Sijivunii wazazi wangu

Sijivunii wazazi wangu

Naam kuna wakati wazazi wanazingua sana, ila hupaswi kuwa na kinyongo kwa mzazi wako kamwe. We samehe kisha sahau kama kuna jambo limetokea, tumia akili kuepuka matatizo yanayo kukabili, kamwe usitumie mihemko.

Epuka kuingilia ugomvi wa wazazi wako, wazazi ni wakuwapenda sana ata kama hawaja tenda wema kwako. Wapende, waheshimu na wajali wazazi wako kadri uwezavyo.
ahsante kwa ushauri mkuu wangu
 
Kwakuwa umechagua ID nayoiheshimu sitatumia lugha inayoudhi kwako.
Umeandika kwa hasira Sana,Tulia urudi kuandika vizuri. Nasisitiza WAHESHIMU WAZAZI mwenye masikio na asikie
Tumia hujakatazwa. Wazazi tunawaheshimu na wao watimize wajibu wao waache ujanja ujanja wa kujificha kwenye laana. Wazungu wana sheria kali sana za kumlinda mtoto na wako mbele yetu karibu kwenye kila kitu... sisi na maadili yetu ya woga tunazidi kuzama kwenye umaskini.
 
dah! mkuu maisha mbona ni mapana sana kuliko kunyonya? okay nikuulize wewe unajuaje kwamba nilinyonya? wewe ni mama yangu?
Nitoe shule kidogo!
Mahitaji muhimu kwa binadamu ni Chakula (food), malazi (shelter) na mavazi (clothes) ,ukiwa tumboni yote uliyapata kwa mama yako!

Tuseme basi kakutelekeza ukiwa mdogo haibadili ukweli hapo juu.

Unachopaswa kufanya ni kumheshimu na kumuombea unapoweza msaidie. Ni hayo tu
 
Nitoe shule kidogo!
Mahitaji muhimu kwa binadamu ni Chakula (food), malazi (shelter) na mavazi (clothes) ,ukiwa tumboni yote uliyapata kwa mama yako!

Tuseme basi kakutelekeza ukiwa mdogo haibadili ukweli hapo juu.

Unachopaswa kufanya ni kumheshimu na kumuombea unapoweza msaidie. Ni hayo tu
we jamaa kuna mtu kasema hamuheshimu mzazi wake? are sure una uelewa mzuri kweli?
 
Nitoe shule kidogo!
Mahitaji muhimu kwa binadamu ni Chakula (food), malazi (shelter) na mavazi (clothes) ,ukiwa tumboni yote uliyapata kwa mama yako!

Tuseme basi kakutelekeza ukiwa mdogo haibadili ukweli hapo juu.

Unachopaswa kufanya ni kumheshimu na kumuombea unapoweza msaidie. Ni hayo tu
Nasisitiza wewe ni mpumbavu na nusu. Wakati unamwagia/mwagiwa ndani hukujua kuna mimba itatungwa? Kama mtu hayuko tayari kwa majukumu avae zake tu condom kuliko kuleta viumbe vya kuja kuwatesa na kuwapa laana kiholela.
 
dah! a people like you ni waelewa sana mkuu nimekukubali sana mkuu wewe ndo umeelewa ni nini nilichozingumzia humu, Me mtu akinikosoa kwenye huu uzi namuona sio muelewa, maana hadi naandika nilijua naandika nini, aijawahi kuwakosea adabu wazazi wangu ila wao kuna wakati wananikosea mimi waziwazi ila mjmi hujikuta nikiwaweka sawa
Tunazidi kuwa maskini kama taifa kwa watu kufanya starehe zao huku baadae wakikwepa majukumu yao. Watoto wa mitaani wengi wao wana wazazi ila ndo hivyo hawataki majukumu. Wapo wazazi wanaokula mema ya nchi kwa kuhangaikia watoto wao since day one. Mama Diamond pamoja na ufukara wake alikomaa na mwanae hadi alipofikia.
 
Tumia hujakatazwa. Wazazi tunawaheshimu na wao watimize wajibu wao waache ujanja ujanja wa kujificha kwenye laana. Wazungu wana sheria kali sana za kumlinda mtoto na wako mbele yetu karibu kwenye kila kitu... sisi na maadili yetu ya woga tunazidi kuzama kwenye umaskini.
Labda tujiulize heshima maana yake nini?
Heshima ni sawa na neno RESPECT, (treat someone or something with kindness and care) hiyo ndiyo heshima tunayopaswa kuwapa wazazi wetu. Mapungufu yao hayabadili ukweli kuwa ni wazazi wako.
 
Labda tujiulize heshima maana yake nini?
Heshima ni sawa na neno RESPECT, (treat someone or something with kindness and care) hiyo ndiyo heshima tunayopaswa kuwapa wazazi wetu. Mapungufu yao hayabadili ukweli kuwa ni wazazi wako.
Fuatilia sheria za USA au Europe kuhusu watoto ndo utajua hapa kwetu tunafanya mizaha sana.
 
Hilo ni somo kwako ,nawewe ukipata mtoto hakikisha unakuwa responsible parent , responsible parenthood inatakiwa , huu utamaduni wa watu kuzaa tu kama sifa au fashion ni utamaduni wa kipumbavu sana , sio watu kuzaa tu kama panya halafu viumbe wanaozaliwa wanateseka tu , kabla ya kuzaa hakikisha una uwezo wa kumhakikishia maisha bora huyo kiumbe .
Hivi ni wote mna wazazi kama wangu?, au mliwahi kuwa na wazazi kama wangu?, Najua ambao hamuelewi nini nazungumzia hapa haiwezi kuwaingia akilini au pia mnaweza kuhisi labda sina akili timamu na wale ambao kwa bahati mbaya mlishapoteza wazazi wenu basi pia hii tungo haitowaingia akilini, ila aina ya maisha ninayoyaishi ndo yanafanya niandike tungo hii ngumu ambayo si rahisi kuisikia kwa watu.

Sorry kwa kusahau kuwasalimu, ila kwa leo nipo na bad mood naji-feel tu kutema hii sumu ili isiniue maana hii kitu inaniuma sana wakuu, Imagine unakuwa na wazazi ambao hawajawahi kukupa direction ya maisha, Connections, Hawajaaliwa kumiliki kiwanja au hata nyumba useme utarithi, Haya basi wangekupambania usome uwatoe kwenye hiyo hali. wapi, Haya basi hata shughuli ya kufanya basi iwe imetokana na connection zao. wapi, Haya basi hata ushauri nini cha kufanya au pita njia hii. wapi, Kiufupi baada ya kumaliza Kidato cha nne nikaja Dar habari ya wao na mimi iliishia palepale.... I'm sure hata matokeo yangu hawayajui, ila wao wanajua mimi nimefeli. Mimi kuamua kuwaacha nisiwasumbue masuala ya kunisomesha kwa kuwa niliona hali ya nyumbani sio basi wao akili zao zimesave kwamba nilifeli ila sivyo. Okay, tuseme ni ukweli nimefeli hebu niambie je, mwanao ikitokea ameshindwa kuendelea na masomo basi unamtelekeza akajuane na maisha yeye mwenyewe?

Dah! Asee inaniuma kinoma ni Dsm mwaka wa nne sasa, Mzee yupo Arusha mama yupo Iringa (Wao waliachana punde tu baada ya mimi kuzaliwa) Mimi ni mtoto wa pekee kwa baba ila mama tayari ana watoto wengine wawili huko alipo.... Simu zao zikiita kwangu basi najua ni vizinga tu, Baba aliwahi kuanzisha mradi wake huko Moshi akanishawishi nimtumie kahela fulani tuwekeze tufanye jambo litatulipa nikafanya ikaja ikalaga kwangu nikasemehe kwa kuwa ni mzazi, Baba yangu anaishi kwa wazazi wake yaani kwa bibi yangu mimi., Mama yangu anaishi Iringa amepangisha na hata baba wa watoto wawili aliokuwa nao pia walishaachana (sahivi ni single mother)

Dah wakuu kuna vitu navificha hapa sitaki visema kutoka kwa huyu baba yangu na mama yangu kuna maneno waliwahi kunitamkia kwa nyakati tofauti tofauti maana nilishajuza kwamba hawaishi pamoja, ila acha niseme tu, kwa sasa wao wanajua mimi napiga harakati zangu za hapa na pale kwahiyo kuna wakati nawakumbuka japo 10k kila mmoja, Sasa ikitokea labda imepita muda mrefu sijafanya hivyo kila mmoja wao huisi kwamba nampendelea mwingine na pengine labda ndo inapelekea nisitume hela kwa muda mrefu. Jambo hili huleta mgogoro wa vinyongo baina yangu mimi na mzazi atakaehisi hivyo, Ni wote tu sometimes ni mama sometimes baba me, hupambana kuwaelewesha kwamba sivyo wanavyofikiriana hadi huchoka.... Kuna siku mzee aligomba hadi akanikatia simu nikakopa 12k nikamtumie eti akapiga simu muda huohuo huku anacheka "Mwanangu wewe ndo umetumia hii asante sana" nikamjibi ndiyo kwa hasira nikamkatia simu.

Wote tunaamini wazazi wetu ndo wanatupenda kwa dhati ila mimi kwangu ni tofauti kwani nilishajithibitishia kabisa kwamba wazazi wangu wapo after money, hata simu zao zikiita muda huu najua tayari hapa napigwa kizinga.

Baba alishawahigi kunitamkia maneno haya "Mimi nahesabu sina mtoto bana, Mtu hata hunisaidii chochote hapo nikikuambia nitumie kalaki kamoja utasema huna, kwenda kule me sio baba yako" hiyo ilikuwa kwenye simu and i was in hard situation for sure imagine pa kulala penyewe palikuwa kwa mshikaji kanisitiri, ila baadae tulikuja tukamalizana mshua kiume tukaendelea kuishi kinafki. Mama nae aliwahi kuniambia maneno haya "Yaani mi nahesabugi nina watoto wawili tu, We mtoto gani unamsahau mama yako kiasi hiki? Yaani hujawahi hata kunitumia zaidi ya 30,000 acha nimuombee huyu mwanangu wa pili ndo naona atakuja kunitoa kwenye umasikini...." Huyu mtoto wa pili sahivi yupo form 5 na anasomeshwa na mashangazi zake wao upande wa ndugu zake wapo vizuri kiuchumi kiasi chake so, mama yupo proud na huyu wa pili.... Me hiyo kitu though inaniuma mimi kama first born ila me humuachia Mungu wangu kwani ndiye alieruhusu niishi haya maisha.

Kiufupi me najionaga kama nina laana hivi, Imagine unazaliwa nje ya ndoa alafu bado wazazi wanaachane tena punde tu after umezaliwa😁😁😁, Acha nicheke tu maana muonekano wangu jamani ndo unafanya nione kabisa kwamba familia yetu ni kama kuna mahali ilichezewa, Me muonekano wangu ni ambao unaonesha kabisa kwamba imetokea bahati mbaya tu me kuzaliwa kwenye aina hii ya familia, Me najipenda sana watu hudhani me ni mtoto wa geti kali, Huishia kuitwa majina kama Bishoo,Sharo, Wa kishua ila me hubaki tu kushangazwa na hayo majina laiti wangejua.

Anyways ambao wangependa kujua naishije hapa Dar ni kwamba naishi ki-mission zaidi, Me ni kijana ambae napenda uhakika sana sinywi pombe,sivuti bangi, sina hobby na ladies, Me ni mtu ambae kiufupi sina mambo mengi, Me ni kijana ambae Mungu angenijaalia wazazi ambao wanaelewa wajibu wao ningekuwa mbali mno, Fikiria nimelelewa na baba pekee... though alikuwa careless ila hadi namaliza 4m4 sijawahi kuingia kwenye mtindo mbovu wa maisha, Me nimekuja Dar mbali na wazazi sina hili wala lile and they didn't even care of me na still nimeweza kujitegemea, Hadi kuna wakati najiuliza usikute hii kitu ndo imefanya wakaona huyu kashajiweza tuachane nae. Maana me nikiwa 17 tuu washaanza kunipiga vizinga na nikaonesha kuvimudu japo kibishi.

Simu zao za kinafki husema kwamba "Mwanangu lini uje kunisalimia, miaka mingi hujaonana na na baba/mama yako hivi unajua najisikiaje huku nilipo fanya uje bana" hapo ni baada ya 10k kuingia kwenye cm ya mmoja wapo... Kimoyomoyo mimi hujosemea kwamba "Kama sio ninyi maisha yangu yasingekuwa ya taabu hivi, Acheni niwatumie kidogo changu hiki ili mjihisi nanyi mna mtoto" Ila kiukweli sijivunii wazazi wangu, Sasa jamani hata useme ukasalimie unaenda kulala wapi Baba hana nyumba yupo kwa bibi imagine kweli tuende wote tukarundikane kwa bibi mjukuu na baba yake kweli? au haya kwa mama, Kapanga room mbili mimi na midevu yangu nikaingie nikae kwenye bedroom ya mama sure?

Eeh Mungu wangu nisamehe kama nakosea ila acha niyatoe tu maana sina wa kunisikiliza nitakufa kwa maumivu haya niliyonayo, Sometimes inafikia nakufuru kuona ni bora mtu uwe hauna wazazi kuliko kuwa nao ambao wanachangia kukurudisha nyuma na kukuvunja moyo, Wazazi waliotangulia wenye ramani ila hawakuoneshi njia.

Mtu mnajua mmeshindwa kumhakikishia mwanenu maisha bora haya basi kaonesha anaweza kupambana basi muacheni still bado mnataka kumpa majukumu ya kuwazingatia ninyi sure?
 
Natumai wanao watakuja kujivunia wewe kama mzazi wao. Subira yavuta kheri
 
Kweli kabisa eti unatakiwa ushukuru ulizaliwa wanaoshukuru ni kama watoto wakalelewa vyema na wazazi na sio kutelekeza watoto
Na mengine hata pesa za kuhudumia malezi ya mtoto huwa hayataki hata kutoa ni kuzaa tu na kutekeleza as if ni nini sijui , kule America na Europe waliliona hili mapema ndio maana kuna sheria kali za child support , ni lazima uwajibike asilimia 100 kwa kiumbe uliyemzaa ,hiyo ni lazima na ipo kama sheria kule.
Ile wako uikiuke sasa ,utatamani uzikwe ukiwa mzima .
Ilipaswa iwe hivi hata huku nchi za kishenzi kama hizi
 
Hilo ni somo kwako ,nawewe ukipata mtoto hakikisha unakuwa responsible parent , responsible parenthood inatakiwa , huu utamaduni wa watu kuzaa tu kama sifa au fashion ni utamaduni wa kipumbavu sana , sio watu kuzaa tu kama panya halafu viumbe wanaozaliwa wanateseka tu , kabla ya kuzaa hakikisha una uwezo wa kumhakikishia maisha bora huyo kiumbe .
kweli mkuu
 
Na mengine hata pesa za kuhudumia malezi ya mtoto huwa hayataki hata kutoa ni kuzaa tu na kutekeleza as if ni nini sijui , kule America na Europe waliliona hili mapema ndio maana kuna sheria kali za child support , ni lazima uwajibike asilimia 100 kwa kiumbe uliyemzaa ,hiyo ni lazima na ipo kama sheria kule.
Ile wako uikiuke sasa ,utatamani uzikwe ukiwa mzima .
Ilipaswa iwe hivi hata huku nchi za kishenzi kama hizi
alafu unakuta kuna mtu anatetea eti mzazi ni mzazi dah! hizi akili
 
Back
Top Bottom