Sijui kwanini nimeumia hivi

Sijui kwanini nimeumia hivi

Na hata kupigia nakuambia,Akipiga atakuja na excuse ya kitoto kweli.Ndivyo walivyo.

Atakuweka karibu akiwa na tatizo tena trust me.

Wewe ni daraja,Kuwa daraja ni kazi sana
Binafsi Nime deal na watu wa hivyo wengi mno.Nilipopata somo kwama mimi ni daraja nikaona.Ila nimepumguza huruma.Sababu mtu wa hivyo hata siku ukiwa na shida ya mia mbili hutaipata kwake.
Nimeliona hilo mkuu, Nashukuru Mungu nimejifunza japo in a hard way, ila nitabadilisha namna ya kuwatazama na kudeal na watu
 
Huruma isipungue bhana , unajua msaidie mtu kama umeguswa na anayo yapitia kwa kujipa amani yako ww mwenyewe kwa kuona angalau ule ugumu kwa huyo mtu umepungua , bila kuweka matarajio ya malipo ya aina yoyote kutoka kwa yule mtu , matarajio ndio yana waumiza watu pale yanapokwenda kinyume .
Bro nishapigwa matukio mpk yesheeeeee sina huruma za bei rahisi hivyo
 
kwanza nine jisikia faraja kusikia ume tenda wema.

kuhusu shukrani USI iwazie sana mkuu, binadamu Wana differ Sana huenda hakukuona Kama mtu wake wa karibu.

kingine uki kutana nae USI igize unafiki, just laugh a little Kisha tembea zako. Mana she doesn't deserve your attention again.

And last Nili jua ana hitaji counselling, Ninge Sema mlete tu🤓😂
Asante kwa ushauri mzuri mkuu
 
Ndo maana nasema bado hamjanielewa.

Mungu ndo anaweza saidia kila mtu, sio binadam mwenzake.

Huyo mtoto sio responsibility yake, ni responsibility ya mzazi ambae ni rafiki tu kwake. Kwa logic yako hapo juu basi aende hospital akasaidie wagonjwa wooote ambao wanaundugu na rafiki zake sasa

Bado hujanielewa. Narudia tena, mwenye uwezo wa kusaidia kila mtu ni Mungu, sio binadamu. Saidia unapoweza ukishindwa acha, wala sio dhambi, ni common sense, but common sense is not aways common
Bado hujanielewa na wewe, natafuta hoja yako ya kujifanya Mungu inatoka wapi kwenye incident hii, unafikiri kwa nini huyu ambae hakuwa na hela nae akaomba tena ndio akapata hela nyingi kuliko walikuwa nazo cash lkn wakatuma buku ten, huyu aliyekuwa hana akapata laki 2+ umeona uponyaji wa huyo mtoto umepatikana kwa aliyeenda kuomba,
Wewe umetuambia ukiwa huna pesa usisaidie kwa kuwa utatafuta Umungu Mtu kitu ambacho ni sawa kwa baadhi ya matukio lkn sio hili.
Dunia ya ajabu sana hii, nikiwa na miaka kama 8 au 9 niliwahi kuokolewa kwenye hatari ya kufa na binti mmoja hapo mtaani kwetu aliyekuwa na upungufu wa akili (tahaira, sijui kama nimepatia) wenye utimamu wa akili wote walitoka nduki.
Hoja yako ya umungu mtu labda niielewe hivi usiende kukopa benk, vikoba, kwa mtu nk kwa ajili ya mtu aliyekuomba hela ya harusi yake.
 
Kiubinadamu inaumiza ila kuna uzi upo humu unahusu watu wema kwa nini Mungu huwachukua mapema kuliko hata muda ambao jamii/familia inavyowahitaji. Fact ambayo imeungwa mkono na wengi ni kwamba sifa, utukufu na shukrani wanazopata kutokana na huo wema unabeba sifa na utukufu wa Mungu. Hivyo Mungu anabeba hicho kiumbe chenu mnachokipa utukufu kuliko yeye ili awaonyeshe kuwa YEYE ni MKUU kuliko huyo.
Unapaswa ushukuru kwa alichokifanya ili wewe ubaki salama mikononi MWAKE.
 
Pole sana kwa yaliyokukuta....ubinadamu kazi!

Ila kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako inaelekea kuna namna umemkwaza wakati unamsaidia(aidha kwa maneno au matendo), jitafakari.

Kwa mazingira ya kawaida hawezi kumshukuru aliyetoa elfu tano akakuacha wewe wa laki tatu.
Angeacha kushukuru wote ingeeleweka kwamba ni mtu asiyekuwa na shukurani.
Kuna watu huwa na roho ya kutothamini watu Fulani harafu wanathamini watu wasio wathamini.
 
Jumla unetumia kama laki 4 hivi.. ambayo ungekaa na familia yako hapo mle KUKU kila siku mngekula KUKU kwa takribani miez miwili.. kila siku ni KUKU tu.

Ah.. ktk swala la Fadhila... huwa sitegemei saana maana yashanikuta, na nikajifunza kuwa natoa hichi ki2 ili kisaidie tu na wala sihitaji any kind of feedback.

And, kizuri zaidi huwa naomba nikutane na watu kama huyo Dada hapo.. huwa ananirahisishia sana endapo baadae akirudi niweze kumchinjia baharini bila HURUMA yoyote ile... tofauti na yule uliyemsaidia na akaonesha positive feedback ya msaada wako, akirudi utapigana tena kumsaidia.. ila hawa wanaojitoa akili ndio wazuri.. akijikausha kama hivyo na ww unamsubiri tu aingie tena kwenye Mfumo.
Yani akiingia kwenye mfumo lazima afurahi😃😃😃
 
rafiki yangu usiumie hapo huja msaidia huyo rafiki yako... aliekuwa na shida ni huyo malaika...! ambae kupitia wewe amepata kupona...!

ambae nina amini ipo siku isiyo na jina atakuja kukushukuru... iwe kwa kutamka au kwa vitendo ila shukrani ya kumsaidia huyo mtoto utaipata.

na inawezekana muda sio mrefu ukapanda cheo au ukapata ajira nzuri zaidi ya hiyo unayo fanya lolote jema kubwa litakalo kutokea ujue ni sauti ya yule mtoto ulieokoa maisha yake.

wala usinung'unike... mtu akikufanya mjinga wewe mpuuzie...!​
 
Ndo maana nasema bado hamjanielewa.

Mungu ndo anaweza saidia kila mtu, sio binadam mwenzake.

Huyo mtoto sio responsibility yake, ni responsibility ya mzazi ambae ni rafiki tu kwake. Kwa logic yako hapo juu basi aende hospital akasaidie wagonjwa wooote ambao wanaundugu na rafiki zake sasa

Bado hujanielewa. Narudia tena, mwenye uwezo wa kusaidia kila mtu ni Mungu, sio binadamu. Saidia unapoweza ukishindwa acha, wala sio dhambi, ni common sense, but common sense is not aways common
Skia, huyo Mungu aliweka watu ili hao watu wawe msaada kwa watu wngn. Sasa ww kaa ndani na shida zako ukimuomba Mungu bila kutoka nje kwa watu uone kama huyu Mungu atakusaidia
 
Back
Top Bottom