Mnakumbuka Kikombe cha babu wa Loriondo?
Hii ni ushahidi kwamba WaTZ kadri ya 92% wanaamini kwene ushirikina.Haijalishi wanakwenda Kanisani au msikitini bado Wana ushirikina.Hapo Pana msomi Kaenda Kuombewa alinde Kazi yake.Katika waliohudhuria wapo watu wa madhehebu ya kila Aina.Yaani sehemu kubwa ya Maisha ya mwafrika inacheza Kati ya kwenda Kwa waganga na Kwa manabii na Watu wa upako.Hili Siyo geni.Mwisho watu kama Mwamposa na wengineo wanaitwa social entrepreneurs:Wameiona Fursa wakachangamka.Kama Hujui watu Wana shida nyingi hasa za kiakili.Biashara zikiyumba watu wanatafuta ufumbuzi,mtoto akifeli Mtihani Wazazi wanawahi,Mtu asiye na kazi pia anapop Kati ya waganga na manabii.