Sijivunii wazazi wangu

Sijivunii wazazi wangu

Sasa wewe ushajitambua anzia hapo kuweka mambo sawa kwa kizazi chako...Wengi wazazi ni chenga ..

Kuna somo hapo nimeona sidhani Kama karma pia inaweza kukurudia we nenda mbele kwa mbele ,kama sijakosea hata kuwasalimia mara nyingi huendi ila sio kwamba hupendi basi ni changamoto tu za maisha.

Piga moyo konde wengi hawataki kurudi kwao na kutokana na matatizo kama hayo yako ..pambana
 
kuna ule msemo

"unazaliwa bira ridhaa yako ila kesho ya maisha yako n ujipambanie mwenyewe"
🤣🤣🤣🤣 only encounter from Africa ...Kuna kipind watu watawafungulia wazazi wao kesi kama wale wahindi na wazungu.
 
Jamani,tajiri mmoja ajitolee kunioa Mimi single mom,nikimbie matusi ya wanangu huko mbeleni.Daaa ,sikulaumu ni kosa letu kuwaleta duniani ingali hatujakaa vyema kiuchumi😭😭😭😓 aisee
20221202_060249.jpg
 
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu? Au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?
Pole sana mkuu ila make sure watoto wako hawaji kukulalamikia namna hii

Hiyo laana iishie kwako
 
Usimtukane wala kumtanzaga mama yako (eti singo mama).

Usimseme vibaya baba yako kwasababu bado anaishi kwa wazazi wake na hajafanikiwa kutoboa maisha.
Hao bado ni wazazi wako (haijalishi hata kama wangelikua vichaa)
Hajawasema ila ameongea ukweli tu

Ni kweli mama yake ni Single mom
Na
Ni kweli baba yake hana nyumba anaishi kwa mama yake


Huu ni ukweli hajasemwa mtu
 
Mkuu unajua kwenye maisha mtu akieleza hisia zake za kuumia usilinganishe na za mtu mwingine watu tunatofautiana mioyo so, lengo la huu uzi wangu ilikuwa ni kutua ya moyoni mwangu sio kutoa ya moyo wa mwingine, sijasema mimi nina situation mbaya kuliko wengine ila kwa kiasi changu hapo imefika nimeona niandike humu maana nobody knows me, nobody knows my parents pia.

So inabaki kama slogan ya Jf isemavyo "A place where we dare to talk" ila ahsante kwa maoni yako pia ya kujaribu kuonesha kwamba hii issue ni ndogo sana kwako inanipa moyo pia.
Binafsi I appreciate hiki ulichokifanya, kusema yanayokusibu ni hatua moja ya kukuponya
Pole na hongera sana mkuu
 
Si bora wewe ulisomeshwa mpaka form four! Wengine wamezaliwa wakaishi kwao kama gerezani hakuna amani, ni fujo mwanzo mwisho Matokeo yake watoto wanakimbilia kujitegemea mitaani wakiwa bado wadogo kiumri, Hata hivyo shukuru maana kwenye maisha kuna mambo yanatokea na usiweze kuzuia lolote.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Duh ndefu

Ila pole kwa masahibu.
Mwaka huu naacha pombe nilee wanangu vizuri 🤪🤪🤪 wasijenilaumu huko mbeleni
 
Nitoe shule kidogo!
Mahitaji muhimu kwa binadamu ni Chakula (food), malazi (shelter) na mavazi (clothes) ,ukiwa tumboni yote uliyapata kwa mama yako!

Tuseme basi kakutelekeza ukiwa mdogo haibadili ukweli hapo juu.

Unachopaswa kufanya ni kumheshimu na kumuombea unapoweza msaidie. Ni hayo tu
Kama hakukuwekea misingi imara ya maisha utamsaidia nini? Waafrika tuache upumbumbaf eti kuombeana,iko hivi,kama hukufanya/hufanyi juhudi zozote kutayarisha maisha yako,maombi yatakuwa nonsense.
 
Fuatilia sheria za USA au Europe kuhusu watoto ndo utajua hapa kwetu tunafanya mizaha sana.
Yaani waafrika ni wajinga sana,wanaona mzazi kumnyima haki mtoto ni Sawa,Ila mtoto kulalamika haki kutoka kwa mzazi au mapunngufu ya mzazi,eti ni kutoheshimu wazazi 🚮
 
Yaani waafrika ni wajinga sana,wanaona mzazi kumnyima haki mtoto ni Sawa,Ila mtoto kulalamika haki kutoka kwa mzazi au mapunngufu ya mzazi,eti ni kutoheshimu wazazi 🚮
Mwaka jana Ferre Gola alifungwa miezi mitatu Ufaransa kwa kosa la kumpiga mwanae. Mtoto alienda kushtaki. Ferre akala mvua ya miezi mitatu.
 
Umejawa na manung'uniko sana hata hizi baraka zitaingilia mlango upi, kila mtu akimtafuta wa kumuangushia jumba bovu humu hakutatosha,,

Huna shukrani kabisa shenzi
 
Wanaweza wasikuelewe , wanaJF wengi Ila nakuelewa vzr kabisa Mkuu

Bora pia ulivolisema hapa!

Mungu akusaidie katika mapito yako na akanyooshee njia zako
KABLA YA KUANDIKA COMMENT YAKO ZINGATIA KWAMBA HAKUNA ANAEPENDA KUWEKA WAZI BACKGROUND YAKE YA NYUMA IJULIKANE HASA KAMA SIO NZURI, UKIONA MTU ANAIWEKA WAZI MEAN KWAMBA IMEBIDI TU HAINA JINSI, SO NAANDIKA KUHUSU HAYO YOTE ILI WATU KUELEWA SITUATION NZIMA ILI UKITOA USHAURI MAYBE AU MAONI YAENDANE NA MAISHA YANGU KIUJUMLA.
 
Watu mnamshambulia mtoa mada lakini mnaweza sema ana haki ya kulaumiwa lkini vaeni viatu vyake tafadhali.

ni hivi me binafsi am proud na wazazi wangu cause walivaa uhusika wao inavotakiwa.

ila kiuhalisia cheo cha uzazi ni beyond kuzaa. ni kulea pia. Wangapi wamechukuliwa na kulelewa na adopting parents . Yaani hakuna uhusiano wa damu lakini mtu anakua anajua kuwa hawa ni wazazi wangu lakini kumbe siyo.

Nimesoma comment ya mamaSamia kaelezea vizuri sana ila watu nimeona wengi mmecomment kwa hisia.

acheni hisia tumieni logic.

Africa tunalelewa kwa uoga sana. Ndio maana hat vipaji vingi vya watoto hupotea hivihivi Ndio maana hatuendelei.

Pia unakuta mzazi anazaa mtoto ili uwe mtaji wa kumtunza yeye. what the https://jamii.app/JFUserGuide!!! Hata Mungu katuumba lakini anatuhudumia milele. analeta mvua nk.

mtoto sio mtaji. kama huwezi kulea vaa condoms.

Wenzetu wanazaa kama wajibu kuendeleza kizazi. mtoto anazaliwa anakuta kawezeshwa akili yako tu ikengeuke ndio atakuja lbda kuwa wa hovyo lakini msingi mzuri wa kimaadili unawafanya asilimia kubwa wanafanikiwa.

Dear future parents. tutafute mafanikio ili watoto wavikute pia uzee wetu usitegemee watoti wetu. Bata hadi uzeeni. ili kwamba mtoto akikukumbuka ni hisani tu sio lazima na yeye alee watoto zakee.

.wazazi wa hovyo mtu haumwi kazi kukaa kwa watoto tu mpaka wanakosa uhuru..

Me binafsi nimemaliza shule nilimuambia mzazi asiwe na any expectations kwangu maana mtaani hakuna ajira ila inshallah nauona mwanga nimepata pa kujishikiza. nikimtumia elfy tano anashukuru na nikimpa 50k anashukuru pia. sasahivi ninajitegemea lakini nikiwatembelea home lakini hata wakiwa hawana kitu huniambia tukupe nini baby? Mahindi ama? au chuma hata mboga.

acheni kuzaa kisa nyege.

NB nimelelewa na wazazi wote na nimekulia kwa ndugu. Hao ndugu sio wa damu na wanamchango mkubwa kwangu wakishirikiana na wazazi wangu.
shukran sana mkuu
 
Muombe Mungu wako akujalie hekima zaidi na mafanikio.Binafsi sikujudge kwa chochote, wala siwajudge wazazi wako.
Jitahidi kuwa mkweli tu kwa Mungu wako, uendelee kukua ukimpendeza Mungu na watu..(wazazi wako included)

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
much love mkuu
 
Back
Top Bottom