Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwaiyo kutokuwekwa status imekuuma je kama alikuweka na ulivo busy hukuiona hadi ikaondoka?Habari za asubuhi wana JF,
Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.
Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.
Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.
Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli tukamshawishi mzee bila hiyana akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.
Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.
Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini walikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.
Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtumia hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi na kitu hivi na amewataja na majina kabisa...
Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambia na mimi niende kwake kumuona( Nilikua nasoma tarehe na muda wa zile transactions ).
Mimi ambaye nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.
Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee, sijui nifanye nini nikae sawa😥😥
Mamaaa🤔🤔🤔.. Hiyo mbona inaogopeshaNi kweli lakini pia biblia imetutaka tuwe na kiasi. Unamsaidia mtu, umemnunulia bodaboda ajikwamue kiuchumi, bahati mbaya baada ya miezi 5 akapata ajali akafariki. Ukoo mzima unakaa kikao kwamba wewe umemtoa kafara, unasikia hayo maneno utajisikiaje?? Mbaya zaidi ulifanya kwa upendo...je akija ndugu mwingine utamnunulia tena bodaboda? Sio kwamba tutaacha kutoa fedha hapana tutatoa lakin tunakuwa na ukomo. Kujimaliza tena kwa ajili ya undugu wa fedheha na toxicity its a big NO!!!!
Mkuu angenipa tu taaarifa kuwa wameruhusiwa na wanaendelea vizuri wala nisingeshuhulika nao. Imagine mda anaweka hizo status nimempigia zaidi hata ya mara5 , nyumbani nimewakosa nimeenda tena hadi hospital na kulivyo mbali naambiwa wameruhusiwa, hapokei simu na yuko online anaweka status kma hizo, ungejiskiaje ungekua ni wewe??? Usingehisi kudharauliwa maybeKwaiyo kutokuwekwa status imekuuma je kama alikuweka na ulivo busy hukuiona hadi ikaondoka?
Ushauri mzuri mkuu, Asante..Kuna sababu, Mungu alikuwa anawatumia kwa sababu zake, mshukuru Mungu umeweza kufanya alichokuwa anataka wewe na familia yako mfanye, usiumie wala kuweka kinyongo, mkikutana mwambie ukweli, na iishie hapo usimchukie wala kumpotezea... Siku moja utakuja kunishukuru kwa huu ushauri wangu..
Afu mtoto mzuri bado unakaa nyumbani kweli na kazi unafanya? Nilete posa?
Mungu akubariki sana.Habari za asubuhi wana JF,
Iko hivi, nina rafiki yangu ana mtoto (naweza nikasema ni single mom) ila isieleweke vibaya, nilisomaga nae O level huko ila nikama bahati tu tumejikuta tunaishi tena mtaa mmoja.
Ijumaa jioni wakati natoka tu ofisini alinipigia Simu akaniambia anashida kama naweza nipitie nyumbani kwao nikamuone, kwakua nilikua sina ratiba nyingine nikasema isiwe tabu kabla sijafika nyumbani nikapitia.
Nilimkuta yuko good ila mwanaye alikua anaumwa sana ile mtoto kazidiwa na akaniambia ameshindwa kwenda hospitali hana hela na almost kila aliyempigia simu wamemuahidi tu tangu asubuhi na hakuna aliyemtumia mpaka muda huo sa 1 jioni inaelekea saa 2.
Kiukweli sikua na hela and i was totally broke, yaani wiki ile iliyoisha mwenyewe nimeishi tu kwasababu nina wazazi maana nilikua nina mambo mengi yananihitaji hela kiasi kwamba sikua nimebakiwa na hata Mia mbovu. Lakini nikasema kwenye suala la kuokoa maisha ya mtoto isiwe kesi nikamwambia ngoja nirudi kwanza nyumbani, nikamsimulia mama tukaongea na dada yangu wakasema tu hapa kwa harakaharaka hatuna namna tumdanganye tu mzee kitu chochote jioni hii atupe hela, kweli tukamshawishi mzee bila hiyana akanipa 150k nikamfata kwao tukaenda hospitali usiku uleule.
Mtoto akapewa huduma ya kwanza na baadhi ya vipimo wakamlaza ili asubuhi aendelee na matibabu mengine (muda wote huo anawapigia ndugu zake wakiwemo na baba wa mtoto hata simu hawampokelei wengine), asubuhi yake niliomba ruhusa kazini nikawaambia nitachelewa ili nione mtoto atakua anaendeleaje.
Case ya mtoto ikawa kubwa wakasema tuende nae hospitali nyingine kubwa (Peramiho nadhani watu wa songea wanaijua), kuna vipimo alivyoambiwa wampime vilikua vinahitaji hela almost kama laki 2 tena nikamwambia mama akanitumia tukafanikisha. Kwasababu kazini walikua wanapigapiga sana simu na nikaona wanaendelea vizuri na mama yake alikua ashafika nikamwambia naenda ofisini incase kimetokea chochote utatuambia nikampa na namba ya mama kama mimi nisipopokea ampigie, nikaondoka. The bad thing is nilikua busy busy sana hadi siku ikaisha sikuwatafuta tena.
Kinachoniumiza ni kwamba, jana mchana nilimpigia simu hakupokea nikaenda kwao sikukuta mtu, nikaenda hadi Peramiho tena kulivyo mbali nikaambiwa wameruhusiwa na hakunipa taarifa. Jioni nimeingia WhatsApp naona ameweka status nyingi nyingi kufungua nikawa naona amescreenshot miamala yote ya watu waliokua wanamtumia hela na kuwapa credits Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya mwanae maana alikua kwenye hali mbaya sana na nini nini. Screenshot kama kumi na kitu hivi na amewataja na majina kabisa...
Cha ajabu hiyo miamala hakuna hata wa mtu mmoja uliofikia hata 30k, wote ni hizo hizo tu efu10 ef5 ef7, kawaandikia macaption mazito mazito. Nimebaki najiuliza mbona alikua ananiambia hawapokei simu, na hela inaonekana walimtumia siku ileile ambayo aliniambia na mimi niende kwake kumuona( Nilikua nasoma tarehe na muda wa zile transactions ).
Mimi ambaye nilikua nae kuanzia siku ile hadi usiku nikaacha na kwenda kazini na tumeclear bills zote hata asante hajaniambia na wala taarifa kama wameruhusiwa hajanipa. Nimesubiri jana yote hadi leo saizi hajanipigia hata simu, Kina mama wananiuliza wanaendeaje nawaambia tu wanaendelea vizuri huku roho inauma.
Nimetenda wema nimeenda zangu wakuu, lakini bado roho inaniuma aisee, sijui nifanye nini nikae sawa😥😥
Inaumiza sana mkuu,, sema ndio hivyo hatuwezi acha kusaidiana tunapambana nao hivyo hivyoDuuuh! kesi kama hii nilihadithiwa na dada mmoja hivi,alimtendea mwenzake wema,akashangaa alivyoruhusiwa hospitali,hata hajawahi kumpigia simu mwenzake,yaani hata kumjulisha tu kua wameruhusiwa,mbaya zaidi hadi mama wa yule dada akiyemsaidia mwenzake,anaulizia kama anaendeleaje... yule dada anajibu kua wanaendelea vizuri na wameruhusiwa,ila ndo hivyo mgonjwa hakutoa hata shukrani,mbaya zaidi dada aliyekua anamsaidia,siku ya mwisho alikua kabeba na chakula,akitarakia kua atawakuta(mgonjwa na mwanae).
Anyway tusaudie tu.
Kama kuna ukweli hivi🤔Umeona tabia zenu wanawake sasa, hapo tatizo ni kwamba wewe hujampa hela bali umetatua shida zake... Kwahiyo kikwenu kwenu mnaonaga kama kusolve issue sio kitu cha thamani kama kupewa hela.... Ndo maana mwanaume aliekuoa anaweza akakulisha kila siku na kukuvesha ila ukaja kumuona si kitu kama yule anaekutumia 15000 ya kusuka kila week.
Bora umenielewa mkuu, AsanteKwa hiyo mkuu, tukio hilo mfano ndiyo ingelikuwa ni wewe umetendewa mema na mtu tena wakati ukiwa hauna kitu, hauwezi kusema hata ahsante kwa ajili tu ya kuenzi misemo ya wahenga waliosema 'tenda wema uende na usingojee shukrani'?
Mtoa mada kajieleza vizuri sana kuwa hakuhitaji chochote toka kwa muuguliwa bali ni simple ahsante ama taarifa tu ya siha ya mtoto na kuachiliwa kwao toka hospitali.
Aaah hapo sawaYani kwa taarifa fupi bado najitafuta wao ndo wamejipata
Kuna watu wana roho ngumu.....Asante ya mdomo tu hawezi kusema.Kwa hiyo mkuu, tukio hilo mfano ndiyo ingelikuwa ni wewe umetendewa mema na mtu tena wakati ukiwa hauna kitu, hauwezi kusema hata ahsante kwa ajili tu ya kuenzi misemo ya wahenga waliosema 'tenda wema uende na usingojee shukrani'?
Mtoa mada kajieleza vizuri sana kuwa hakuhitaji chochote toka kwa muuguliwa bali ni simple ahsante ama taarifa tu ya siha ya mtoto na kuachiliwa kwao toka hospitali.
Una roho mbaya kuliko wote humu jfAaah hapo sawa
Watu wa hivi ni kama amekudhihaki kwa msaada uliompa.Binadamu wabaya lakini nnafikiri usingehangaika kumdanganya baba ili akupe 150k naona hapo ndio pabaya zaidi na itakuuma zaidi
Kama huna hata kuna shida gani sema sina au toa kiasi unachoweza
Binadamu wa leo wamekuwa na roho mbaya sana na washenzi haswa
Mtu anakuambia nina njaa unampa hela halafu unamkuta kalewa chakari
Yaani kila leo tunaona watu wa aina aina ila pole sana
Delete her number na akikusemesha mwambie nimekujua ulivyo mind your own business
Hahahaa.......Una roho mbaya kuliko wote humu jf