Sijawahi kununua saa inayozidi Tsh elfu 3. Mnaonunua za laki mbili zinakuwa na nini cha zaidi?

Sijawahi kununua saa inayozidi Tsh elfu 3. Mnaonunua za laki mbili zinakuwa na nini cha zaidi?

Sioni umuhimu wa kununua saa ya mkononi kwa maisha ya sasa ambapo hata mtoto mdogo ana uwezo wa kumiliki simu na hakuna simu iliyo kosa saa.

Saa ungeniambia wavae wanafunzi ambao shuleni hawaruhusiwi kwenda na simu sawa lakini unakuta mtu ana simu huku amevaa saa tena ya nini.

Siku hizi kuvaa saa naona ni ushamba na saa za mikononi siku hizi zimebaki kama fashion tu, mimi kwa mtazamo wangu naona ni ushamba na sipendi kuzitumia,
 
Unasema zimebaki kama fashion hapo hapo unasema ni ushamba mbona hueleweki?
Sioni umuhimu wa kununua saa ya mkononi kwa maisha ya sasa ambapo hata mtoto mdogo ana uwezo wa kumiliki simu na hakuna simu iliyo kosa saa.

Saa ungeniambia wavae wanafunzi ambao shuleni hawaruhusiwi kwenda na simu sawa lakini unakuta mtu ana simu huku amevaa saa tena ya nini.

Siku hizi kuvaa saa naona ni ushamba na saa za mikononi siku hizi zimebaki kama fashion tu, mimi kwa mtazamo wangu naona ni ushamba na sipendi kuzitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saa za bei ya chini hazina ubora, huwa haziendi sawa sawa, huwa zinakimbiza muda, pia huwezi kuogelea nayo au kufua. Mimi napenda saa za Casio haziingizi maji, zina memory, zina timer, alarm,na light hata usiku naona, napendelea hasa zile za plastic na bei sijawahi kununua chini ya 40,000/= Pia zinadumu, nakaa nazo hadi miaka 10. Tangu mwaka elfu mbili hadi leo ni saa ya tatu kununua.
Mara ya mwisho nanunua saa ya mkononi ilikuwa Tsh elfu 3000. By then ilikuwa saa kali tu.

Sasa siku hizi naona marafiki wananunua saa hadi za laki mbili.

Je, hizo saa za gharama huwa na nini cha ziada?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi napenda kuvaa saa vigezo vifuatavyo vimenifanya nijichagulie saa ye thamani ya 75000 (NX05) apo kulingana na kipato changu na mapenzi yangu ya kuvaa saa.

>rangi nyeusi
>mikanda plastiki
>water&dust resistance
>inahimili misukosuko
>Pia iwe na uwezo wa kuconnect na smartphne yngu (smartwartch)
>iwe ya mshale
Sasa kwa sifa hzo chache huweza eti ukapata hyo saa kwa 3000 au 10000, ila ifahamike kuna wale wanao nunua vitu kutokana tu na makundi au fulani amuone au urembo,mm binafsi saa kwangu ina kazi zaidi ya urembo.
 
Duu wewe unaweza kuwa unakula ugali dagaa kila siku, kwa kisingizio cha kwamba aliyekula chips kuku na aliye kula ugali dagaa, wote wameshiba, wote kesho njaa itawakaba tena and wote watatoa kinyesi chenye rangi moja bt wametumia gharama tofauti!!! Mmmh hyo ni defence merchanism ukweli ni kwamba tunaishi kulingana na uwezo wetu kiuchumi tusibeze style za maisha ya watu.

- Hata nyumba za kulala wageni zinatofautiana gharama bt wote mkilala kunakucha salama, lakini haimaanishi ukachukue chumba cha tsh5000, wakati unauwezo wa kuchukua chumba chenye hadhi nzuri kwa gharama ya juu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mmoja wa "walevi" wa saa za mkononi, yaani nikisahau kuvaa saa nitajikuta nahisi mkono umekosa kitu na kusababisha niwe unconfortable siku hiyo nzima.

Nilipofanya vizuri kwenye mtihani nikiwa shule ya msingi (darasa la tano kama sikosei) Mzee alinipa zawadi ya saa mpya, miaka ya tisini mwanzoni wakati huo ndio saa za digital zimeingia mtaani...sitosahau ile harufu ya saa mpya ya plastic.

Nahisi ulevi wangu wa saa ulianzia pale.

Nakumbuka nilipoanza kazi nilidunduliza pesa mpaka nikaenda kununua moja ya saa ya ndoto yangu, ilikuwa saa ya TAG HEUER, kwa sasa sina hiyo saa, ila bado navutiwa kuvaa saa nzuri ya gharama.

Mimi huwa najiuliza swali kama hilo kwa ninaowaona wanamiliki zile simu za milioni au zaidi.

Kujibu swali lako, zaidi ya kufahamu muda kwenye saa, huwa napenda saa yenye kuvutia kwa gharama yoyote ile.
 
Back
Top Bottom