Sijivunii wazazi wangu

Sijivunii wazazi wangu

MTU akifanya upumbavu unataka aitwe Mwenye hekima?
Hizi dini zimefundisha Watu unafiki WA kiwango kikubwa Sana.

Yaani Mimi Kwa vile ni Baba nikifanya upumbavu unataka Watoto wangu wanione ninahekima?
Watoto wangu sitawafundisha unafiki.
Baba Yao nikizingua wajue nimezingua, na wewe na uwezo wa kuniambia Mzee hapo umepuyanga. Nami niombe Radhi ikiwa kweli nimekosea.

Sio hizo hadithi za kijinga jinga, zakinafiki, zakizamani, zakitumwa, zakufanya Watu miungu Watu.
Imagine
 
Kama mtu hajawahi kupitia hiyo hali hata kwa udogo hawezi kuelewa jinsi we unaumia.

Mtu ambae wazazi wake ndio backup yake, mtu ambae mzazi wake ndio kaplay/anaplay part kubwa kwenye mafanikio yake hawezi kuelewa zaidi zaidi ataona wewe ni mtukutu, una kiburi, hupendi wazazi wako, hujitumi (mvivu) nk.

Lakini wanasahau wazazi nao ni binadamu, hii story yako ungeitoa wewe uwe kama third part tu(msimuliaji) , ungeona wadau jinsi ambavyo wangewananga hao wazazi wa kijana. Ila kwakua wewe ni wazazi wako basi wanacomment kwa hisia as if unawasema wazazi wao pia.

Mpaka umefikia kuandika hapa basi una njia zako za kuwamudu, washukuru kwa kukuzaa ila kuhusu kujivunia kua nao sidhani kama inamatter sana. Kama wewe hujivunii kua nao basi wafanye wao wajivunie kua na wewe.
Waambie hali halisi jinsi unavyohisi wakikutolea maneno machafu, tena uwaambie kipindi huna hasira.
 
Huwa hatuhesabu tulipotoka, mama wa kambo ambao ni watu wazima wanaisoma namba watoto waliowatesa leo wapo juu aibu kwao, mifano ni mingi.
Kuzaliwa masikini sio kosa lako bali kufa masikini.
 
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu? Au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?
Mjomba hakuna alieko kwa ajili yko dunia hii we chamsingi pambana umiliki utawala wako ila chunga sana kwenye kutafuta wa kuanza nae familia ili kuepusha kuja kutesa watoto wako
 
Waheshimu baba na mama yako upate heri na baraka ...
Me wangu nawaheshimu sana yanii sana mno maana walijua wajibu wao kwetu kama watoto na wakautimiza hawakuzaa kama mbwaa wakatutelekeza... hata leo wanatupa moyo kwenye magumu tusikate tamaa sio wazazi wa huyu jamaa.
 
KABLA YA KUANDIKA COMMENT YAKO ZINGATIA KWAMBA HAKUNA ANAEPENDA KUWEKA WAZI BACKGROUND YAKE YA NYUMA IJULIKANE HASA KAMA SIO NZURI, UKIONA MTU ANAIWEKA WAZI MEAN KWAMBA IMEBIDI TU HAINA JINSI, SO NAANDIKA KUHUSU HAYO YOTE ILI WATU KUELEWA SITUATION NZIMA ILI UKITOA USHAURI MAYBE AU MAONI YAENDANE NA MAISHA YANGU KIUJUMLA. So, Kuandika kuhusu mama yangu kuwa single maza, Au baba kuishi kwa bibi yangu mean kwamba naiweka hivyo ili mjue situation nzima na sio kulaumu au kuwavunjia heshima maana nawaheshimu na kuwapenda sana ila jinsi walivyonitreat au wanavyonitreat hakufanyi nijivunie wao.
Mimi nimekuelewa sana tu
 
Mimi nimekuelewa sana tu
hamna kitu kigumu kama kupambania kesho ya wazazi, kesho yangu, na kesho ya watoto wangu... though inawezekana maana hakuna linaloshindikana ukimuamini Mungu ila inauma ukiona wale unaojaribu kuwapambania wanapoonyesha kutokujali.
 
Dunia ya ckuiz imejaa deadbeat fathers & deadbeat mothers.

Mtoa mada Ni Mmoja tu Kati ya wengi waliotelekezwa na wazazi wao na wakawa na maisha magumu kupitiliza.

Anyways, mi nakushauri upambane tu Wala usiwawekee kinyongo wazazi wako.Muombe Sana Mungu akufungulie njia I'll uweze kufanikiwa mkuu.
 
th
Dunia ya ckuiz imejaa deadbeat fathers & deadbeat mothers.

Mtoa mada Ni Mmoja tu Kati ya wengi waliotelekezwa na wazazi wao na wakawa na maisha magumu kupitiliza.

Anyways, mi nakushauri upambane tu Wala usiwawekee kinyongo wazazi wako.Muombe Sana Mungu akufungulie njia I'll uweze kufanikiwa mkuu.
thank you man
 
Usikate tamaa kijana.ipo siku watoto wako watafurahia kuwa na baba na mama bora. Endelea kupambana Mungu atakusaidia.
 
Nakubaliana na wewe kabisa. Kama vipi bora usiwazae. Kwani walikuomba uwazae ili uwatese. Asee Mungu atuwezeshe na atupe hekima tupiganie uzao wetu

Mi baba angu ukiwa unaonewa na ndugu zake anakaa kimyaa badala ya kunitetea
Siku moja nikauwasha motooo nikamuwashia na yeye kwanin hawezitetea mwanae alaaa
 
Mi baba angu ukiwa unaonewa na ndugu zake anakaa kimyaa badala ya kunitetea
Siku moja nikauwasha motooo nikamuwashia na yeye kwanin hawezitetea mwanae alaaa
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Maza pia alikuwa hivyo ila nilijua tu ananipenda sema kubalansi ndugu zake na mtoto ilikuwa tatizo. Sema ndugu zake walikuwa hawawezi kutotetea watoto wao
 
Mi baba angu ukiwa unaonewa na ndugu zake anakaa kimyaa badala ya kunitetea
Siku moja nikauwasha motooo nikamuwashia na yeye kwanin hawezitetea mwanae alaaa
😁😁😁 utaambiwa ni laana umemvunjia heshima mzazi.
 
Back
Top Bottom