Sijawahi kuvielewa Viwanja vya futi 50 x40 kwa ajili ya makazi

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
4,118
Reaction score
9,864
Ndugu wanabodi.

Kuna utitiri wa uuzaji wa viwanja vidogo sana kwa bei inayoanzia laki nane mpaka milions kadhaa.

Nikipiga hesabu futi 50 kwa 40 hapo utajenga nini. Au tunaenda kutengeneza vingunguti nyingine.

Ushauri wangu kama huna hela ambayo unaweza kupata robo au nusu heka.hapa mjini kwa ajili ya makazi bora hata hiyo hela ukanunue hekari moja huko mkoani utulie.

Nyumba ya makazi inatakiwa iwe pana na nafasi ya kutosha siyo kubanana hata pakutemea mate huna

Kumbuka makazi hayakuingizii faida yoyote. Sasa kiwanja.hakitakiwa kuwa expensive hivyo. Ila.kama unachukua hivyo viwanja kibiashara hapo sawa maana ni vidogo mno afu bei ni.kubwa sana.

Haya makampuni yanafanya biashara ili yakanunue maeneo makubwa zaidi.ili wakuja waje wapimiwe tena. Bora hata wewe ukaenda huko ndani ndani mkuranga ukajipatia.hata hekari moja aridhi ni mali .

Usisahau aridhi ya Tanzania ni mali ya JMT kwa hiyo hata kuuziana viwanja vya makazi kwa kukomoana ni wizi tu
 
Nchi hii ni ndogo sana kwa population iliyopo na ijayo. Mkitaka viwanja vikubwa kwa kila mtanzania, hata idadi iliyopo sasa hivi hatutapata wote. Ardhi siyo kwa kujenga nyumba pekee kuna matumizi mengine, tukubali hicho kidogo tugawane tusonge mbele.

Mkitaka makazi bora siyo ukubwa wa viwanja tu, kuna mpangilio wa majengo na ubora wa majengo yenyewe, na mahitaji mengine.

Tuache ujenzi holele, serikali itoe tender kwa kampuni za nje watujengee kwa mpangilio tununue. Lakini hii ya kila mtu anajijengea kivyake, hata ungejenga ghorofa Vingunguti, bado unakuwa wa vingunguti tu.

Kumbuka pia kuna vile vya 20 x 20 huku kwetu tunaita jirani mwema.
 
Hapo inakusudiwa utunzaji wa mazingira.kwa ukubwa huo,mtapanda miti kuzunguka viwanja vyenu na kuendeleza ukijani kama ulivyokuwa kabla ya viwanja kugaiwa. kipimo cha 20 x 20 ni standard ya uingereza kwa kuwa wao wana ufinyu wa eneo
 
Ila.mkoani napakubali sana hasa kwa mipango miji..kuna.maeneo barabara zinachongwa na halimashauri kabla.watu.hata kujenga hawajaanza
 
Zingatia space standards za Serikali Kiwanja Kidogo ni 90 SQM.Hicho cha 50 Kwa 30 ni kama 150 SQM.Cha Mhimu kuwepo na Barabara Pana, miundombinu ya Maji Safi na majitaka na pia Umeme.Viwanja vya Karikaoo na Sinza vingi ni 288 Hadi 300 SQM na Watu wanaishi.Kumbuka Kariakoo ilipangwa na Mkoloni Mjerumani kisha Waingereza wakapita humo na baada ya Uhuru tunaendelea.Any way Wakati wa kupanga Miji kuna Viwanja Low density,medium density na high density.Waweza kujichagulia size yako kwa kadri ya uhitaji na uwezo wako.Zingatia size za viwanja zinatofautiana baina ya Nchi.Makazi ya Kawaida hata SQM 400 unaishi vizuri Tu,Nyumba,Maegesho,swimming ukiipenda,na bustani.
 
Nchi hii ni ndogo sana kwa population iliyopo na ijayo. Mkitaka viwanja vikubwa kwa kila mtanzania, hata idadi iliyopo sasa hivi hatutapata wote. Ardhi siyo kwa kujenga nyumba pekee kuna matumizi mengine, tukubali hicho kidogo tugawane tusonge mbele.

Mkitaka makazi bora siyo ukubwa wa viwanja tu, kuna mpangilio wa majengo na ubora wa majengo yenyewe, na mahitaji mengine.

Tuache ujenzi holele, serikali itoe tender kwa kampuni za nje watujengee kwa mpangilio tununue. Lakini hii ya kila mtu anajijengea kivyake, hata ungejenga ghorofa Vingunguti, bado unakuwa wa vingunguti tu.

Kumbuka pia kuna vile vya 20 x 20 huku kwetu tunaita jirani mwema.
Mbona mm nimenunua 12 kwa 14 na sisemi
 
Mipango miji wamelala usingizi wa pono
 
Kuna hela ya udalali niliotea ghafla badala ya kuichezea nikaamua kutafta kipande cha ardhi niliangukia huko kwa 50*40 ila niliunganisha viwili angalau kaeneo kakawa na muonekano. Natafta mtu nimveshe nikanunue eneo kubwa next year.
Kisemvule au Kibaha?
 
Ndugu wanabodi.

Kuna utitiri wa uuzaji wa viwanja vidogo sana kwa bei inayoanzia laki nane mpaka milions kadhaa.

Nikipiga hesabu futi 50 kwa 40 hapo utajenga nini. Au tunaenda kutengeneza vingunguti nyingine.

Ushauri wangu kama huna hela ambayo unaweza kupata robo au nusu heka.hapa mjini kwa ajili ya makazi bora hata hiyo hela ukanunue hekari moja huko mkoani utulie.

Nyumba ya makazi inatakiwa iwe pana na nafasi ya kutosha siyo kubanana hata pakutemea mate huna

Kumbuka makazi hayakuingizii faida yoyote. Sasa kiwanja.hakitakiwa kuwa expensive hivyo. Ila.kama unachukua hivyo viwanja kibiashara hapo sawa maana ni vidogo mno afu bei ni.kubwa sana.

Haya makampuni yanafanya biashara ili yakanunue maeneo makubwa zaidi.ili wakuja waje wapimiwe tena. Bora hata wewe ukaenda huko ndani ndani mkuranga ukajipatia.hata hekari moja aridhi ni mali .

Usisahau aridhi ya Tanzania ni mali ya JMT kwa hiyo hata kuuziana viwanja vya makazi kwa kukomoana ni wizi tu
Foot 50 kwa foot 40 ni sawa na mita 17 kwa mita 13. Hiki ni kiwanja kidogo mno. Standard ni mita 20x20
 
Nyumba kubwa ya 3 bedroom ni 9×12 so inafit in sema hutakuwa na extra space. Ndio maana itakubidi aidha ununue viwili ili uwe na nafasi ya parking na mabanda uwani
Mkuu sio kidogo, mm ninacho kimoja ni 15 kwa 15 mita. Ni kikubwa tu kisela sela mtu mjini anaishi fresh. Chumba kimoja kin mita 3 kwenye 15 unatoa vyumba vinne na choo fresh tu
 
Back
Top Bottom