Sijui alipatwa na nini kilichopelekea kujiua!

Sijui alipatwa na nini kilichopelekea kujiua!

aliyetegwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
313
Reaction score
486
Habari wakuu,

Iko hivi alikuwa ni kijana nadhifu, mchangamfu na kikubwa mwenye uwezo mkubwa darasani. Baada ya harakati za masomo alimaliza shahada yake ya kwanza 2014. Kwa kipindi cha karibia miaka nane hakupata kazi ila alichakarika haswa kwa kufungua genge na kuhudumia familia kwa kazi hiyo.

Mungu si Athumani mwaka huu mwezi wa saba alipata ajira serikalini, hajapokea hata mishahara mitatu shetani ashamvaa, sijui alipatwa na nini. Alianza kama matani siku kama nne kabla siku yake ya mwisho akaanza kusema akilewa kuwa atajiua, ila walio karibu yake wakachukulia poa wakihisi ni ulevi.

Siku ya tukio ndiyo inanifikirisha sana, aliamka vizuri mida ya mchana akawa amelewa chakari. Akaanza tabia yake ya kusema anataka kujiua, ila hii siku hii kauli ilionekana kuwa na nguvu zaidi, watu wakamkamata na kampeleka kituo cha polisi. Polisi walikaa naye kama masaa matatu mpaka walipomuona yuko sawa na pombe zimepungua, wakamwachilia, kumbe hawakujua masikini.

Alipotoka hapo alikwenda kumeza sumu ya panya ila akaona haoni matokea hivyo akaanza kupiga kelele kulalamika kwanini hafi na amekunywa sumu, akaamua kumeza coin mbili za shilingi mia mbili.

Baada ya muda mfupi hali yake ilikua mbaya akakimbizwa hospitali, Mungu saidia akapata huduma na kupata nafuu kubwa. Daktari wake akasema angeshughulika na sarafu alizomeza kesho yake, aliyekuwa akimuhudumia akaagizwa kwenda kumtafutia walau uji maana alikuwa amechoka mno, angejua asingekwenda.

Baada ya kuachwa hospitali alitoroka na kwenda kujizamisha ziwani, kitu kilichopelekea kifo chake. Ameacha mke, ambaye ni mama wa nyumbani na watoto wawili wadogo, mdogo akiwa hajafikisha hata mwaka.

Najiuliza kwanini alifanya jaribio la kujiua kwa nguvu namna hiyo kwa zaidi ya mara mbili kwa ndani siku moja? Ameumiza sana moyo wangu nikiangalia watoto wake wadogo.

Wakuu hii kwenu imekaaje, mnafikiri mwana alipatwa na nini?
 
Hili ni tatizo la akili. Na kwa sasa mtu akisema nataka kijiua au akisema nitakuua msichukulie utani, chukua hatua ya haraka sana kumuokoa na kama yupo kwenye hali nzuri mpigishe stori kidogo, lazima kuna kitu kinapita akilini mwake, na ameshindwa kabisa kukitatua
 
Habari wakuu,

Iko hivi alikuwa ni kijana nadhifu, mchangamfu na kikubwa mwenye uwezo mkubwa darasani.
Baada ya harakati za masomo alimaliza degree yake ya kwanza 2014. Kwa kipindi Cha karibia miaka nane hakupata kazi ila vyo akaanza kupiga kelele kulalamika kwanini hafi na amekunywa sumu, akaamua kumeza coin mbili za shilingi mia mbili.



Wakuu hii kwenu imekaaje, mnafikiri mwana alipatwa na nini?
Introversion ni mbaya sana. it can lead to insanity.
 
Duuh ni roho za kipepo hakuna cha afya ya akili wala nini. Huyo aliemfanya akose ajira kwa miaka yote hyo eidha alijisahau au dawa ziliisha nguvu hatimae akapata ajira,kuona hivyo akamtupia jini kujiua likamfanya ajiue.... naandika huku naogopa
 
Back
Top Bottom