Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 21,788
- 34,782
Hii post ikae pale juu bana, mods mbona mnalala?
Mwaka huu wapi?Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.
Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.
Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.
Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.
Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.
Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.
Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!
Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.
Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Ila bro na wewe ni mnafki Sana leo ndio unalialia na kusema umemmiss JK.. Salary Slip itabidi tufanye shereehee kubwa ya kusherekea kutoka kwa jk maana tangu aingie ni shidaaa
Inakuaje Leo mnammiss?naunga mkono hoja
Pumba tupu!!!!Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.
Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.
Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.
Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.
Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.
Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.
Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!
Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.
Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Sasa hivi anasema kammiss JKPumba tupu !!!!
Alichokiandika hata sidhani kama anakielewa !!Sasa hivi anasema kammiss jk
Kauli hii bado upo nayo hadi leo???Mimi nitaridhika tu pale yeye na familia yake watakapofilisiwa mali zao zote walizojipatia kwa kutumia madaraka ya uraisi.
Sasa hivi je??1.Siku hiyo itaitwa kumbukumbu ya dikteta muuaji na mcheshi kuliko wote.
2.AU siku serikali ya majambazi ilipoondoka!
3.AU maadhimisho ya miaka kumi ya mateso chini ya Serikali ya wezi
4.AU siku mtandao wa wezi ulipoachia madaraka!!
Mwaka huu inafanyika beach kidimbwiMleta mada vipi maadhimisho yako yanaendeleaje
We toka lini mtu akajiita salary slip akawa na akili sawa sawa? Haya sasa huu uzi akiuona atabadili macho ka kinyongaHaya yote watu wameyasahau na sasa wanatamani arudi tena...
Sasa hivi wamemmissWapinzani walimuonea sana jk..
Mimi pia nishamuomba radhi maana kwenye uzi huu nili cmnt pia....na kingine siwezi kumsema namba 1 aliyepo sasa maana hata akimaliza muda wake yatakuja yale yale watu watakuja kumuona afadhali ya sasaMleta maada unapaswa kwenda Msoga kuomba radhi