View attachment 331564
Mkuu
BansenBurner na
lusungo hii picha sasa ndio inathibitisha kuwa umisionari huko Iringa ulikuja baadae sana baada ya Uislamu kutamalaki.
Picha hii ni Parokia ya Tosamaganga yenye historia kama nilivyoeleza hapo juu,na nyumba hiyo nyeupe ndio ilikuwa ya mwanzo iliyojengwa kwa ajili ya Mafrateli Wazalendo(yaani weusi,Frateli ni kijana anayelelewa kuja kuwa Padre) na ilijingwa miaka ya mwanzo ya 1900 mpaka sasa ipo.Kushoto kwake ni Kanisa Kuu la Tosamaganga ambalo ndio yalikuwa makao makuu ya Jimbo la Iringa kabla ya kuhamishiwa Kihesa Iringa Mjini.
Huo mnara pembeni ulijengwa mwaka 1997 kwa ajili ya kumbukumbu ya Mapadre Wazungu na Waswahili(Wazalendo) tokea kazi ya umisionari ianze jimboni Iringa.Mpaka sasa Tosamaganga ni kati ya Parokia chache za Jimbo la Iringa zinazoendelea kukaliwa na Wamisionari wa Consolata wa kutoka Italia,parokia nyingine zinaendelea kuongozwa na mapadre waafrika wa Jimbo hilo.Hivyo Mzee
Mohamed Said yupo sahihi katika uchambuzi wake,mimi kama mkristo mkatoliki ninakubaliana na uchambuzi wake kuhusu eneo hili.
Namuomba na
FaizaFoxy maeneo ya kukubaliana na ukweli awe anakubali kama wenzake