Mimi ni mmoja wa "walevi" wa saa za mkononi, yaani nikisahau kuvaa saa nitajikuta nahisi mkono umekosa kitu na kusababisha niwe unconfortable siku hiyo nzima.
Nilipofanya vizuri kwenye mtihani nikiwa shule ya msingi (darasa la tano kama sikosei) Mzee alinipa zawadi ya saa mpya, miaka ya tisini mwanzoni wakati huo ndio saa za digital zimeingia mtaani...sitosahau ile harufu ya saa mpya ya plastic.
Nahisi ulevi wangu wa saa ulianzia pale.
Nakumbuka nilipoanza kazi nilidunduliza pesa mpaka nikaenda kununua moja ya saa ya ndoto yangu, ilikuwa saa ya TAG HEUER, kwa sasa sina hiyo saa, ila bado navutiwa kuvaa saa nzuri ya gharama.
Mimi huwa najiuliza swali kama hilo kwa ninaowaona wanamiliki zile simu za milioni au zaidi.
Kujibu swali lako, zaidi ya kufahamu muda kwenye saa, huwa napenda saa yenye kuvutia kwa gharama yoyote ile.