Sijui kwanini, nahisi kama Kassim Majaliwa Majaliwa atang'olewa Uwaziri Mkuu kabla ya 2025

Sijui kwanini, nahisi kama Kassim Majaliwa Majaliwa atang'olewa Uwaziri Mkuu kabla ya 2025

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Hisia zangu zinazonionesha kuwa Kassim Majaliwa Majaliwa anapwaya sana katika timu ya Mama Samia hazijaja bure, bali nimekuwa nikimtazama na kumfatilia sana utendaji wake katika hii miaka miwili akiwa chini ya Mama Samia, kwa
kumliganisha na hapo alipokuwa chini ya mwendazake.

Hata hivi sasa namuona akiwa bungeni kwenye hotuba ya bajeti akiwa ni kama mtu ambae hana raha kabisa, ni kama mtu aliyechoka na anajisukuma tu, siioni kabisa hamasa binafsi.

Ama anaumwa ama mengine zaidi.

Huu siyo utabiri bali ni uchambuzi wangu binafsi wa kawaida tu. nimeona nimsanuwe.
 
Kwasababu katiba yetu inatupa marais DHAIFU.

kwahiyo Waziri Mkuu akiwa HODARI analazimishwa KUDHOOFISHWA.

Tuliona kipindi cha JK, Lowassa alikuwa FIRM Prime Minister akaundiwa Zengwe akalazimiswa ng'atuka.

Magufuli alikuwa Rais IMARA, alikuwa na Majaliwa Imara hivyo hakuna aliyehisi mwenzake anataka mpoka sifa.

MAMA ni WEAK.... anahitaji the WEAKEST PM, otherwise atajihisi na anajihisi hata sasa anafunikwa na PM.
 
Hisia zangu zinanionesha kuwa Kassim Majaliwa Majaliwa anapwaya sana jatika timu ya Mama Samia hazijaja bure, bali nimekuwa nikimtazama na jumfatilia sana utendaji wake katika hii miaka miwili akiwa chini ya Mama Samia kwa
kumliganisha na hapo alipokuwa chini ya mwendazake.

Hata hivi sasa namuona akiwa bungeni kwenye hotuba ya bajeti akiwa bi kama mtu ambae hana raha kabisa, ni kama mtu aliyechoka na anajisukuma tu, siioni kabisa hamasa binafsi.

Ama anaumwa ama mengine zaidi.

Huu siyo utabiri bali ni "analysing" yangu binafsi ya kawaida tu, nimeona niisanuwe.
Ni «analysis» siyo «analysing». Halafu «jumfatilia» ndiyo nini? Huna lolote wewe. Kaa kimya na «mama» wako wa mchongo. Hapo ndiyo umeandika «analysing» yako?
 
Back
Top Bottom