Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Magufuli atakuja kuonekana shujaa na hatutaamini. Watanzania tunapenda sana kulaumu Kwa mtu aliepo madarakani.
Hata kipindi cha Mkapa pia watu walilaumu sana na ndio maana alipaaga Kura nyingi sana. Lakini mwishowe ndio haya tena.
Watanzania tujirekebishe.
 
Na akitoka magu akija mwingine ntakufukua uzi! Watu ni wanafki sana brother, we ngoja tu 2026 sio mbali sana!
Unamaanisha Tanzania itaendelea kupata viongozi wabovu? Kwa mtazamo wangu na hali halisi ilivyo nchini Magu ndio Rais mbovu zaidi kuliko wote waliowahi kuongoza nchi hii
 
unamaanisha Tanzania itaendelea kupata viongozi wabovu?kwa mtazamo wangu na hali halisi ilivyo nchini Magu ndo rais mbovu zaidi kuliko wote waliowahi kuongoza nchi hii
Hata Kikwete mlisema hivyo na ushahidi ni huu uzi nilioufukua! Ni suala la muda tu kuja kusema mmemmiss magu!
 
Hata kikwete mlisema hivyo na ushahidi ni huu uzi nlioufukua! Ni suala la muda tu kuja kusema mmemmiss magu!
Jk alikuwa mbovu ila huyu ni mbovu zaidi, yaani ni sawa na kuruka mkojo then ukakanyaga kinyesi
 
Kweli sijijui ila viongozi wabovu wanajua, korosho shida, Kule Tabora wakulima wa tumbaku wameshindwa kulipa mikopo kisa kaingia huko pia,sasa wewe kumjua kwamba huyu ni mbovu tunahitaji mpaka uwe professor?
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
[emoji4][emoji4][emoji4]
 
Na siku nikisikia jiwe kaachia ngazi nitapendekeza iwe national daynmaana haijawahi nchi hii kuwa na uchumi mbovu wa wananchi wake kama wakati huu. tangu tupate uhuru hatuwaji kuwa na mtu............kama huyu
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Hii thread yako tamu sana
 
Kwa kusema yote haya tunamalizia kwa kusema UHURU WA HABARI MA KUTOA MAONI UNAKANDAMIZWA🤷🏾
 
Mwaka huu vipi umeshafanya au utafanya lini kama bado na utafanyia wapi? Pilau na nini vitakuwepo?
 
Back
Top Bottom