#COVID19 Sijui kama mtazamo wangu uko sawa, ila nawaona wote wanaopinga chanjo kama wana shortage kichwani!

Mpaka sasa pande zote mbili, kichanjwa na kutokuchanjwa, woote hakuna mshindi!!

Kwa hiyo usimseme yeyote kwa lolote, Ukisha chanja, kaa kimya maana hujui itakuwaje baada ya miaka miwili au mitatu ijayo

Halafu, ikiwa chanjo zilizoletwa ni m.moja tu, na waliochanjwa kwa mjibu wa kitengo, watu kama laki moja tu na ya waiochanjwa,

Sasa ikiwa, Watu laki moja wanachanjwa kwa wiki nzima, chukia idadi ya watanzania m 60000000 ÷ 100000 × 7 = na siku 420000

Ambapo unachukua siku 420000 ÷ 365= na miaka 11+ ndipo xoezi la kuchanja litamamlizika

Sasa mbona tunalaumiana bhana?

Mimi nitakuwa wa mwisho kuchanja, kwa hiyo ninamiaka 10 na nikisubili zamu yangu ya kuchanja
 
Reactions: Ame
Hata microphone anayoitumia Rashidi kuwasema vibaya hao mabeberu,nayo imetengenezwa na hao hao anaowaita Mabeberu,

Hata Gari inayompeleka kwenye hiyo microphone nayo imebuniwa na kutengenezwa na hao hao mabeberu pia,

Beberu ni kama maji,usipo yaoga basi utayanywa.
 
Rashid hata elimu ya dini hana! Ni mchawi fulani aliyepata ujanja nigeria wa kupambaza watu wampe sadaka! Hili dubwana ni jini,
 
unauhakika chanjo ni za marekani tu na uingereza? unajua zanzibar imepokea chanjo kutoka nchi gani? ndio maana nasema mna shortage kichw

unauhakika chanjo ni za marekani tu na uingereza? unajua zanzibar imepokea chanjo kutoka nchi gani? ndio maana nasema mna shortage kich
Wabongo bana hamnazo kabisa hivi unaweza tokea kusikojulikana ukasema una chanjo bila ya kuidhinishwa na w.h.o na hilo shirika unayafahamu fika makao yake makuu kwa taarifa yako hata hao wachina waliidhishswa na w.h.o
 
Kusema kuwa ni za Wamarekani na Waingereza tu siyo kweli. Hata hiyo Pfizer imetengenezwa na Wajerumani (Biontech) na Boss wa ile Kampuni ni asili ya Uturuki .... Alizaliwa Uturuki akakulia Ujerumani.

Kuna chanjo pia za Wachina (Sinopharm na CoronaVac), Warusi (Sputinik V) na Wacuba (Abdala).
 
Wabongo bana hamnazo kabisa hivi unaweza tokea kusikojulikana ukasema una chanjo bila ya kuidhinishwa na w.h.o na hilo shirika unayafahamu fika makao yake makuu kwa taarifa yako hata hao wachina waliidhishswa na w.h.o
unafahamu kwamba dawa zote unazotumia hospitali zimeidhinishwa na hao hao WHO? kweli we unamakamasi kichwani sio akili za kawaida hzo
 
Mkuu, ulitaka kuandika kitu kizuri sana but you missed some good points somewhere...🤔
 
unafahamu kwamba dawa zote unazotumia hospitali zimeidhinishwa na hao hao WHO? kweli we unamakamasi kichwani sio akili za kawaida hz

unafahamu kwamba dawa zote unazotumia hospitali zimeidhinishwa na hao hao WHO? kweli we unamakamasi kichwani sio akili za kawaida hzo
Acha uongo tangu mdogo nimekuwa nakunywa miti shamba na mpaka sasa nipo gado na naendelea kujifukiza bila hao w.h.o wameidhinisha nn apo
 
Kuna jambo halijawekwa sawa kwenye chanjo ya corona hapa nchini na hapo ndipo Gwajima anaonekana kama atashinda hili gemu na litampa umaarufu sana kuliko alivyo sasa.

Suala la kwanza ni la kimantiki. Watanzania wapo milioni 60, chanjo dozi zipo milioni moja. Hata kama chanjo inafanya kazi kama wanavyozipigia chapuo wenye nazo hazitaonyesha tofauti hata kidogo kwenye kwa nchi yetu. Kwa uzoefu wa mawimbi ya corona yaliyopita hili nalo litapita na watu wengi watabaki hawajachanja na chanjo ya corona itakuwa irrelevant. Gwajima wins, na maana yake hiyo ni kubwa sana kisiasa na kisaikolojia.

Suala la pili ni la ushawishi. Wanaotetea chanjo wana hoja moja tu ya maana, kwamba kama chanjo ya corona mnaitilia shaka mbona hamtilii shaka madawa mengine yanayotoka nchi za kibeberu? Kama wazungu wangetaka kuwaua si wangewaua kwa ARVs? Bla bla kama hizo. Gwajima na watu wenye mawazo kama yake wana hoja kinzani zinazopenya kwenye maisha ya kawaida ya watu wa kawaida kabisa. Kwa watu wengi tulio wa kawaida kiukweli tumaini letu la afya halipo kwenye dawa za kizungu. Tanzania ni nchi very religious na ni ukweli kwamba kwa nchi ambayo watu wengi wamekufa kwa malaria (misaada ya maana kutoka nchi za nje ni net za mbu) na kwa nchi ambayo watu wengi wamekufa kwa HIV (msaada wa maana ni ARVs zinazowafanya watu watumwa wa hizo dawa na kubaki dhoofu maisha) sidhani kwamba leo hii wataliona suala la chanjo ya corona kama ni suala la kufa na kupona. Tumaini la watanzania limebaki kuwa kudra za Mwenyezi Mungu na ndio maana watu kama akina Gwajima wanaonekana kuwa common sense katika hili. Kama kweli serikali inawajali watu kwenye inshu ya corona where are real ventilators? How many ICU beds equipped with modern ventilators? Waliowaletea msaada wa chanjo kwa nini wasiwape msaada wa ventilators kwanza kabla ya hizo chanjo?

Mwisho Gwajima ana hoja na anashawishi, wakati wenye mamlaka wamejikunyata hata hawawezi kuitetea hiyo chanjo yao ya kupewa. Kuna ombwe kubwa la uongozi kwenye hii nchi na hii ni hatari sana.
 
Uko sahihi! Kuna tatizo sehemu mtu anahoji chanjo lakini aliuhua anakwenda hospitali ambako madawa yote yanatoka kwa hao hao wazungu wanaosemekana kuwa hawatupendi.
 
Kutumia hisia kwa mambo yanayohitaji utafiti ni janga la kitaifa. Corona imetusaidia kujua kiwango cha uelewa miongoni mwetu watanzania. Kuna watu wanatumia consipiracy kupata publicity kama akina gwajima niwakupuuza. Tuliosoma political psychology tunajua ujinga wa gwajima vyombo vyetu vya ulinzi vinamcheki tuu
 
Hadi miaka 10 ifike virusi watakuwa wamemaliza hizo akili chache za kuvukia barabara ulizobaki nazo.
 
Nao watakuona hamnazo. Achana na kujisumbua na uamuzi wa mtu, angalia mbele. Kama unaweza shauri tu halafu jiishie upate amani moyoni
 
Huna makala zingine za kuandika? Unategemea mawazo ya watu wote yatakuwa sawa kuhusu chanjo?
Usalama wa hizo chanjo unazijua, uko na utafiti kuhusiana na hilo?
Mwisho, kila mtu ashinde mechi zake.
 
Huna makala zingine za kuandika? Unategemea mawazo ya watu wote yatakuwa sawa kuhusu chanjo?
Usalama wa hizo chanjo unazijua, uko na utafiti kuhusiana na hilo?
Mwisho, kila mtu ashinde mechi zake.
usalama wa hizo chanjo naujua kwasababu nimechanjwa na nipo salama! kazi kwako kudhibitisha kama sipo salama
 
Kwa hiyo ww ni mtafiti kuwazidi hao wazungu wenyewe wanaopingana ?
 
Kwa hiyo ww ni mtafiti kuwazidi hao wazungu wenyewe wanaopingana ?
unajua wazingu mpaka leo wamechanja wangapi? nani kakwambia wazungu wanapinga chanjo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…