Sijui kwanini nimeumia hivi

Mimi sioni haja ya kumtafuta. Huyo ni rafiki anaependa kusaidiwa ila siku ukipata shida, haitatokea akajitoa au hata tu kuifikiria shida yako. Majibu yao ni mimi sina basi, afu anaendelea na yake.

Na wewe kaa kimya,afu Maisha yaendelee,usijitie tena kiherehere kwenye mambo yake.
 
Yaani nashindwa kueleza ninavyojiskia,, sihitaji anilipe chochote wala chochote ila tu nimeumia ndomana najishangaa kwanini inakua hivi hadi nashindwa kujizuia.. Hata sielewi naumia nini yani
Huyo we mchane live ndio utapata unafuu tofauti na hapo utaumia sana. Baada ya hapo mtoe kwenye list
 
Tenda wema, nenda zako!
 
Pole sana Mungu atakulipa kwa msaada wako wala usimtafute asione unaomba asante yako we piga kimya tu au kama vipi mchane aache tabia mbaya
 
Mie yameshanikuta Mara nyingi huwa hata sipend kumbuka kabisaaa

Unasaidia watu wanageuka kuwa kichomi kwako !!!!

Kichomi kichomi kweli kwelii!!!
 
Aisee
 
Alafu unatoka Songea Mjini mpaka Peramiho mission mbali kinoma, Anyway take it easy but punguza kujali sana
 
Aisee.

Huyo rafiki yako bila shaka anakuonea wivu kwa namna moja au nyingine hatua uliyopiga kimaisha .

Kataa urafiki naye nyoka huyo na usitegemee ukipata shida atakusaidia.
 
Mkuu kwa jinsi alivyo atarudi tu,, maana hij ni mara ya pili namsaidia halafu inatokea vilevile.. Sijui hata natakiwa kufanya nini, ila ngoja nimpigie kwanza simu nitarudi
Punguza shobo na kujikomba komba.

Achana naye kabisa kama hakijatokea kitu.

Balance shobo narudia tena!!!
 
Pole sana mkuu. Cha kujifunza hapo ni kwamba tambua always binadamu huwa na second option kwenye jambo lolote lile. So hata wewe ulikuwa kwenye option tu moja wapo na uliona kwamba usingemsaidia asingesaidiwa na mwingine but kumbe haikuwa hivyo. The thing is ameu disvalue mchango wako huwezi jua kwanini lakini bora umefanya hivyo coz usingemsaidia ungepata msononeko wa nafsi yako kutokana na empathy. Ondoka na funzo kwamba sasa umemjua vizuri tabia yake hata ikitokea next time una reference ya kuelezea. Amekuumiza lakini imekuwa faida ya kumjua vizuri and that's how most human beings are.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…