Sijui kwanini nimeumia hivi

Sijui kwanini nimeumia hivi

Pole ndo ukubwa huo mi siku hizi nimekuwa na roho mbaya baada ya kupigwa vitu vizito huko nyuma yani shida za mtu wa karibu sijui ndg au nani nani hazinigusi kabisaaa ndo ije kuwa classmate,
Sasa wewe siku zikikukuta? Unaona Kwa kuwa umezipata unadhani Umemaliza Safari?

Safari bado ndugu yangu ukipigiwa simu pokea.
 
Yaani nashindwa kueleza ninavyojiskia,, sihitaji anilipe chochote wala chochote ila tu nimeumia ndomana najishangaa kwanini inakua hivi hadi nashindwa kujizuia.. Hata sielewi naumia nini yani
Na hiyo miamala ameiweka kumkomoa Baba watoto ambaye hajatuma hata mia.

Baadhi ya wanawake ni wajinga sana.
 
Siku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.

Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.
Nyinyi ndio huwa hamtoi msaada.......hamjui faida ya Shukrani.

Mungu mwenyewe anataka Tumshukuru na ana kila kitu.

Shukrani ni Ibada Ndugu.

Asiyeshukuru kwa kidogo hata kikubwa hawezi kushukuru.

Ni maneno ya Yesu mwenyewe
 
Binadamu wabaya lakini nnafikiri usingehangaika kumdanganya baba ili akupe 150k naona hapo ndio pabaya zaidi na itakuuma zaidi
Kama huna hata kuna shida gani sema sina au toa kiasi unachoweza
Binadamu wa leo wamekuwa na roho mbaya sana na washenzi haswa
Mtu anakuambia nina njaa unampa hela halafu unamkuta kalewa chakari

Yaani kila leo tunaona watu wa aina aina ila pole sana
Delete her number na akikusemesha mwambie nimekujua ulivyo mind your own business
 
Siku zote ishi kwa kusaidia bila kutegemea malipo yeyote. Iwe ya shukrani ama chochote.

Kwa sababu hata shukrani isingekuongezea chochote.
Kwa hiyo mkuu, tukio hilo mfano ndiyo ingelikuwa ni wewe umetendewa mema na mtu tena wakati ukiwa hauna kitu, hauwezi kusema hata ahsante kwa ajili tu ya kuenzi misemo ya wahenga waliosema 'tenda wema uende na usingojee shukrani'?

Mtoa mada kajieleza vizuri sana kuwa hakuhitaji chochote toka kwa muuguliwa bali ni simple ahsante ama taarifa tu ya siha ya mtoto na kuachiliwa kwao toka hospitali.
 
Habari za asubuhi wana JF,

Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.

Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.

Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.

Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli tukamshawishi mzee bila hiyana akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.

Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.

Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini walikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.

Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtumia hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi na kitu hivi na amewataja na majina kabisa...

Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambia na mimi niende kwake kumuona( Nilikua nasoma tarehe na muda wa zile transactions ).

Mimi ambaye nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.

Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee, sijui nifanye nini nikae sawa😥😥
Tenda wema nenda zako.
 
Binadamu wabaya lakini nnafikiri usingehangaika kumdanganya baba ili akupe 150k naona hapo ndio pabaya zaidi na itakuuma zaidi
Kama huna hata kuna shida gani sema sina au toa kiasi unachoweza
Binadamu wa leo wamekuwa na roho mbaya sana na washenzi haswa
Mtu anakuambia nina njaa unampa hela halafu unamkuta kalewa chakari

Yaani kila leo tunaona watu wa aina aina ila pole sana
Delete her number na akikusemesha mwambie nimekujua ulivyo mind your own business
Kwakweli, ila nimejifunza kitu japo in a hard way
 
Sasa mnaelewa kwa nini Mtu anakuwa Single Maza, sio kwa sababu K yake mbaya bali Tabia.

Mimi najua fika Single maza anakuwa single maza sababu ya Tabia zake.

Wenye Tabia nzuri hata kama ni single maza watoto wawili bado wanaolewa na kuishi vyema.
Kwakweli nimejua, Mungu tu atusaidie
 
Huwa mnakuja kuwashutumu wanaume wanazalisha na kuwaacha wanawake (single moms)
Ukimuona mtu kazalishwa na hajaolewa. Usimlalamikie aliyemzalisha na kumuacha maana unaweza kuwa na mipango na mwanamke kumuoa ila kutokana na ujinga wake. Unamuacha tu
Yeah kuna baadhi ya tabia hazivumiliki walai, nimeamini
 
Napenda sana watu wa hivi 😂😂😂 yaani mtu anakuwa amejikatia ticket mazima.

Pole sana Leejay49 kuna msemo unasema hivi; ukubwani ukianza kuinteract na watu ndio utajua ni kwakiasi gani wazazi wako walikulea vyema 😂
Tatizo wengine roho mbaya hatuwezi hata tujifunze namna gani, ndio hapo tunaishia kuumia tu..
Asante mpenzi binti kiziwi
 
Back
Top Bottom