Siku ambayo Kikwete anaondoka madarakani nitaiadhimisha kila mwaka

Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Maandishi huwa hayaozi!!
 
hahahahahaha bila kujali atakayemrithi....hahahaha bavicha chaliiii kifo cha mende
Wote ni wale wale.Huyo JK ndie alieweka msingi wa baadhi ya mambo tunayoyaona leo hii.

Ni katika utawala wa JK tumeona watu wakitekwa kama kina Dr.Ulimboka.

Ni katika utawala wa JK ndio imetungwa sheria ya mitandao.

Huyu JPM ana-take advantage ya mazingira yaliyoachwa na JK.
 
Mtoa mada siku hizi we mpumbavu sana ,
 
Wakubwa msifukue vikaburi vyao hawa jamaa maana huwa vinanuka sana. Cheki paragraph ya pili kutoka chini, Eti bila kujali atakayemrithi...
Acheni kujifariji.

JK ndio kaweka msingi wa haya yote tunayoyashuhudia leo.

Angefanikisha Katiba mpya hata huu udhalimu usingekuwepo.

Wote ni wale wale ila kwa viwango tofauti.
 
Mbona ufipa mnamshangilia? Mnasema bora ya jana?
 
Wote ni wale wale.Huyo JK ndie alieweka msingi wa baadhi ya mambo tunayoyaona leo hii.

Ni katika utawala wa JK tumeona watu wakitekwa kama kina Dr.Ulimboka.

Ni katika utawala wa JK ndio imetungwa sheria ya mitandao.

Huyu JPM ana-take advantage ya mazingira yaliyoachwa na JK.
Mkuu leo utasema mengi!! Angalia wenzio wasije wakakutenga kama kipindi Fulani
 
Tangu nchi hii ipate uhuru,hakuna awamu ambayo taifa limepata hasara kubwa na ya kutisha kutokana na wizi na ufisadi wa kiwango cha juu kama awamu hii ya Kikwete.

Ni katika awamu hii wanyama wamepandishwa ndege na kuuzwa nje ya nchi;ni katika awamu hii kashifa za wizi wa mabilioni ya fedha za umma zimetokea na wezi kulindwa;pia,ni katika awamu hii,operation za kinyama kama "tokomeza" zimetendeka;ni katika utawala huu watu wameng'olewa kucha na meno bila ganzi na kisha kutupwa wakiwa mahututi;ni katika awamu hii ambapo wezi wa mabilioni ya umma wamesamehewa na ni katika awamu hii pia,ndugu zetu albino wameuwawa kinyama huku serikali ikishindwa kuwalinda.

Jambo lingine baya kabisa ni unyama wa Jeshi la polisi katika kudhibiti wapinzani na hata kutuhumiwa kuua raia kwa risasi na mabomu.Tuhuma za mabomu ya Arusha na kwingineko kila mtu amezisika.

Mfano mbaya kuliko wote ni mauaji ya Daudi Mwangosi ambayo polisi wanatuhumiwa kuyatekeleza na kwa mshangao wa wengi, RPC mtuhumiwa akapandishwa cheo.

Vile vile bila kusahau mgomo wa madaktari na jinsi serikali hii ilivyoumaliza bila kusahau madhara ya mgomo huo kwa wagonjwa wasio na hatia.

Pia,ni katika awamu hii maoni ya wananchi katika kupata katiba mpya yametupwa bila huruma.

Haya yote yametokea katika awamu hii ya JK ambapo watuhumiwa wengi bado wanapeta uraiani!!

Kwasababu hizo,bila kujali nani amtamrithi JK,nina kila sababu ya kusheherekea kuondoka madarakani kwa Kikwete na ni imani yangu nchi itaapumua.

Hiyo siku kila mwaka kama ni kuchinja mbuzi nitachinja,kama ni vinywaji, basi idadi na variety kwa siku hiyo itaongezeka na pia nitawaombea dua wale wote walioathirika kwa namna moja au nyingine na utawala huu.
Shikamoo Kamanda mshahara kwa Uzi murua kabisa
 
Pamoja na matusi yako mengi,je hayo niliyoyasema hayajatendeka chini ya awamu hii ya JK?

Je,haya ndio maisha bora aliotuahidi mwaka 2005?

Matusi hayajibu hoja bali yanakudhalilisha wewe mwenyewe tu.
Kamanda Mshahara unatisha kwa hoja
 
Back
Top Bottom