Sijivunii wazazi wangu

Sijivunii wazazi wangu

Ulitaka wakaibe wakupe maisha?? Kama wao tu hawajiwezi kwanini utake kupewa msaada wewe? Aise...
Wewe baba yako akikutukana kisa umekosa hela ya kumpaa unajisikiaje??? Wazazi wengine vimeoo tuu huo ndio ukweliii...
 
Nafikiri kwasasa haupaswi kulaumu kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako. Zaidi ebu libebe kama fundisho ili nawewe usije ukarudia kosa hilo kwa watoto wako.... lakini pia sio vyema mtoto kumnenea vibaya mzazi wake hata kama mzazi anakasoro tayari ni mzazi wako na ndio maana halisi ya kuvumiliana.
Vipo vya kuvumilia ila sio Mzazi kumtukana mwanae kisa hana helaaa ya kukusaidiaaa... Hao ni wazazi wapumbavuuuu
 
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu? Au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?

Haya mawazo yanakutesa wewe na sio wao, achana nayo kabisa, wasamehe, wapuuze, na huwajibiki kutumwa kwao hat 1000. Usiseme hukuambiwa.
 
Mambo ya baba, mama na mtoto ni yametengenezwa tu na jamii tunazoishi. Hayana uhusiano wowote kimwili Wala kiroho; ukizaa ndo umemaliza tu, uliyemzaa halazimika kumtambua aliyemzaa. Ndiyo maana wazazi wengine wanatumia muda na ngunvu nyingi kuwaaminisha watoto wao kuwa wamewazaa kwa jina la malezi. Wewe chapa kazi, hakuna kitu kinakufunga eti Kwa jina la wazazi. Nasema chapa kazi.
 
Me sijakutukana na wala siwezi kutukana mtu ambae simjui mkuu sifahamu umri wako wala unapotokea, Kiufupi wewe ndo umekuja kwenye uzi wangu kujaribu kunipinga na sijakulazimisha uniunge mkono maana pia haitosaidia chochote, ila kwa comments zako me nakuambia sijakuelewa hata kidogo vitu unavyoviandika naona kama vimekaa kulazimisha mtazamo wako uwe wangu ila haiwezi kuwa hivyo maana nimegundua bado kuna code umeshindwa kufungua kwenye uzi wangu... Unachonishauri mimi nakijua kabla ya kuanza kuandika kichwa cha uzi huu na nilitegemea pia kukutana na comments kama zako..... Advice yangu ni kwamba kama wewe ni aina ya wazazi wangu basi jitahidi ubadilike mapema.
Pole kwa maumivu uliyo nayo.

Umeleta uzi wako jukwaani jitahidi usome ukiwa positive, tarajia maoni tofauti,anaetoa ushauri usioupenda usione kuwa anakupinga au hajakuelewa.
Nimeona unafurahia comments zile tu zinazolaumu wazazi, yes wazazi huwa wanakosea sababu nao ni binadamu.
Naunga mkono alichosema Ushimen.
Mungu akuondolee maumivu uliyo nayo moyoni uwe huru.
 
Mimi nafikiri haya umeyaandika ili upate kuuponya moyo na kupunguza maumivu.
Kama umefikiri hivyo,muache Basi Basi apunguze maumivu kuuponya Moyo wake...kuanza kumpa maelezo mengi nahisi utamuongezea maumivu
 
Vipo vya kuvumilia ila sio Mzazi kumtukana mwanae kisa hana helaaa ya kukusaidiaaa... Hao ni wazazi wapumbavuuuu
Ni kweli mkuu.[emoji817][emoji817][emoji817]

Mtu mjinga na mpumbavu akiwa mzazi, HAIFANYI ujinga wake kuisha Akilini.

Watu wajinga na wazazi wazembe wanataka kutumia kigezo cha "Uzazi" kama defence mechanism (silaha ya kujilinda) na uzembe wao pamoja na ujinga...

Hakuna kulea kujinga let them reap what they sow!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu? Au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?
Hakuna slope babuu pambana
 
Kamwambie baba /mama yako kwamba ungeweza kuzaliwa na couple nyingine yoyote duniani halafu utuletee mrejesho! Au mwanao akwambie hivyo utajiskiaje? HESHIMU WAZAZI UNA DNA ZAO [emoji120]
Ndio ingewezekana kabisa kuzaliwa na couple nyingine, Haikuwa lazima iwe wao..

Hapa najibu kwa hoja sio Hisia... ukweli ni kwamba wazazi walikuwa kwenye starehe na raha zao tu wala hawakujua kwamba ningezaliwa mimi.

Ni mipango ya Mungu tu, kufahamu mtu fulani atazaliwa na couple gani...wala sio lazima kwamba eti kulikuwa na ulazima wa wewe kuzaliwa na hiyo couple...

Nachojaribu kukwambia hapa ni kwamba wazazi wasi watishie wanao na kuwanyanyasa kwa kigezo cha"Uzazi" na kukitumia kama defence mechanism ya kuficha ukweli wa uzembe na ujinga wao.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Kwani mkuu, kwanini mleta mada asinge amua kubadilisha then akuwe na wazazi wa vile anataka, kwani shida ingekua wapi??
Hawezi kuwabadilisha awe na wazazi anao wataka...

Lakini pia hichi sio kigezo cha kufanya mleta mada ashindwe kuzungumzia Uzembe wa wazazi wake..

Kushindwa kuwabadilisha wazazi wake awe anavyo taka, Sio Kigezo wala defence mechanism ya kutetea "uzembe wa wazazi" ....

Naona wewe unatumia Asili(nature) kwa vile haibadiliki kutaka kumwambia mleta mada Awasifiee tu, Licha ya kwamba walikuwa wazembe...

Yani unataka hata mzazi awe mzembe au mjinga basi mtoto anapaswa Kumsifu na kumsifia tu, kitu ambacho ni ujinga na kinalea na kutetea ujinga....

Mzazi anastahili kukosolewa kwa Uzembe wake,Sio asifiwe tu eti kwa vile huwezi kumbadilisha..!!! Utakuwa ni ujinga wa hali ya juu....

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mie kwa mtazamo wangu naona mtoa mada .. sio kwamba analaumu wazazi au kutoheshimu wazazi.
Ni kwamba anatoa maumivu anayopitia kutoka kwa wazazi

wangapi n wazazi maskini lakini anakaa kwa upendo na mtoto mpaka mtoto anaona mzazi wangu pamoja na umaskini ila kanilea kwa upendo na anamwombea mwanae apate na anashukuru anachotumiwa.

Sasa wewe hujamlea mtoto kiupendo pia bado unajua kwa umri huu mwanangu angetakiwa kuwa shule ila kaamua apambane na maisha.. kwanini usimpe support kwa maneno ya upendo ,faraja na kumuombea apate zaidi.

Ila wanachofanya wazazi wa huyu kijana ni ubinafsi na kutojali ndo kinachoumiza zaidi sio umaskini...
Ifike muda mzazi utake responsibility ya matendo yako.

Haya huyo baba ye mbona hana msaada kwa mama yake ..mpaka analelewa na mzazi wake tena mzee..hamuoni kuwa ye ndo anamatatizo.

Kijana endelea kupambana.. saidia unapoweza usipoweza usijiumize.
Mwenyezi Mungu anajua dhamira yako kuliko sie binadamu.
 
Mtu anazaaa ili asichekwe na jamii lkn deep down hana mapenzi na huyo mtoto / watoto...what a waste![emoji848]
So sad kwa kweli, Hao ndio wazazi wajinga ninao wazungumzia....

Mtu anakurupuka huko kuleta kiumbe duniani hajui atamhudumia vipi,hajui atamleaje, hajua atavaa nini,

Mwisho wa siku anakimbia majukumu na kumtelekeza mtoto...

Mtoto anakua kwa tabu, Anapambana kweli kweli mwisho wa siku anatoboa na kufanikiwa...

Mzazi yule yule mkwepa majukumu anakurupuka kutoka kusikojulikana ana anza kutumia "Uzazi" kama defence mechanism (silaha ya kujilinda) kuficha Uzembe na ujinga wake kumsumbua mtoto...

Hii haikubaliki kabisa na sio sahihi... wazazi wazembe sio wa kuwasaidia hata senti moja!! Ni kuwaacha wavune walicho panda na wao waonje joto la jiwe...

Principle ya dunia ni moja "You will reap what you sow"....wala hakuna kulea ujinga.never!!!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Umefika fomu foo bado unataka wakubebe wawe wanatembea na wewe huko mjini.

Pambaneni huko na msisahau kuleta pesa kwa wazazi.
 
Mzazi ni mzazi hata kama alikutupa jalalani wasamaria wema wakakuokota. Samehe patana nae, let the universe decide.
 
Mzazi wako unamwita mzembe aloo [emoji15][emoji15], natamani mzee wangu angekuwepo asee
Mtu kuwa mzazi sio kigezo cha kwamba hawezi kuwa mjinga!!!

Pia mtu mjinga kuwa mzazi HAIFANYI ujinga wake kuisha Akilini...

Mzazi kuwepo ama kutokuwepo ni sawa maana kifo ni njia yetu sote...

Uzembe wa mzazi lazima usemwe haijalishi yupo hai ama huyupo hai kama alikuwa mjinga na mzembe ukweli utabaki ndio huo.....

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mzazi ni mzazi hata kama alikutupa jalalani wasamaria wema wakakuokota. Samehe patana nae, let the universe decide.
Hii kauli yako ni defence mechanism (silaha ya kujilinda) kwa wazazi wazembe wasiowajibika kuficha Uzembe wao na ujinga....

Mzazi akutupe jalalani abaki kuwa mzazi.Huyo ni mzazi Jina tu na mzazi wa kibaiolojia tu...

Ila huyo mzazi anakuwa ni mjinga, mwehu na mpumbavu na wala hastahili heshima ya kuitwa mzazi..

Ova!

Back
Top Bottom