Sijui ndio tuwaite washamba au limbukeni wa magari?

Sijui ndio tuwaite washamba au limbukeni wa magari?

Asubuhi ya leo nimetoka nyumbani Mapinga kuelekea kazini.

Kama kawaida nikakunjia Boko Magengeni kuelekea njia ya Mbweni JKT ili nikatokee Ununio hadi Kunduchi kuelekea Mwenge kwa njia ya kuingilia Clouds Media.

Nilikuwa na Escudo langu edition ya Singapore, niko kwenye mwendo wangu wa kawaida tu wa 100/km mida ya saa 12 bado wadau hawajawa wengi road!... kama ilivyo kwa watu wengi wanaowahi kazini asubuhi. Kila mmoja ana safari yake!!

Kwa muda nikawa nyuma ya Land Cruiser GX yenye namba EDJ. Jamaa alikuwa kibati sana nami nikawa nafuatana nae si kinyonge tangia tukiwa Mbweni roundabout-Ununio then Kunduchi....

Kwenye ile njia ya chini ya Kunduchi, wenyeji wanaijua vizuri; asubuhi magari mengi yanatanua na yanakuwa kibati cha kutosha....watu wanawahi zao job!

Tulipofika usawa wa Kota za Polisi Kunduchi, jamaa akaruka tuta la ile down, nami nikaruka nyuma yake. Akaruka lile la pili baada ya kumaliza ile down nami nikaruka!.

Ghafla baada ya kuruka tuta akasimamisha chuma lake akaegesha pembeni mbele yangu kiasi cha kunifanya nami nipunguze mwendo na kusimama.

Nikadhani labda amepata hitilafu ya gari ili nikunje zangu kulia nisepe.

Kabla sijaanza kuondoka, akanizuia, akashuka kwenye gari yake na kuja niliposimama.

Nikashusha kioo nikamuuliza, "Kuna shida?"

Akaniambia: "Mbona unanifuatilia?"

Kwa kweli nilibaki nimeshangaa.

Nikamuuliza, tangu lini kuendesha gari nyuma ya gari lingine kwenye barabara ya umma ikawa ni kumfuatilia mtu na ni asubuhi kweupe wala sio maporini?

Hapa kila mmoja anaelekea uelekeo wake!. Why useme nakufuatilia!!

Sio kila gari lililo nyuma yako lina maana linakufuatilia! Kwamba kwa sababu wewe uko na mbio nami na mbio nikiwa nyuma yako ndio nakufuatilia, liko wapi kosa hapo!?


Tukabadilishana maneno kwa muda wa dakika mbili 3 pale!!!

Nikamweleza kuwa sikuwa namfuatilia wala sikuwa na tatizo lolote naye.

Sikuwa nimemgonga, sikuwa nimemkwaruza gari, wala sikuwa nimemzuia kupita. Nini shida yake.

Barabara ni ya wote.

Uwe unaendesha Land Cruiser, Prado, V8, bajaji, honda au Escudo ya miaka ya nyuma, hakuna anayepaswa kujiona anaimiliki njia au kuamua nani aruhusiwe kuwa nyuma yake, mradi kila mtu anazingatia sheria na usalama barabarani.

Mwisho wa siku akarudi kwenye gari yake akionesha dole la kati nami nikajirudishia na kila mmoja akaendelea na safari yake.

Nikajiahidi angeleta za kuleta stori zingekuwa nyingine.

Kwa kweli kuna baadhi ya madereva wanaonekana kuamini kwamba akiwa barabarani na gari la thamani kuwazidi wenzake anaweza akawaamrisha kufanya lolote;

Somo:
  1. Tuwe wastaarabu barabarani.
  2. Barabara ni ya wote, na kila mmoja ana haki ya kuitumia kwa kuzingatia sheria na kuheshimiana.
  3. aisee kuna siku utapasuka humo road kuna watu wanatembelea CC 660 na wana wadhifa fedha na ushawishi kukuzidi, so tulia usijione umo kwenye Jetour au BYD ukahisi unammiliki na kummudu kila mtu humo road; kuna watu unapishana nao wamo kwenye bajaji na nwe umo kwenye kimulimuli lakini wanaweza kuamua hatma yako kwenye eneo unalotamba nalo!
Mwakatapanya Nyadikwa
Mitaa yenyewe Ununio? Jamaa yuko sahihi
 
Mzee acha visingizio 😀😀
Kweli mzee, kwa situation aliyoielezea mtoa mada mimi ndio ningekuwa kwenye position yake huwezi jua nini kingetokea.
Kuna jamaa wiki iliyopita hapo nairobi kapigwa kisu cha tumbo na dereva wa uber kwa ujinga ujinga tu wa barabarani, saizi anaitwa marehemu na dereva kadakwa anaenda kunyea debe chanzo Road Rage
 
Ukiwa safarini na gari yako mtu anaetaka ligi kumjua ni simpo maana atakaka akupite,mt mwenye uelekeo mmoja utamjua maana anaweza kukupita ukimpisha na anaekufuata utamjua maana anaenda kama uendavyo ww na hatak kukupita so ww ulionesha kumfuata angekulima chuma
 
Ukiwa safarini na gari yako mtu anaetaka ligi kumjua ni simpo maana atakaka akupite,mt mwenye uelekeo mmoja utamjua maana anaweza kukupita ukimpisha na anaekufuata utamjua maana anaenda kama uendavyo ww na hatak kukupita so ww ulionesha kumfuata angekulima chuma
Kwa hiyo jamaa angelimwa risasi ya komwe saa hizi angekuwa "rehemu"?Marehemu ni wengi.
 
Tulipofika usawa wa Kota za Polisi Kunduchi, jamaa akaruka tuta la ile down, nami nikaruka nyuma yake. Akaruka lile la pili baada ya kumaliza ile down nami nikaruka!.

Ghafla baada ya kuruka tuta akasimamisha chuma lake akaegesha pembeni mbele yangu kiasi cha kunifanya nami nipunguze mwendo na kusimama.
Hahaha,
Itakuwa jamaa alihisi kayakanyaga kwa kukutana na watekaji live, na ndo sababu alisimama karibu na kituo cha polisi
 
Kwa umbali mliotoka hata ningekuwa mimi ningepata wasiwasi. Ila huyo jamaa kanishangaza,sasa kama watu wanakufuatilia na wewe ukasimama na kuwafuata si umewarahisishia kazi. Mimi ningetafuta kituo cha mafuta nikazuga naingia nikuache upite nione utanifuata na huko au vipi.

Kuna mambo mawili anakwambia ili ujue amejua unamfuatilia ni njia sahihi kama eneo ni la wazi na halina risk. Njia yako pia ni sahihi na salama zaidi
 
Back
Top Bottom