Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Salary slip, unaendeleaje na maadhimisho? Unafanya mwezi gani kila mwaka?
 
1.Siku hiyo itaitwa kumbukumbu ya dikteta muuaji na mcheshi kuliko wote.
2.AU siku serikali ya majambazi ilipoondoka!
3.AU maadhimisho ya miaka kumi ya mateso chini ya Serikali ya wezi
4.AU siku mtandao wa wezi ulipoachia madaraka!!
Kila Rais anaitwa dikteta!
 
Ninaahidi mbele ya mashahidi wa JF kwamba katika maadhimisho yako ya kwanza ( bila shaka itakuwa november hii ) nitakuchangia pesa taslimu 200000 ( laki mbili ) ili kujazia patakapopungua , wakati ukifika njoo PM .
Vipi mchango ulipeleka? Inawezekana ukapinga kwamba you siyo comment yako maana Wana saccos mna tabia za kupinga pinga kila kitu.
 
Vipi mchango ulipeleka? Inawezekana ukapinga kwamba you siyo comment yako maana Wana saccos mna tabia za kupinga pinga kila kitu.
Halafu kwa Utukufu wa Mungu nilichabgia laki 5 badala ya laki 2 nilizoahidi
 
1.Siku hiyo itaitwa kumbukumbu ya dikteta muuaji na mcheshi kuliko wote.
2.AU siku serikali ya majambazi ilipoondoka!
3.AU maadhimisho ya miaka kumi ya mateso chini ya Serikali ya wezi
4.AU siku mtandao wa wezi ulipoachia madaraka!!
Aisee....kumbe hadi JK alikuwa anaitwa dikteta?
 
Tangu nchi hii ipate uhuru, hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi; ni katika awamu hii kashfa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa; pia ni katika awamu hii, operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka; ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi; ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia, ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu. Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia, ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo, bila kujali nani atamrithi JK, nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja, kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
[emoji23][emoji23][emoji23] aisee nimecheka, sherehe unafanya?
 
Ila bro na wewe ni mnafki Sana leo ndio unalialia na kusema umemmiss JK
Mambo yale yalishaisha ndomana hata sahv huyu #1 siwezi ponda maana atakuja mwingine wataona afadhali ya huyu
Bora uwe nutral ila ukosowe sehemu fulani muhimu ....ila ubinadam kazi sana

Ova
 
Back
Top Bottom