Sijui ndio tuwaite washamba au limbukeni wa magari?

Sijui ndio tuwaite washamba au limbukeni wa magari?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Asubuhi ya leo nimetoka nyumbani Mapinga kuelekea kazini.

Kama kawaida nikakunjia Boko Magengeni kuelekea njia ya Mbweni JKT ili nikatokee Ununio hadi Kunduchi kuelekea Mwenge kwa njia ya kuingilia Clouds Media.

Nilikuwa na Escudo langu edition ya Singapore, niko kwenye mwendo wangu wa kawaida tu wa 100/km mida ya saa 12 bado wadau hawajawa wengi road!... kama ilivyo kwa watu wengi wanaowahi kazini asubuhi. Kila mmoja ana safari yake!!

Kwa muda nikawa nyuma ya Land Cruiser GX yenye namba EDJ. Jamaa alikuwa kibati sana nami nikawa nafuatana nae si kinyonge tangia tukiwa Mbweni roundabout-Ununio then Kunduchi....

Kwenye ile njia ya chini ya Kunduchi, wenyeji wanaijua vizuri; asubuhi magari mengi yanatanua na yanakuwa kibati cha kutosha....watu wanawahi zao job!

Tulipofika usawa wa Kota za Polisi Kunduchi, jamaa akaruka tuta la ile down, nami nikaruka nyuma yake. Akaruka lile la pili baada ya kumaliza ile down nami nikaruka!.

Ghafla baada ya kuruka tuta akasimamisha chuma lake akaegesha pembeni mbele yangu kiasi cha kunifanya nami nipunguze mwendo na kusimama.

Nikadhani labda amepata hitilafu ya gari ili nikunje zangu kulia nisepe.

Kabla sijaanza kuondoka, akanizuia, akashuka kwenye gari yake na kuja niliposimama.

Nikashusha kioo nikamuuliza, "Kuna shida?"

Akaniambia: "Mbona unanifuatilia?"
Kwa kweli nilibaki nimeshangaa.

Nikamuuliza, tangu lini kuendesha gari nyuma ya gari lingine kwenye barabara ya umma ikawa ni kumfuatilia mtu na ni asubuhi kweupe wala sio maporini?

Hapa kila mmoja anaelekea uelekeo wake!. Why useme nakufuatilia!!

Sio kila gari lililo nyuma yako lina maana linakufuatilia! Kwamba kwa sababu wewe uko na mbio nami na mbio nikiwa nyuma yako ndio nakufuatilia, liko wapi kosa hapo!?


Tukabadilishana maneno kwa muda wa dakika mbili 3 pale!!!

Nikamweleza kuwa sikuwa namfuatilia wala sikuwa na tatizo lolote naye.

Sikuwa nimemgonga, sikuwa nimemkwaruza gari, wala sikuwa nimemzuia kupita. Nini shida yake.

Barabara ni ya wote.

Uwe unaendesha Land Cruiser, Prado, V8, bajaji, honda au Escudo ya miaka ya nyuma, hakuna anayepaswa kujiona anaimiliki njia au kuamua nani aruhusiwe kuwa nyuma yake, mradi kila mtu anazingatia sheria na usalama barabarani.

Mwisho wa siku akarudi kwenye gari yake akionesha dole la kati nami nikajirudishia na kila mmoja akaendelea na safari yake.

Nikajiahidi angeleta za kuleta stori zingekuwa nyingine.

Kwa kweli kuna baadhi ya madereva wanaonekana kuamini kwamba akiwa barabarani na gari la thamani kuwazidi wenzake anaweza akawaamrisha kufanya lolote;

Somo:
  1. Tuwe wastaarabu barabarani.
  2. Barabara ni ya wote, na kila mmoja ana haki ya kuitumia kwa kuzingatia sheria na kuheshimiana.
  3. aisee kuna siku utapasuka humo road kuna watu wanatembelea CC 660 na wana wadhifa fedha na ushawishi kukuzidi, so tulia usijione umo kwenye Jetour au BYD ukahisi unammiliki na kummudu kila mtu humo road; kuna watu unapishana nao wamo kwenye bajaji na nwe umo kwenye kimulimuli lakini wanaweza kuamua hatma yako kwenye eneo unalotamba nalo!
Mwakatapanya Nyadikwa
 
Asubuhi ya leo nimetoka nyumbani Mapinga kuelekea kazini.
enye Jetour au BYD ukahisi unammiliki na kummudu kila mtu humo road; kuna watu unapishana nao wamo kwenye bajaji na nwe umo kwenye kimulimuli lakini wanaweza kuamua hatma yako kwenye eneo unalotamba nalo!
Mwakatapanya Nyadikwa
Kwa umbali mliotoka hata ningekuwa mimi ningepata wasiwasi. Ila huyo jamaa kanishangaza,sasa kama watu wanakufuatilia na wewe ukasimama na kuwafuata si umewarahisishia kazi. Mimi ningetafuta kituo cha mafuta nikazuga naingia nikuache upite nione utanifuata na huko au vipi.
 
Mungu mwema huyo jamaa amekuuliza kimahaba tu nawe ukamshangaa kishkaji ila kwa hali yasasa uyo jamaa angekua na manati ya kizungu angekulipua maana ulimletea ligi isiyo na maana tena mtaa mliotokea ni wakutilia mashaka
 
Mimi naona jamaa alikuwa sahihi kusimama kukuuliza.Haiwezekani wewe ufuate mwendo wake hata kama ningekuwa mimi lazima ningejihami kama sheria inavyonitaka kuchukua hatua ili kujilinda.Ilitakiwa wewe kama unaharaka umpite uendelee zako au umwache aende na siyo kumfuata mwendo wake kuwa aktanua na wewe unatanua na akikimbia na wewe unakimbia.
 
Back
Top Bottom