Sijawahi kuona tajiri ameanguka kwa mapepo kanisani

Sijawahi kuona tajiri ameanguka kwa mapepo kanisani

Linapokuja swala la Imani tunapaswa kutumia akili sana na si hisia wakristo wengi wanaamini katika ishara na miujiza lakini maandiko yalishaweka wazi, Mungu ni Mungu wa maarifa (Hosea 4:6, warumi 11:33).

Yesu alipokuja Duniani alikuta waumini walioshika maandiko(torati) japokiwa Agano la kale torati na manabii vyote vilikuwa vikimshuhudia Yesu lakini viongozi wa dini na waalimu wa dini walishindwa kumtambua Yesu alipokuja. Wale waliompokea waliweza kuhakiki kupitia maandiko na kuamini ya kuwa ndiye masihi aliye ahidiwa (yohana 1:45)(yohana 1:11-13).

Maandiko yanashuhudia kuwa yamebeba Siri kubwa (Marko 4:11) na hakuna theolojia ya Dunia hii inayoweza kuyafasiri maandiko kwa ufasaha isipokuwa Mungu mwenyewe (mithali 30:5-6). Leo hii yeibuka madhehebu mengi mno kila dhehebu likiwa na theolojia yake ambazo ukipima unaona ya kuwa ni mawazo ya kibinadamu tuu.

Maandiko yanazungumza juu ya ufalme wa Mungu na uzima wa milele, ukisoma
Yohana 11:26
[26]naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?. Mchungaji wa kweli anapaswa kumueleza muumini kupitia Biblia Nini afanye (mapenzi ya Mungu) ili basi awezeishi milele kama Yesu alivyoahidi apo. Msingi wa Imani ni maarifa ata Yesu alipokuja mara ya kwanza alifundisha watu kuyajua mapenzi ya Mungu kwanza ndio maana mara nyingi alikuwa akiwaita enyi wenye Imani haba si kwa kuwakejeli la ila alikuwa akiwakumbusha kuwa maarifa ndio ujenga Imani ya kweli na hata wanafunzi walimjibu Yesu "utuongezee Imani bwana".

Ufalme wa Mungu umefichwa katika maandiko swali la kujiuliza ni je umeuona na kama bado ni kwanini, ukisoma mathayo 13 tunaona Yesu ameutaja ufalme wa Mungu kwa namna mbali mbali za mifano na mafumbo ukielewa maana ya hayo mafumbo na mifano kupitia Biblia waweza uona ufalme uliozungumziwa. Amka ndugu yangu badala ya miujiza naishara tafuta kimjua Mungu kupitia neno lake na kama alivyoahidi kupitia YEREMIA 33:3 utashangaa jinsi yalivyo makuu matendo yake na uweza wake.

BiBLIA ni njia ya kutuongoza kwenye ufalme wa Mungu, ni ngumu kueleweka kwakuwa imeandikwa kwa lugha ya mafumbo na mifano yapo Cha ajabu ni kuwa Biblia yenyewe inamajibu yote ya hayo mafumbo na mifano iliyopo. Nikushauri tafuta chuo Cha Biblia kinachoitwa Sayuni mission center kimetapakaa Duniani kote kwa kwetu Tanzania wanamatawi mbali mbali kwa Dar ni (Mwananyamala, tegeta, g.mboto, kigamboni, kimara, tabata) na mikoani kama Arusha, iringa, mbeya, Mwanza, nk. Wanatoa mafunzo BURE kabisa na utafundishwa Biblia kuanzia kitabu Cha MWANZO mpaka UFUNUO, lakini pia utaweza kupata majibu ya maswali yako yote yanayohusu Biblia kupitia Biblia.

MUUJIZA WA KWELI NI KUMJUA MUNGU KUPITIA NENO LAKE (YEREMIA 33:3)
Hizi hekaya za Biblia ndio unaita maandiko?
 
Hayo mambo yamekaa kiimani zaidi

Tuwaache akina Mama/Dada waendelee kuona upako wa KiMungu kupitia maombi 🙏
 
Hizi hekaya za Biblia ndio unaita maandiko?
Ndio hizi unazozisoma kama hekaya kwenye Biblia nayaita maandiko. Ukielewa ujumbe uliobebwa na maandiko haya hayatakiwa hekara tena kwako. Swali ni je unayokiu ya kufahamu?
 
Back
Top Bottom