Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari Waheshimiwa!
Najua kuna watu hamjawahi kuitwa Waheshimiwa, ngoja niwatoe lock na ninyi muonjeonje kidogo majina ya heshima. Mimi mara ya kwanza kuitwa Mheshimiwa ni siku nimeenda kutoa posa huko madongo kuinama, niliazima VX ya kijivu, nikaiweka bendera ya Tanzania upande wa mbele, kisha nikatimba Ukweni. Kila mara nilikuwa nikiwakatisha na kuwakataza wasiniite Mheshimiwa, halafu walikuwa wakikosea, walikuwa wakiniita "Mesimiwa", hatari sana. Tuachane na hayo, ilikuwa nje ya mada. Sisi wengine tunapenda stori.
Hivi uliwahi kujiuliza siku mtoto wako akikua, akaingia mitandaoni halafu akasoma posts na comments zako atajisikiaje? Je, atafurahi au atahuzunika? Je, atajivunia baba au mama bora au atajiona ana bahati mbaya kuwa na baba au mama mjinga kama wewe?
Je, utamkatisha tamaa na kumkwaza au utampa moyo?
Mfano, akute ukiwaponda wanawake wasio na shape halafu yeye muda huo mwili wake haueleweki kiuno kiwapi, tumbo li wapi, yaani ni amorphous fulani hivi. Au ulikuwa unaponda wanawake au wanaume wafupi kama mtungi wa gesi, halafu mtoto wako ndio yuko hivyo. Je, atafarijika au atakata tamaa?
Ndugu Mesimiwa, kwa ridhaa yako naomba nihitimishe kwa kusema, ujumbe wowote utakaoutoa basi angalia na kizazi chako ili usijekuwa baba au mama jinga.
Achana na kauli ya kujifariji kuwa hakuna baba au mama jinga. Hizo ni lugha za kujifariji tu, lakini watoto wanajua hapa wana mzazi au hawana.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.