Sijivunii wazazi wangu

Pole sana mkuu hii ndo Dunia
 
PART TWO (SIJIVUNII KUWA NA WAZAZI WANGU)
Simu zinapishana kila mzazi (baba na mama) analia na shida yake, Huyu anataka hela ya kufanya hili na Huyu anataka hela ya kufanya vile... Wanaemuomba hizo hela sasa, Yupo mjini na hana shughuli ya maana, Anawaza kesho yake asijue ipo vipi huku bado ana wazazi wawili na kila mmoja akimvuruga kichwa kwa mahitaji yake.

Wazazi wa wazazi waliwaachia wazazi wangu urithi ila amini usiamini sina chochote cha kurithi kutoka kwao zaidi ya mimi mtoto kufanya wazazi warithi kitu kutoka kwangu.

Ni lini mimi nitaoa na kuanza kufiri maisha ya wanangu ikiwa kufikiri juu maisha yangu kunawekwa ugumu na maisha ya wazazi wangu?

Eeh Mungu wangu nisaidie.
 
Pole sana, unatakiwa kujiombea kuvunja hizo roho za kutumika vibaya na wazazi wako, Kuna watu wanaitwa dunia Haina huruma Sasa hao watu kazi Yao nikubebesha mizigo Yao kwa wengine ili wao wawe wepesi, hao watu wanaweza kuwa wazazi, watoto, ndugu, marafiki au hata jamii yoyote wao kazi nikutumia wengine bila huruma, Sasa hapo muombe Mungu akuondolee Hilo vazi la kutumika vibaya, kikubwa upende kuwa mtu wa haki ili unapoomba maombi yako yajibiwe, pia Anza Sasa kujiombea wewe na kufanya kazi kwa bidii kwaajili ya watoto wako na wajukuu zako bila kufikiria Kuna mtu atayabadilisha maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…