Sijawahi kuvielewa Viwanja vya futi 50 x40 kwa ajili ya makazi

Sijawahi kuvielewa Viwanja vya futi 50 x40 kwa ajili ya makazi

Nchi hii ni ndogo sana kwa population iliyopo na ijayo. Mkitaka viwanja vikubwa kwa kila mtanzania, hata idadi iliyopo sasa hivi hatutapata wote. Ardhi siyo kwa kujenga nyumba pekee kuna matumizi mengine, tukubali hicho kidogo tugawane tusonge mbele.

Mkitaka makazi bora siyo ukubwa wa viwanja tu, kuna mpangilio wa majengo na ubora wa majengo yenyewe, na mahitaji mengine.

Tuache ujenzi holele, serikali itoe tender kwa kampuni za nje watujengee kwa mpangilio tununue. Lakini hii ya kila mtu anajijengea kivyake, hata ungejenga ghorofa Vingunguti, bado unakuwa wa vingunguti tu.

Kumbuka pia kuna vile vya 20 x 20 huku kwetu tunaita jirani mwema.
Jirani akiachia ushuzi unaanza kugombana na mwenza wako ukijua ni yeye
 
Hii nchi bado iko vizuri. Wananchi wengi bado wanaweza kununua viwanja
 
Kama mm nina plan ya kujenga chumba na sebule tu kama hivi bas. Nitaki mita za skwea 2400 za nn? Yani mita 10 kwa 10 tu tukutane kariakoo mambo yasiwe mengi
20241106_134220.jpg
 
Nchi hii ni ndogo sana kwa population iliyopo na ijayo. Mkitaka viwanja vikubwa kwa kila mtanzania, hata idadi iliyopo sasa hivi hatutapata wote
We jamaa umetembea kweli hii nchi? Ni ndogo kwa idadi yetu?
 
Zingatia space standards za Serikali Kiwanja Kidogo ni 90 SQM.Hicho cha 50 Kwa 30 ni kama 150 SQM.Cha Mhimu kuwepo na Barabara Pana, miundombinu ya Maji Safi na majitaka na pia Umeme.Viwanja vya Karikaoo na Sinza vingi ni 288 Hadi 300 SQM na Watu wanaishi.Kumbuka Kariakoo ilipangwa na Mkoloni Mjerumani kisha Waingereza wakapita humo na baada ya Uhuru tunaendelea.Any way Wakati wa kupanga Miji kuna Viwanja Low density,medium density na high density.Waweza kujichagulia size yako kwa kadri ya uhitaji na uwezo wako.Zingatia size za viwanja zinatofautiana baina ya Nchi.Makazi ya Kawaida hata SQM 400 unaishi vizuri Tu,Nyumba,Maegesho,swimming ukiipenda,na bustani.
Kwa taarifa yako Dar mipango.mini ni ya bovyo.. ukitoa.baadhinl ya meneo machache. Miaka ijayo huko wanaponunua 15 x12 i majanga tupu hata sehemu yanm kumwaga.maji hupati.maana wengi wao ni wa vipatamo vya chinj na seriakli bado haijapitisha miundo mbinu yake
 
Back
Top Bottom