Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Unoboy hana nafasi ya kushinda labda kwa "kafara ya damu" kama ilvyokuwa kwa "MTOLEA"
Ruksa kushangilia goli za kuotea na faulo lakini washangiliaji na mashabiki wanajulikana maamuzi yao wakiona haki inaporwa hawachelewi kuvunja viti na kurushia waamuzi na wachezaji chupa na vinyesi!!
 
Kwa jinsi ninavyomfahamu Gwajima hizo tuhuma anaweza kuzipooza vizuri sana na akashinda mapema sana.

Ile video yake ya anavyokula boga la kondoo wake kanisani imeshaondoshwa mitandaoni??
 
Kwa Halima Mdee hawana la kufanya zaidi ya kutapatapa. Hata hivyo waliamua kumfuta Dominic Furaha wakiamini anagalau Gwajima atasaidia lakini wapi.
 
GENTAMYCINE,

Wakristo wenye misimamo mikali wanamkubali Gwajima, nakusudia walokole na the likes, pia watu wa mfumo wanaona atafaa sana kwa sababu zao' tufanye subra na hio ndio raha ya siasa bwana dawa.
 
Ni sahihi
 
Kwanini mnawasemea
 
Gwajima atapita tu!!!
 
Kusema ukweli gwajima hapa kawe watu hatumtaki
Siasa ina mengi mkuu, lolote laweza jitokeza, mpiga kura anapokabidhiwa karatasi ya kura anaweza fanya lolote.

Tuombe uzima, ila Ccm wamempitisha Gwajima hapo kimkakati yaani wameamua kumuwekea Halima (Chadema) kisiki.

Wakati mmoja huyu Gwajima alishangiliwa sana na CDM huku akionekana kama shujaa na mwenye msimamo (rejea vita yake na Makonda), Sasa amegeuka hasimu wa CDM, hapa Ccm wamefanya makusudi kabisa ili washirika wawili wa zamani (CDM na Gwajima) wapambane wenyewe kwa wenyewe huku wao wakimsaidia mmoja (Gwajima) kutwaa jimbo.
 
Paskali alipata kura ngapi?
 
Kwa kuwa waislamu na Wakotoliki ni waungwana sana basi huyu Bwana alishasamehewa Kwahyo msimu ujao atatimba bungeni na chopa yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…