barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,880
Askofu wa kwanza Jimbo Katoliki la Iringao(Kwa maana ya Muafrika) alitokea Kalenga,Ukoo wa Mgulunde ambaye alikuwa moja ya wanandugu wa Chief Mkwawa,Aliitwa Mario Abdalah Mgulunde...huyu ndie Askofu wa kwanza mkatoliki mweusi wa Iringa baada ya Francesco Caligliero(tamka Caliero) ambaye alikuwa Padre mlezi wa jimbo kabla ya kuja Askofu Attilio Betlamino aliyekuwa mtaliano.
Askofu Mario Abdalah Mgulunde alitoka ktk familia ya Kiislamu na alikulia ktk uislam mpaka pale Wamisionary wa shirika la Consolata walioingia Iringa mwaka 1897 walipomchukua na kumpeleka shule za mission na kumbatiza.Wahehe Waislam wanapatikana Kalenga ktk mkoa wa Iringa,japo kiukweli wapo wachache,na wengine wapo eneo la Pawaga Itunundu.Uislam Kalenga uliletwa na Waarabu waliokuwa wanafanya biashara na Mkwawa,na kwa sbb Wazungu walikuwa "waonezi" na wauwaji,Mtwa Mkwavinyika Mkwawa akaamua kujiunga na Muarabu na akafuata dini hiyo na watu wake akawaamuru kufuata dini hiyo.
Wamisionary walikuja baadae sana,wakaja kuomba ardhi kwa Mkwawa,sbb Mkwawa alikuwa hataki wakae pale akawapa mlima wenye mawe sana ambao alijua kwa ukubwa wa mawe yale Wamisionari Wabenedictin toka Ujerumani watakata tamaa na kuondoka.Wajerumani wakapokea eneo na kuanza kucharanga mawe na kuyatupa pembeni,ndio maana eneo hilo Wahehe wakaliita "Tosa-Maganga" maanake "Tupa Mawe".Walijenga majengo juu ya miamba ya mawe,mpaka leo ukienda unayakuta.Hapo sasa ndio Ukristo ukaanza kuenea eneo la Iringa.Hivyo Ukristo Ukatoliki uliukuta Uislam umeshaenezwa eneo la Uhehe