Nachoka mimi babu yake mwandambo! Kuna kikundi gan kenya kila sku wanakimbilia uko
Unajua jamaa ameuliza swali zuri tu lakini hisia za wajibuji zimekuwa kama jamaa anajua sababu na amekuja kukejeri .mimi sijaona kejeri kauliza kutaka jua tu pengine hajawahi fika kenya wala uganda anauliza kiungwana tu kuelewa tu.
MM NATAMJIBU KWA USERIOUS
Kaka nchi zote duniani ziko kwenye kupambana kufikia utawala bora wa kidemokrasia ,vitendo vya rushwa kuwa duni na kujitegemea.
Haya unayoona maandamano ya vurugu mara chaguzi za kuibiana kura mara kutekana na kufira wapinzani ni mambo yametokea mataifa yote kuelekea taifa lenye maendeleo na huru.
Kwa east africa kimaendeleo hayo kenya huwa iko mbali sana kulinganisha na Tanzania .
Ni kama tanzania ilivo mbali kulinganisha na rwanda huwezi kuwa rwanda eti ukaandamana au et una ofisi kabisa ya upinzani na unafanya mikutano wao bado hatua za zaman za nyerere.ndo maana wao kagame anaenda mwaka wa 30 sisi tushabadili maraisi wanne toka aingie na uganda marehemu kabisa wako na babu yao.
Nimeishi kenya uganda na tanzania nikutajie machache ukiwa kenya ambayo yanafanya wakimbilie kule
1.Kenya ukishaingia kwa taratibu zote hata rais ruto hana uwezo wa kukufanya lolote kwa mujibu wa katiba .kenya mtanzania uliegonga pasport unamfokea polisi kama mwanao katiba inalinda wote.
2.kenya hakuna wa kukuonea yaan watanzania huwa wako huru na wana haki zao kenya kuliko tanzania .
3.kenya hakuna utekaji holela .na ukishitakiwa kubambikiziwa haina maana .MAKOSA YOTE KENYA YANA DHAMAN HAFI KUUA.Kwa hiyo tundu lissu angekuwa kenya angeendelea na kesi na angegombea uraisi vizuri
Kwa nini utekaji mgumu kenya? Kwanza jeshi liko huru kukataa hata maagizo ya rais bila kufukuzwa kazi .waliwahi jaribu teka teka mahakama ilifuta kazi maafisa polisi kibao .je unadhani hawa polisi chadema wangeenda na ushahidi hata wa kutekwa watu 10 tu mahakama ikafukuza kazi wakuu wa polisi 20 wapya wangekubali atekwe mtu??
4.kenya hakuna mambo ya kinga dhidi ya kushitakiwa ukipewa amri uue ukaua unashitakiwa unafungwa na hakuna mkono wa rais jela unaenda kukaa kikwel .mahakama imewahi mfuta kazi igp kwa sababu ya yale maandaman aliitwa mahakaman akakaidi wakampiga chini rais akamrudisha wakamchapa na yy barua akanyoosha mikono
5.KIUCHUMI :Kenya hakuna mambo za kuchungulia akaunti za mtu leo ww nenda na mabilion kanunue majengo hakuna ataekuja hata kukuongelesha ndo maana wasomali wamejaa .Kampuni zote za magari na zote kubwa east africa makao makuu yao nairobi si kwa bahati mbaya watu wanaweka mabilion mahali sheria imenyooka kenya unaweza ishitaki serikali mahakama yao na ikashindwa na ikakulipa fidia vizuri tu na rais hana lolote mahakaman zinashindana hoja no maagizo
5.uchumi mzuri .ukitaka ufungue kampuni tanzania inachukua wiki mbili hadi mwezi mamilolongo .kenya katiba imekaba taasisi ndani ya siku 3 unafungua kampuni yenye kila kitu hadi akaunti.niliishi kenya miaka 3 sikuwahi kujua tra wanavaa nguo gani hawapo kabisa kusumbua biashara za watu
6.kwa kuhitimisha hapa bongo unaweza kaa wiki nzima hujawahi muona mtu asie mtanzania ila kenya huwezi maliza siku nzima hujaonana na mtanzania mwenzio mnaijeria etc pia kenya wazungu kibao huomba uraia NINI MAANA YAKE? Yaani hata raia wengine dunia wanajua kwa east africa nchi huru zaidi ni kenya tena kwa mbali kabisa ukifika soko la kikombaa wachaga wamejazana .
Na mm nimeishi miaka 3 na walikuwa wananiita kijana wa kikwete lakin sijawahi hata siku moja kuulizwa passport yako iko wapi na uliingiaje kenya.wakati bongo uliza polizi wanaamsha hadi wageni usiku kukagua passport
UNavoiona tanzania ilikuwa hivo enzi za arap moi aliteka sana .walifirwa sana .aliua sana hata raila alikaa jela kama tundu lisu