Sijawahi kusikia hotuba yenye nguvu kama hii aliyotoa Malcom X

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Nimekuwa nasoma biography ya Malcom X. Huyu mtu alikuwa wa pekee sana. Hapa nataka kuzungumzia hii hotuba yake(The ballot or the Bullet) ukweli sijawahi sikia hotuba yenye nguvu namna hii.

Hotuba nyingi bora huwa za kujifanya tu, wanasiasa wakitumia maneno makubwa, wakiongea wanayotaka watu tu. Si hotuba hii. Hii hotuba aliyeitoa anamaanisha. Hotuba hii inamaana hata leo hii, hata kwa nchi yetu.

na Nimekuwa nasoma biography ya Malcom X. Huyu mtu alikuwa wa pekee sana. Hapa nataka kuzungumzia hii hotuba yake(The ballot or the Bullet) ukweli sijawahi sikia hotuba yenye nguvu namna hii.

Hotuba nyingi bora huwa za kujifanya tu, wanasiasa wakitumia maneno makubwa, wakiongea wanayotaka watu tu. Si hotuba hii. Hii hotuba aliyeitoa anamaanisha. Hotuba hii inamaana hata leo hii, hata kwa nchi yetu.

Lycoon...
Unasoma kitabu kipi cha Malcolm X?
Malcokm X ana vitabu viwili maarufu kuhusu maisha yake.

Kipo alichoandika Alex Hailey ''The Autobiography of Malcolm X (1964) alichoandika Manning Marable, ''Malcolm X Life of Reinvention,'' (2011).

Kitabu cha Hailey kilitoka baada ya kifo cha Malcolm X na inasemekama kuwa Hailey alibadilisha mambo mengi baada ya kuona Malcolm hayupo tena duniani.

1686084480142.png
 
Ninasoma hiki cha hiki cha Haley. Wanadai kweli kuna sura na baadhi ya mambo alipunguza. Hiki cha Manning kipo full?
 
Lycaon...
Kitabu cha Marable Manning kimefanya kile kilichotakiwa.

Nimekinunua kitabu hiki New York juma lile lile kilipotoka na kwa bahati mbaya mwandishi alifarika kabla ya kukizindua kitabu.

Kitabu cha Alex Hailey nimekisoma nikiwa na miaka 15/16 sekondari na vijana wengi tulimpenda kwa ajili ya ule msimamo wake mkali.

Leo naona hapa vijana mnazisifia hotuba za Malcolm X.

Kwangu mimi mnanikumbusha ujana wangu.

Nimefika katika mitaa ya Malcolm X 125th Street, Harlem na nimeona pia ule ukumbi Audibourn Hall alipopigwa risasi.

Spike Lee ametengeneza movie ya maisha ya Malcolm muigizaji Denzel Washington ikiwa hujaiona itafute.
 
Nimekuwa nasoma biography ya Malcom X. Huyu mtu alikuwa wa pekee sana. Hapa nataka kuzungumzia hii hotuba yake(The ballot or the Bullet) ukweli sijawahi sikia hotuba yenye nguvu namna hii.

Hotuba nyingi bora huwa za kujifanya tu, wanasiasa wakitumia maneno makubwa, wakiongea wanayotaka watu tu. Si hotuba hii. Hii hotuba aliyeitoa anamaanisha. Hotuba hii inamaana hata leo hii, hata kwa nchi yetu.

Ikitafisiriwa Kiswahili labda wengi wangeelewa na kufunguka kiakili
 
Huyo jamaa ilikua deluded na mafundisho ya National of Islam,akaaminishwa adui yake mkuu ni mzungu na ukristo,
 
Lycaon...
Kitabu cha Marable Manning kimefanya kile kilichotakiwa.

Nimekinunua kitabu hiki New York juma lile lile kilipotoka na kwa bahati mbaya mwandishi alifarika kabla ya kukizindua kitabu.

Kitabu cha Alex Hailey nimekisoma nikiwa na miaka 15/16 sekondari na vijana wengi tulimpenda kwa ajili ya ule msimamo wake mkali.

Leo naona hapa vijana mnazisifia hotuba za Malcolm X.

Kwangu mimi mnanikumbusha ujana wangu.

Nimefika katika mitaa ya Malcolm X 125th Street, Harlem na nimeona pia ule ukumbi Audibourn Hall alipopigwa risasi.

Spike Lee ametengeneza movie ya maisha ya Malcolm muigizaji Denzel Washington ikiwa hujaiona itafute.
Utakuwa unamfahamu vyema sana, nitatafuta hiki cha Manning nijazilizie. Kumsoma kunakufanya utamani uijue mitaa ya Harlem, uijue suti ya zoot na Lindy Hopping ni nini. Nimeona movie yake, lakini nilikuwa sijawahi kumsoma wala sijawahi kusikia hotuba na interviews zake. Simjui Dr. King kwa undani lakini niseme kuwa Malcom X alikuwa zaidi ya Dr. King. Nafikiri tunahitaji movie yake nyingine au hata series yake kabisa, series itakuwa nzuri sana.
 
Huyo jamaa ilikua deluded na mafundisho ya National of Islam,akaaminishwa adui yake mkuu ni mzungu na ukristo,
Pengine mwanzoni mwa maisha yake. Ukimsikiliza kwenye hotuba zake alizotoa mwishoni-mwishoni mwa maisha yake, alipojitenga na National of Islam anasema kuwa dini yake bado ni Islam(Wakati huo akifuata Orthodox Islam) lakini dini yake ni kati yake na Mungu wake, falsafa yake ni Black Nationalism.
 
Wewe jamaa haujui kitu unaropoka bila kufuatilia mambo jinga kabisa.

Malcom maisha yake katika harakati za kisasa yana two phases .Phase one wakati yupo National of Islam(NOI) ambao unaweza kuuita uislamu fake yeye na wenzake wakawa na mahubiri ya chuki.

Phase two ni baada ya kwenda kuhiji Makka na kuwa muislamu wa kweli hapa akawa anahubiri umoja na akaanzisha organization yake ya Afro-american hii ikawa na watu wote bila kujali dini ,rangi nk hapa ndipo Malcom akapendwa na watu wote ,na alikuwa na washirika wengi hata wasio waislamu.

Kwa uelewa zaidi tafuta hotuba yake ya Ballot or Bullet na Lycaon pictus ameleta uzi wenye hotuba hiyo ambayo ibataka umoja wa dini zote na mengineyo.
 
Pengine mwanzoni mwa maisha yake. Ukimsikiliza kwenye hotuba zake alizotoa mwishoni-mwishoni mwa maisha yake, alipojitenga na National of Islam anasema kuwa dini yake bado ni Islam(Wakati huo akifuata Orthodox Islam) lakini dini yake ni kati yake na Mungu wake, falsafa yake ni Black Nationalism.
Huyo jamaa anatabia ya kuongea kitu pasipo kuchunguza , Malcom X wakati wa mwisho baada ya kutoka NOI mitizsmo ya chuki na kibaguzi aliifuta.
 
Huyo jamaa unatabia ya kuongea kitu pasipo kuchunguza , Malcom X wakati wa mwisho baada ya kutoka NOI mitizsmo ya chuki na kibaguzi aliifuta.
Na ndiyo maana nasemaga ujumbe ambao Malcom X aliiachia dunia ni upendo. Sema wengi wanataka kumpaka matope kwa makusudi, kwa kupotoshwa au kwa kutomuelewa vizuri..
 
Lycoon...
Unasoma kitabu kipi cha Malcolm X?
Malcokm X ana vitabu viwili maarufu kuhusu maisha yake.

Kipo alichoandika Alex Hailey ''The Autobiography of Malcolm X (1964) alichoandika Manning Marable, ''Malcolm X Life of Reinvention,'' (2011).

Kitabu cha Hailey kilitoka baada ya kifo cha Malcolm X na inasemekama kuwa Hailey alibadilisha mambo mengi baada ya kuona Malcolm hayupo tena duniani.

Hiki ngoja nikisearch kama nitaweza kukipata mtandaoni Pdf bure.Maana kununua vitabu mtandaoni kama Amazon sio mzoefu na nahofia bei inaweza kuwa kubwa nisiimudu.

Ninavyojua Halley kuna baadhi ya vitu amevitoa hata yeye amekiri hilo ila kiujumla kitabu chale kuzuri kineCover mambo mengi muhimu zaidi kuhusu Malcom X pamoja na kasoro hiyo.

Kuna kingine hiki nacho nakitafuta ni kipya ambacho rafiki yake wa ndani yule Shorty akimzungumzia Malcom X ,kina mambo mengi ambayo huwezi kukuta kwenye vitabu vingine.
images (2).jpeg

Kuna hiki nacho ni moja Kati ya vitabu maarufu kuhusu Malcom X nimekisoma na ninacho ni kuzuri mno utapata vitu vingine vizuri zaidi.

download.jpeg
 
Utakuwa unamfahamu vyema sana, nitatafuta hiki cha Manning nijazilizie. Kumsoma kunakufanya utamani uijue mitaa ya Harlem, uijue suti ya zoot na Lindy Hopping ni nini. Nimeona movie yake, lakini nilikuwa sijawahi kumsoma wala sijawahi kusikia hotuba na interviews zake. Simjui Dr. King kwa undani lakini niseme kuwa Malcom X alikuwa zaidi ya Dr. King. Nafikiri tunahitaji movie yake nyingine au hata series yake kabisa, series itakuwa nzuri sana.
Movie inaitwaje niitafute kesho?
 
Back
Top Bottom