Sijawahi kuona timu inafanyiwa maombi ili ifuzu World Cup

Sijawahi kuona timu inafanyiwa maombi ili ifuzu World Cup

Ila corona iliombewa mkuu na tukaishinda.

Hata hili litawezekana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ni Tanzania pekee timu inafanyiwa maombi ili ifuzu World Cup, sijawahi ina na haingii akilini!! TFF achaneni na huo ujuha mtakuja kujuta...
Ndugu na ndiyo maana Watanzania tunadharauliwa sana na Majirani zetu na mno na Wazingu mpaka Waeshia.
 
Mimi mganga. Uwezo wa kuipeleleka timu Doha ninao. Ila nahitaji mpunga mrefu kidogo.
 
Mie namsubiri nabii na mchungaji wa mitume na manabii wa TZ, komando Mashimo, aweke wazi ufunuo aliofuniliwa kuhusu kufuzu kwetu kwenda kombe la dunia Qatar.
 
Ni Tanzania pekee timu inafanyiwa maombi ili ifuzu World Cup, sijawahi ina na haingii akilini!! TFF achaneni na huo ujuha mtakuja kujuta...
Kwa sababu hujawahi ona haina maana kuwa hakuna.
Hujawahi ona wachezaji wanasali kabla ya mechi?
 
Kumuomba Mungu akusaidie jambo lako ni ajabu badilikeni basi kama unaona kwako si sahihi unapiga kimya.....Taifa stars wamefanikiwa kuongoza kundi hizo ni juhudi tosha sasa wakimuomba Mungu awavushe hatua inayofuata ni vibaya wabongo mnachuki za ajabu sana.
Wamisri na timu zote za kiarabu swala ni nguzo yao popote waendapo kucheza lazima wamuombe Mungu sioni ajabu hapo kama timu inafanya mazoezi kujiandaa na mechi wakimuomba Mola karima sio vibaya kijana.
 
Kwa sababu hujawahi ona haina maana kuwa hakuna.
Hujawahi ona wachezaji wanasali kabla ya mechi?
Algeria timu yao nzima waliswali hapo uwanjani kwa mkapa walivyokuja kucheza na Taifa stars....wabongo ni mambumbumbu huwezi kuchukia kile ulichokadiriwa na Mungu....kama ulikuwa mdau wa soka toka kitambo kuna mabadiliko makubwa sana ya soka hapa nchi watu wanalia uwekezaji kuanzia academy na level zote...kwa mimi naona uwekezaji watu wanafanya japo sio kama wenzetu waliotutangulia hao wanaoilinganisha na Tanzania....leo tuna vijana wanacheza nje ligi za kueleweka zamani unasikia mchezaji ameenda Oman au Quwait tulikuwa na wachezaji wanacheza ligi za kujitolea nje huko,Taifa stars ilikuwa haiwezi kupiga pasi tatu bila kupoteza...wachezaji walikuwa wanatetemeka wakiwa na mpira...hiyo ni kabla ya Maximo baada ya yule mbrazil timu ya taifa imebadilika sana na soka letu limepiga hatua sasa watu wanabeza nini sijui naona ni upumbavu au ni watoto wa juzi hapo ndio wanaleta ujuaji.
 
Back
Top Bottom