Suala la kuliliwa nalishuhudia kwa wenzangu tu, umri sasa unanigongea hodi lakini mpaka sasa sijabahitika kukutana na mtoto shombeshombe au tipwatipwa aliyejaribu walau kutoa leso yake na kufuta malengelenge ya machozi kwenye macho yake kwa kitendo cha kumwacha. Huu si mkosi kweli?
Nifanyeje wandugu, kwa sababu kama ni pesa zimenitoka sana, mwisho mimi ndiye nakuwa mzee wa kuwapigia magoti kuokoa manowari isizame.
Nifanyeje wandugu, kwa sababu kama ni pesa zimenitoka sana, mwisho mimi ndiye nakuwa mzee wa kuwapigia magoti kuokoa manowari isizame.