, basi naweza kukihifadhi kwa namna tatu. Mosi, nikifunge kwenye kamba, alaf nikibane mkononi kama wanavyofanya makepteni wa mpira, Pili, nikizungushie big g, alaf nikienda eneo la tukio, nikibane mdomoni, tatu, nikitengenezee bangili, au pete ya kukibana then niivae.
Mimi nilitengeneza pete za kacha zile, alafu nikakishonea pale. Nikaivaa kwenye kidole cha pete, mkono wa kulia.
Zikiwa zimebaki siku tatu twende kwenye lile dili kubwa. Nilikuwa zangu gheto tu nimekaa, wazo likanijia nikajaribishe zile dawa sehemu. Akili ikanituma niende kwa Shani.
Mida ya jioni, nikaoga, nikapaka mafuta yangu ya nazi yenye dawa, mikononi na usoni. Kisha nikatoka.
Aisee Hii Dunia ni zaidi ya tuijuavyo. Kuna vitu vingi sana vipo beyond our explanations.......