Siku 100 za Rais Samia Suluhu, Tundu Lissu Amsifia sana, ataka maboresho zaidi ya kimfumo

Siku 100 za Rais Samia Suluhu, Tundu Lissu Amsifia sana, ataka maboresho zaidi ya kimfumo

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Akiwa katik maahijiono ya maswala mbali mbali ya kisaisa, kijamii na uchumi nguli huyo wa sheria na siasa za afrika mashariki amejikita ktk maswala ya
1. Haki
2. Ukweli na usuluhishi
3. Mabadiliko ya katiba
4. Harakati za kisiasa
5. Mageuzi katika uchumi wa Tanzania
6. Maendeleo endelevu.

Tundu Lissu amemsifia Rais Samia Suluhu hasani na kusema kuwa Rais huyo aliyeapishwa baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dr John Joseph Magufuli mnamo tarehe 19 Machi 2021, amesema amelete nafuu na pumzi ya ahueni kwa raia wengi waliokuwa wamechoshwa na uongozi wa kibabe usiozingatia haki na sheria za nchi.

Amesema Rais ameanza vizuri kwa matumaini makubwa ikiwemo kuachia huru sehemu ya wafungwa wa kesi za kubambikiza na za uongo ikiwamo swala la Mashekh wa uamsho na wanasiasa wa upinzani.

Ameongeza kwa kusema Rais anapaswa kuendeleza na kuongeza imani hiyo kuwaachia wafungwa wengi zaidi walioko katika magereza mbalimbali kwa kesi za kisiasa na za kubambikiza.

Licha ya pongezi hizo ametoa wito kwa Rais Samia Suluhu kulitendea haki taifa kwa kuleta mabadiliko ya kimfumo yatakayowezesha kuondoa hitilafu na matendo kama yaliyopita awamu ya tano, mabadiliko hayo yawe pamoja na kuanzishwa Tume ya usuluhishi na ukweli, Tume huru ya uchaguzi, katiba mpya na maboresho ktk sheria kandamizi zisizokuwa na maslahi kwa taifa.

" Hii ni hatua nzuri kwa Rais Mama Samia Suluhu, ameleta matumaini mapya na amani kwa watanzania na mimi mwenyewe"... ilisema sehemu ya hotuba yake .

Tundu Lissu aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais akipeperusha bendera ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, amesema ni wakati sasa Rais Samia kuiachia nchi urithi wa kudumu wenye tija badala ya kufanya mambo madogo madogo kama ujenzi wa mutaro, mifereji, barabara ambazo zinajengwa kila wakati. Katiba Mpya ndio Legasi yake anahitaji kuizingatia na iko ndani ya uwezo wake kuruhusu mchakato kwa amani.

WANANCHI WANASEMAJE?
Wengi wameunga mkono hatua zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu na kutaka atuachie mchakato wa Katiba mpya kuendelea pale ulipoishia kwa Katiba ya Jaji Sinde Warioba.

Ktk hatua nyingine wapenzi wa demokrasia amani na maendeleo nchini wameshangazwa na baadhi ya wanasiasa kuwa vigeugeu na kutaka Katiba Mpya isiwe kipaumbele.

Ikumbukwe ni kundi lule lile la wanasiaaa waliotaka katiba ibadilishwe ili aliyekuwa Rais Hayati Magufuli aongezewe kipindi cha utawala. Hii ina maana kwamba walikuwa wanampenda Magufuli na sasa hawaoni haja ya Katiba kubadilika, pengine walifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi hivyo watanzania tuwapuuze na tuendelee na kudai Katiba Mpya kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.
 
28 June 2021
Nairobi, Kenya



Mahojiano exclusive katika ya Maureen Medza wa kituo cha Mwanzo TV na Makamu Mwenyekiti wa chama cha siasa cha CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu.
Source : mwanzo tv

Asante sana Mr Bagamoyo. Unifundishe na mimi jinsi ya kubandika link youtube
 
Samia sio shetani useme hana mazuri yake, lazima awe nayo, huwezi kumpinga kwa kila atakachoongea utaonekana chizi.
Sahihi kabisa mwanzo ni mzuri ukifatilia tulikotoka.
 
Inapendeza hizo ndio fikra huru Sasa
Kwenye ukakasi unakosoa,penye zuri unapongeza na kuongeza maoni Ili paboreshwe zaidi!

Viva Lissu!✊👊
 
Back
Top Bottom