Siku 21 za maombolezo ya kifo cha Rais Magufuli zafika ukingoni

Siku 21 za maombolezo ya kifo cha Rais Magufuli zafika ukingoni

Ndio hivyo si unajua unafiki wa wabongo? Wanaenda na mdundo tu,kama maombolezo na wao wanaenda hivyo hivyo kimaombolezo yakiisha tu wanaweka KAPUNI.
He he he wabongo wana stress mpaka stress zenyewe zinawakoma[emoji16]
 
Kule kwetu msiba ikitokea ng'ombe, mbuzi na kondoo wanachinjwa na watu wanakula na mboga iliyoenda shule. Pia pombe inakuwepo kwa wingi na nyama za kuchoma.
Kumbe kitaifa Ni tofauti.
 
Mtu yoyote anaecha mazuri na mabaya pia hawez sahaulika kamwe wapo watakao mkumbuka kwa mazuri yake na wapo watakao mkumbuka kwa mabaya yake

RIP JPM nitakukumbuka daima
 
wiki izi mbili kila ukienda ATM kuchukua hela unakutana na fedha mpyaaa mpyaa
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipokuwa makamu wa Rais alitangaza kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli Machi 17, 2021 na kutangaza maombolezo ya siku 21 kwa mujibu wa sheria.

Hayati Rais Magufuli amefanyiwa maombolezo yakiwa ni pamoja na bendera kupepea nusu mlingoti na vyombo vya habari hasa televisheni na vituo vya redio vikipiga nyimbo za maombolezo.

Rais Magufuli alizikwa Machi 26, 2021 wilayani Chato, Mkoani Geita baada ya kuagwa na wananchi wa Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar na Mwanza.

Rais Magufuli aliingia madarakani Mwaka 2015 ambapo alichukua kiti cha urais kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.
 
Unataka yale makoti makubwa?

Mimi naombeni mnipe ile TShirt Jiwe alivaa juu ya jiwe.

images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom