Sijui kwanini nimeumia hivi

Sijui kwanini nimeumia hivi

Kuna sababu, Mungu alikuwa anawatumia kwa sababu zake, mshukuru Mungu umeweza kufanya alichokuwa anataka wewe na familia yako mfanye, usiumie wala kuweka kinyongo, mkikutana mwambie ukweli, na iishie hapo usimchukie wala kumpotezea... Siku moja utakuja kunishukuru kwa huu ushauri wangu..

Afu mtoto mzuri bado unakaa nyumbani kweli na kazi unafanya? Nilete posa?
 
Shida tuna saidia kwa kutegemea malipo, shida ina anzia hapo tuu Mwisho wa siku kusamehe kuko pale pale, TUISHI kwa kusameheana na kusaidiana haijalishi nini kimetokea baina yetu mkuu.
Kusamehe tunasamehe na ndo maana hata tukiambiwa wana matatizo sometimes tunajigusa lakin hatutajimaliza kwa sabbu yao. Yani kama iko ndan ya uwezo fresh, haiko ndani ya uwezo basi hatuna!!! People are very toxic mkuu, by the way hatuhitaji malipo na ndo maana hatutoi risiti ndugu basi na wewe kaishi nao huo msaada sio baadae tunakuja kusikia maniaje mengine pembeni...
 
Ni kweli 💯, sasa hutakiwi umia moyo maana ukweli una ujua weww hujafanya hivyo eti kutoa kafara. Hiyo ni uwezo mdogo wa akili yao kushindwa kufikiri.
Pole sana ila piga moyo konde ila usichoke saidia kama uko na uwezo.
Nikiwa na uwezo...hapo tumeagree. Achana na habari za kutumia akili kwenye mambo ya hisia maana tunafanya kwa upendo na kujali ndugu maana tungesema tutumie akili tungewaza wazazi wake walikuwa wapi wasimsaidie. Hiyo yote ni upendo so hata mambo yakibackfire ni hisia zetu zimejeruhiwa. Am a peace ambassador though...maRas tunasema one love
 
Kusamehe tunasamehe na ndo maana hata tukiambiwa wana matatizo sometimes tunajigusa lakin hatutajimaliza kwa sabbu yao. Yani kama iko ndan ya uwezo fresh, haiko ndani ya uwezo basi hatuna!!! People are very toxic mkuu, by the way hatuhitaji malipo na ndo maana hatutoi risiti ndugu basi na wewe kaishi nao huo msaada sio baadae tunakuja kusikia maniaje mengine pembeni...
Huyo ni ndugu lawama. Mjue mtu ishi kulingana na alivyo Mkuu.
 
Pole
Simu hufanya tuwe karibu na watu walio mbali nasi na tuwe mbali na watu walio karibu yetu.

Nawe ungetumia ile laki mbili huwenda muamala wako ungewekwa status.
 
Habari za asubuhi wana JF,

Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.

Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.

Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.

Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli tukamshawishi mzee bila hiyana akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.

Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.

Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini walikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.

Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtumia hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi na kitu hivi na amewataja na majina kabisa...

Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambia na mimi niende kwake kumuona( Nilikua nasoma tarehe na muda wa zile transactions ).

Mimi ambaye nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.

Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee, sijui nifanye nini nikae sawa😥😥
Uzuri wake shida mwanaharamu haziishi atarud tu wew mshukuru mungu
 
Duuuh! kesi kama hii nilihadithiwa na dada mmoja hivi,alimtendea mwenzake wema,akashangaa alivyoruhusiwa hospitali,hata hajawahi kumpigia simu mwenzake,yaani hata kumjulisha tu kua wameruhusiwa,mbaya zaidi hadi mama wa yule dada akiyemsaidia mwenzake,anaulizia kama anaendeleaje... yule dada anajibu kua wanaendelea vizuri na wameruhusiwa,ila ndo hivyo mgonjwa hakutoa hata shukrani,mbaya zaidi dada aliyekua anamsaidia,siku ya mwisho alikua kabeba na chakula,akitarakia kua atawakuta(mgonjwa na mwanae).
Anyway tusaudie tu.
 
Umeona tabia zenu wanawake sasa, hapo tatizo ni kwamba wewe hujampa hela bali umetatua shida zake... Kwahiyo kikwenu kwenu mnaonaga kama kusolve issue sio kitu cha thamani kama kupewa hela.... Ndo maana mwanaume aliekuoa anaweza akakulisha kila siku na kukuvesha ila ukaja kumuona si kitu kama yule anaekutumia 15000 ya kusuka kila week.
 
Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.
Utasikia Nyege zikikolea, Bwana wee kama hutaki Mi nitazaa na nitalea mwenyewe.

Sasa kabaki mwenyewe analaumu watu hawajampa pesa hadi jioni.
 
Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambia na mimi niende kwake kumuona( Nilikua nasoma tarehe na muda wa zile transactions ).
Sasa mnaelewa kwa nini Mtu anakuwa Single Maza, sio kwa sababu K yake mbaya bali Tabia.

Mimi najua fika Single maza anakuwa single maza sababu ya Tabia zake.

Wenye Tabia nzuri hata kama ni single maza watoto wawili bado wanaolewa na kuishi vyema.
 
Back
Top Bottom