Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

JF ni habari ingine kabisa!!!
Unajua hata hizi ID mpya nyingi nyingi unazoziona ni wenyeji ila imebidi tu wafungue zingine, kukwepa matapishi yao, au wengine wamehamia vyama vingine na hali thread za mwanzo alikuwa kidedea na chama fulani. JF tuwekeeni option ya kufuta thread bwana! hahahahahaahahha
 
Uzuri wa jf ukianzidha Uzi bure kuufuta ndio mbinde, anatamani audelete
Ila anaweza kufanya kama the bold siku hizi anaitwa Habibu A. Hanga alichofanya thread zake amefuta maandishi yake yote zimebakia heading tu. halafu ana andika kabisa dilitedi bai otha
 
Unajua hata hizi ID mpya nyingi nyingi unazoziona ni wenyeji ila imebidi tu wafungue zingine, kukwepa matapishi yao, au wengine wamehamia vyama vingine na hali thread za mwanzo alikuwa kidedea na chama fulani. JF tuwekeeni option ya kufuta thread bwana! hahahahahaahahha
Napinga hoja kwa nguvu zote!! 🙈
Hakuna ku-delete. Ziwepogo tu ili tukumbushane
 
Watu waling'olewa sana kucha kipindi hicho, according to mtoa post
 
Huyu bosi aje aandike uzi mwingine tu ili akili imuende sawa
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Mkuu maoni yako ni nini kuhusu serikali ya sasa
 
Kwakweli jakaya mrisho kikwete aliliyumbisha Sana hili Taifa nakumbuka ndo enzi hizo kila nilipokuwa naingia kwaro na mtu nisiemjua unashangaa naambiwa kijana unanijua kuwa Mimi Ni Nan? Dah yani ulikuwa Ni uongozi wa kupigana biti mwanzo mwisho... Mtu anafanya kila analojisikia katika jamii harfu anasema wewe Ni peleke unapojua..
Ndo hikihiki kipindi ambacho wanafunzi kupigwa Mimba ilikuwa kawaida Yan ndo kipind hichohicho Cha kikwete ambapo ulikuwa unaweza kuingia guest na mwanafunzi akiwa amevaa sare za shule..

Daaah huu ulikuwa uongozi wa ajabu Sana ctaki hata uje kujirudia vizazi vyote..
Umezidisha chumvi
 
natarajia siku moja mtoa post aje akane kauli yake kwani yaliyopo ni heri JK, uchumi ni tete, ajira ni balaa,wasiojulikana usiseme, demokrasia mmmhh chichemi. ukiangalia maisha ya Mtanzania wa leo na yule wa JK kiuchumi ni tofauti sana, kwani tumebugi kwa kweli

Hakuna kitu kama hiko.
Ukweli ulio wazi, Mabaya yanayoendelea sasa yanamfanya JK aonekane malaika na hata wakati wa Mkapa tulilia sana, lakini balaa aliloleta JK, Mkapa akaonekana msafi.
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Haya yote watu wameyasahau na sasa wanatamani arudi tena...
 
Mkuu, mkuu Salary Slip hakika 2015 ungeyajua yajayo usingeandika kabisa. 2016-2019 shamba letu limeingiliwa na viwavi jeshi. Viwavi jeshi wanaweza kuwa sio wengi lakini style yao ya kula huku wanakunya ni hatari sana katika kumaliza shamba
 
Back
Top Bottom