Sijivunii wazazi wangu

Sijivunii wazazi wangu

Umejawa na manung'uniko sana hata hizi baraka zitaingilia mlango upi, kila mtu akimtafuta wa kumuangushia jumba bovu humu hakutatosha,,

Huna shukrani kabisa shenzi
haina noma mkuu
 
Sasa wewe ushajitambua anzia hapo kuweka mambo sawa kwa kizazi chako...Wengi wazazi ni chenga ..

Kuna somo hapo nimeona sidhani Kama karma pia inaweza kukurudia we nenda mbele kwa mbele ,kama sijakosea hata kuwasalimia mara nyingi huendi ila sio kwamba hupendi basi ni changamoto tu za maisha.

Piga moyo konde wengi hawataki kurudi kwao na kutokana na matatizo kama hayo yako ..pambana
thank you mkuu
 
Pole man muombe Mungu akupe kipato n Mke mwema ilo badae usije ukafny kw wtt wako km walicho Fny wazazi wako
 
Si bora wewe ulisomeshwa mpaka form four! Wengine wamezaliwa wakaishi kwao kama gerezani hakuna amani, ni fujo mwanzo mwisho Matokeo yake watoto wanakimbilia kujitegemea mitaani wakiwa bado wadogo kiumri, Hata hivyo shukuru maana kwenye maisha kuna mambo yanatokea na usiweze kuzuia lolote.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
unajua mkuu kila mmoja ana kikomo chake cha uvumilivu? So mtu akieleza hisia zake kama msaada hauna japo ushauri don't start comparing shida zake na za mwingine maana hatushindani yupi ana shida zaidi ya mwenzake ila tunajaribu kusaidiana kutatua shida za wengine
 
nilichonacho kipi sasa mkuu huoni kwamba ndo nalalamika kuwa sina kitu.
Huko kulalamika ndio kubaya, be proud to your parents whatever the situation is,
Hapa jukwaani hatujuani we ungesifia tu wazee wako upate kubarikiwa kuliko kuwasemea hapa(kama ni kweli)coz mzazi ni mzazi tu hata iweje ndio nikakwambia
Wewe na kila chako ni vya wazazi wako,
Ulikua mdogo wakakulea, umekuwa mkubwa wao wamezeeka walee, hii ndio kanuni
 
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu? Au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?
Hawa ni wale wazazi hata humu wamo. Wao wanajiona wajanja kutusua Mbususu tu. Lakini kulea familia hawana habari.

Pole sana mkuu.

We komaa Mungu atakujalia.

Sio kila mzazi ni mwema.
 
Huko kulalamika ndio kubaya, be proud to your parents whatever the situation is,
Hapa jukwaani hatujuani we ungesifia tu wazee wako upate kubarikiwa kuliko kuwasemea hapa(kama ni kweli)coz mzazi ni mzazi tu hata iweje ndio nikakwambia
Wewe na kila chako ni vya wazazi wako,
Ulikua mdogo wakakulea, umekuwa mkubwa wao wamezeeka walee, hii ndio kanuni
wazazi wangu hawajazeeka bado, kuhusu kuandika huu uzi inatokea tu wakati unamood mbaya mambo hayaendi alafu unatafakari unaona kikwazo kipo sehemu fulani, Ujue mkuu kuna nguvu za kieoho zinaendesha maisha yetu.... Imagine wazazi wangu ni watu wa vinyongo wakati wote so hata nikiona mambo hayaendi naanza kuhisi au baba/mama ana kinyongo sijamtumia hela muda.... then unaniambia nisiseme kweli?
 
Hawa ni wale wazazi hata humu wamo. Wao wanajiona wajanja kutusua Mbususu tu. Lakini kulea familia hawana habari.

Pole sana mkuu.

We komaa Mungu atakujalia.

Sio kila mzazi ni mwema.
shukran sana mkuu
 
Mshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuwatunza wazazi,,kuna watu wanaitamani iyo nafasi uliyonayo kwa sasa lakini ndo ivo kazi ya Mungu haina makosa,,,kumbuka no one's perfect,,,hayo ni madhaifu madogo sana na amini ya kwamba ipo siku watatambua makosa yao kwa kukutamkia mambo ambayo hawakupaswa kukutamkia na watatubu,,,unachopaswa kwa sasa ni kuwapenda na kuzidi kuwaombea wazazi wako,,,changamoto zao zisikufedheeshe na kujiona umeshindwa,,,muombe mwenyezi Mungu maneno ya kinywa chako na mawazo ya moyo wako yapate kibali mbele zake,,utaishi vizuri sana.
 
shukran sana mkuu
Ukiwasikia humu wanavyojidai kunyandua mbususu utajua ndio aina ya wazazi kama hao.


Watu sasa wabebe matokeo ya matendo yao.

Kama mtoto hukumwandalia mazingira bora usitegemee kupata msaada wake eti kisa ni mzazi.

Tujifunze kwa watu waliofanikiwa.

Mfano Mtoto wa Kikwete pamoja na kwamba ni bilionare lakini usishangae kuambiwa bado anaishi kwenye nyumba ya Baba yake na Mama yake.

Huo ni mfano tu. Lakini mifano ipo mingi kila mtu pahala pake.

Maskini watoto wakikuwa tu wote anatamani waondoke nyumbani wakaanze maisha yao. Sio kwamba ndio utaratibu bali ni kukosa upendo na kuzaa bila mipango.

Tajiri akizaa watoto anatamani hata ukioa utaoa ukiwa unaishi nyumbani kwa Baba na Mama.

Huku kwetu uswazi ukifikisha miaka 18 tu wanatamani wakufukuze.
 
wazazi wangu hawajazeeka bado, kuhusu kuandika huu uzi inatokea tu wakati unamood mbaya mambo hayaendi alafu unatafakari unaona kikwazo kipo sehemu fulani, Ujue mkuu kuna nguvu za kieoho zinaendesha maisha yetu.... Imagine wazazi wangu ni watu wa vinyongo wakati wote so hata nikiona mambo hayaendi naanza kuhisi au baba/mama ana kinyongo sijamtumia hela muda.... then unaniambia nisiseme kweli?
Tatizo lako ni kwamba huku haupo na kule haupo, yaani unajua kabisa kwamba wazee wakikasirika inaweza kua mbaya halafu bado unawakera kwa kuwasemea hapa jukwaani si sawa, hivi wao nao wakianza kusema hapa huyu alivyokuwa mdogo alitupa taabu hizi na hizi, mara kulia, mara kuumwa, mara njaa, mara nguo mara maradhi mara hivi mara vile utafrahia?
Heshimu wazee kadri uwezavyo ili ubarikiwe
 
Mshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuwatunza wazazi,,kuna watu wanaitamani iyo nafasi uliyonayo kwa sasa lakini ndo ivo kazi ya Mungu haina makosa,,,kumbuka no one's perfect,,,hayo ni madhaifu madogo sana na amini ya kwamba ipo siku watatambua makosa yao kwa kukutamkia mambo ambayo hawakupaswa kukutamkia na watatubu,,,unachopaswa kwa sasa ni kuwapenda na kuzidi kuwaombea wazazi wako,,,changamoto zao zisikufedheeshe na kujiona umeshindwa,,,muombe mwenyezi Mungu maneno ya kinywa chako na mawazo ya moyo wako yapate kibali mbele zake,,utaishi vizuri sana.
Wazazi wazembe kama hawa sio vyea kuendelea kuwahendekeza. Ulaya walishaachana na huo ujinga.

Mtu anakunywa Mbege tu kila siku anazaa bila mpango then ategemee watoto wake kusaidiwa.

Hata sasa mitaani kuna vijana wanazalisha watoto hovyo na matokeo yake tunapata vuzazi kama huyu mtoa mada.

Kama jamii tuikatae hii tabia ya wazazi kupenda starehe ya ngono huku wakiwa hawana habari na matokeo ya ngoni hiyo.

Fikiria hapo ulipo kuna single mother wangapi? Nani atawalea hao watoto?
 
Back
Top Bottom