Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Uchaguzi 2020 Sijui Gwajima atatumia Sabuni gani ya 'Kuwatakatisha' Waislamu wa Kawe 'aliowadhihaki' na 'Wakatoliki' waliokwazika naye 'alipomshambulia' Pengo

Labda wa siku hizi sababu kwa kuzisoma hadithi za Mtume M. S. W. Yeye alijaa subira!

Kwa kuwa bado najifunza Habari zake kwa haraka haraka sizani kama alikuwa mtu wa visasi!

Maana kuna wakati mtu alienda kujisaidia msikitini wafuasi wake walipotaka kumdhuru aliwakataza kabisa badala yake akawaambia wasafishe wapige deki na kumuacha!

Mwishoni yule mtu alirudi kuomba msamaha na akataka atiwe maji awe Muislam sababu wakati ule ilionekana kuwa na amani!

Sasa Kwani siku hizi mmekuwa wa tofauti?

Mtu kama mzee mwinyi ni miongoni mwa wanaoutangaza uislam vizuri sana na Ndiyo maana Mungu anamuweka !

Na atazidi kumuweka InshaAllah maana hanaga ubaya wala nongwa !

Tuepuke kuhusudu vijimambo vidogo vidogo!

Mimi nakwambia yanayosemwa na watoa mawaidha wa dini ya kiislam kwa miaka mingi sana kama wakristo wangekuwa watu wakuyahusudu hayo wanayosemwa nazani amani kwenye jamii ingekuwa mashakani siku nyingi!
Mtume S.A.W siyo Mtume M.S.W
 
Kwako mkuu kuikashifu dini yetu waislam linaweza lisiwe Jambo la maana lakini sio kwetu sisi waislam, dini yetu kwanza Mambo mengine baadae. Kama huamini nayokueleza kuhusu Gwajima naomba tusubiri baada ya octoba 28 tutarud hapa, kama Jimbo lakawe atalichukua huyo muhuni anaechafua dini zawatu.

Kama vyombo vya dola vilishindwa kumtia nguvuni Gwajima ambae alikuwa anatangazia watu wafungua Whatsapp group za kisukuma ili waweke mikakati msukuma mwenzao ashinde, wanashindwa mkamata Gwajima anaejirekodi huku akifanya zinaa kinyume kabisa na maadili na utamaduni wa mtanzania basi hawana uwezo wakukikamata Mimi.


Mbona ile video ilisemekana ilitengezwa na wasiomtakia mema?

Sasa wangemshitaki aloitengeza au wamshitaki aliyechafuliwa?

Manake wangemshitaki Gwajima ambaye amechafuliwa wasingelimtendea haki badala yake ilipaswa wawashitaki walioitengeneza kwa kutaka kumchafua na kuingilia faragha yake!

Hata kama ingekuwa ni kweli amezini bado hiyo serikali haiwezi kuingilia hiyo angejuana yeye na Mungu wake atakavyomhukumu

Kwani nikuulize ni wachungaji/padri na mashekhe/maimamu wangapi wanaozini?

Na wengine wanakutwa ugoni kabisa Je serikali iwe inaingilia kati kuwashitaki?!

Tupendane tushirikiane tusihusudiane
 
Hapa kamati kuu imeingia choo cha kike ikiwezekana wabadilishe gia angani
Kwani choo cha kike hakikidhi haja za wanawake? au ni vyoo vya kiume vinaweza kukidhi haja za wanawake? kama kamati kuu haina wanawake naungana nawe kabisa, vinginevyo hapana
 
GENTAMYCINE,

Kawe asilimia kubwa ni wakristo na walokole sana ndio maana makanisa chungu mzima yako huko.ni sawa useme gwajima kugombania mbagara.
 
Gwajima anagombea kupitia chama kikubwa cha siasa chenye dola na ukwasi.,si rahisi kushindwa!!!
Kwani miaka yote Halima aliposhinda CCM hawakuwa na mgombea? Kuna kiwango cha ushindi hata wenyewe wanajistukia kuchakachua.
 
Ktk kupambana kutafuta ugali mambo mengi sana hujitokeza njiani, kuna kujikwaa, kuanguka, n.k.tuvumiliane na kusameheana sana watanzania hasa vijana, kama gwajima hana sifa za uongozi basi tusimchague kwa sbb hiyo ila kamwe tusimhukumu kwa mapito yake aliyopitia ambapo hata sisi pia tunayo ya kwetu, Ni Mungu tu ametusitiri.

Tutaacha tu akielewa makosa yake na kutubu madhabauni nitakuwa wa kwanza kumpigia kura
 
Mkuu nakueleza kwa sisi waislam hatuna udini juu ya dini yetu, napopote pale tunajiona fahari kuwa waislam, tuna amini kila mtu anadini yake, wao nadini yao sisi na dini yetu. Nahatukashifu dini ya mtu napia hatupendi na hatuko tayari dini yetu kukashifiwa tutailingania popote pale kwa gharama yeyote Ile. Sasa kama Gwajima alitukashifu kwa kinywa chake ,hakuna muislam ambae anaweza mpigia Kura, Halima nimkristo pia lkn hatuko tayari kuongozwa na mkristo Gwajima anaetamka kwa kinywa chake atazigeuza madrasa/misikiti kuwa Sunday school hatuko tayari na kwahilo hatujifichi. Heri tuonekane wadini huku tukipinga wanaokashifu dini yetu waziwazi.
Na mnaowaita makafir ni kina nani?
 
Nauliza kwa dhati kabisa kutoka moyoni

Ni wazi tuna mabinti katika jimbo letu na tungependa wawe chini ya uongozi salama,mabinti zetu wakienda kutembelea ofisi zake watoke salama bila harassments zozote

Tumkabidhi mabinti zetu kweli(au wake zetu)? Watakuwa salama? Huko alikokuwa aliacha usalama ?
 
Kama kuna Jimbo ambalo endapo CHADEMA na Mgombea wao Halima Mdee 'watazichanga' Karata zao vizuri sana basi 'watashinda' mapema tu kutokana na 'Mgawanyiko' mkubwa uliopo basi ni la Kawe. Wale wana CCM mliokuwepo jana Kawe katika Kikao ( japo Mimi nilikuwa mbali na Jengo ) mtanielewa kwani 'Mazungumzo' makubwa ya jana yalikuwa ni Kazi ngumu ya Kumnadi Gwajima.

Sina tatizo na CCM 'Kumpitisha' Gwajima 'Kugombea' Jimbo la Kawe hasa ikizingatiwa kuwa ana 'Ushawishi' wake fulani fulani ( hasa wa Kiimani ) na pia ni 'Mzungumzaji' mzuri ambaye pia ana 'Utajiri' mkubwa sana wa kufanya 'Propaganga' na akafanikiwa. Ila kwa upande wa Pili wa Shilingi kuna 'Dhambi' mbili ambazo Gwajima anazo na kama CCM hawatazifanyia Kazi upesi Halima Mdee anashinda.

Kauli za Gwajima kuwa akiwa Mbunge atavifanya Vyuo vyote vya Kiislamu Kawe kuwa 'Sunday School' na ile Kauli yake ya 'Kumshambulia' Kadinali Pengo ambayo tunajua ndiyo 'Mzizi' Mkuu wa Wakatoliki nchini Tanzania ( na wa Kawe nao wakiwemo ) zisipofanyiwa Kazi mapema tena kwa Gwajima Mwenyewe Kujirudi, Kuzitengua na Kuomba Radhi ( Msamaha ) zinaweza Kumponza

CCM na Kamati Kuu yenu pamoja na 'Umakini' wenu mkubwa hadi kuwa na Madawati ya Usalama ndani ya Chama nashangaa na nimesikitika mno kuona ya kwamba 'Mapungufu' haya Mawili ya Gwajima ama hamkuyajua au mmeyapuuza kwa kudhani kuwa Kazi Kwake itakuwa ni rahisi. Na pia mlisahau kuwa kama kuna Jimbo lina wana CCM 'Wanafiki' basi la Kawe Tanzania nzima.

Yawezekana leo GENTAMYCINE nisieleweke nanyi ( wana CCM ) ila ninachojua wana CCM wengi Kawe kwa 'Hasira' zao ambazo huwa wanapenda mno Kuzionyesha katika 'Karatasi' zao za Kupigia Kura watampigia Mgombea wa CHADEMA Halima Mdee kama walivyofanya mwaka 2010 na 2015. Kuna 'Mgawanyiko' na 'Mpasuko' mkubwa sana ndani ya wana CCM wa Jimbo la Kawe.
October 28 baada ya masanduku ya kura kuongea usiache kurudi hapa na huu ujinga wako uliouweka hapa.
 
October 28 baada ya masanduku ya kura kuongea usiache kurudi hapa na huu ujinga wako uliouweka hapa.

Bora Mimi Mjinga kuliko Wewe 'Pumbavu / Popoma' Mbobezi kabisa hapa Jamvini. Una safari ndefu mno tu ya kuweza Kubishana nami Kihoja hapa.
 
Cha kujifunza zaidi,
KAMA UNA NDOTO ZA KUWA MWANASIASA,LINDA SANA MDOMO WAKO.
Ni hatari sana kama upande wa pili utaamua kutumia udhaifu huo kumtesea Gwajima,hatokuwa na cha kujibu zaidi ya kuwa tu kimya,na kukubali yaishe na yeye kubaki tu akihubiri kanisani.
 
October 28 baada ya masanduku ya kura kuongea usiache kurudi hapa na huu ujinga wako uliouweka hapa.
Ungejibu hoja zake ungeonekana na akili sana kuliko hata yeye,ila kumuonyesha dharau kama hii kabla ya kujibu yale aliyo yatoa ni ishara ya udhaifu wa hali ya juu,hili nalo ni tatizo la wanachama wengi katika huu mtandao,
unaweza kumpinga mtu kwa vile unavyopenda bila kumtusi.
 
Yani nyie chadema ni matopolo kabisa uyuuyu Gwajima angegombea kupitia chama chenu msingekuwa mnaandika huo ujinga wenu mmeona amesimamishwa na chama cha mapinduzi na mmeona dhahiri kwamba awamu hii amtoboi ndio mnandika u ujinga wenu kwa taarifa yenu Gwajima ndio mgombea na atapita kwa kishindo nyie subiri muone tu, niwasauri tu kapambanieni ayo majimbo machache mliobakiza muone kama mtafanikiwa lakini kwa kawe mmeshashindwa .
 
Back
Top Bottom