Mkuu
Ngongo kuna kitu hapa kinataka kisiwekwe sawa,Nimemsoma vizuri Mzee wangu
Mohamed Said lkn kuna mahali kama anaparuka kupasema:
-Kwanza hapa tujue kuwa Mtwa Mkwawa mwenyewe hakuwa na dini kwa maana ya Muislam au mkristo
Yeye alikuwa mfuasi wa dini ya asili akiamini ktk mizimu na waganga wa kienyeji,baada ya kuwa ameli-
ga jeshi la Mjeruma Mtwa Mkwawa alikimbia na akawa anatafutwa sana na Wajeruma popote alipo.
-Baada ya Wajerumani kumkosa wakaamua kumteka mwanae Mtwa Mkwawa aliykuwa anaitwa Sapi Mkwawa
Wakamchukua na kumpeleka Kilwa,kumbuka Kilwa ndio ilikuwa "Escape area" ya Wajeruman wakati wote
Wa utawala wao.Hata Zelewisky anavyokwenda kupigana na Mkwawa alitokea Kilwa kupitia Usagala
Sapi alipelekwa Kilwa ili kumtumia ujumbe Mkwawa kuwa mtoto wake ametekwa hivyo ajitokeze.Baada ya
Kukaa na Sapi Wajeruman wakampenda kwa aina ya uwezo wake wa kuongoza,wakampeleka Ujerumani na
Baadae wakamfanya kuwa Liwali wa Kilwa,na ili awe Liwali ilibidi aendane na utamaduni wa watu wake,hivyo Sapi akaingia kwenye Uislam na akawa Liwali wa Kilwa.
Kuanzia hapo Sapi na kizazi chake cha kuja chini wakawa Waislam,hivyo hata mwanae Adam Sapi Mkwawa alipozaliwa akawa tu "by default" Muislam.Baada ya hapo wale walio ktk ukoo wa Chief kuanzia Sapi na Adam Sapi wakawa Waislam.Hata baada ya Waingereza kurudisha utawala wa machief,Adam na wasaidizi wakke baadhi walioitwa "Wanzagila" walikuwa waislam
Hivyo sehemu ndogo tu ya Wahehe wa kizazi cha Sapi na mwanae Adam ndio walikuwa Waislam,hata wasaidizi wengine na watu wa karibu na Mkwawa kama kina Mwamgongolwa hawakuwa Waislam na Msikiti Kalenga umekuja kujengwa na Chief Adam Sapi miaka ya 1950's
Muingiliano kati ya Wahehe na Waarabu ilikuwa ni sbb ya biashara,Mtwa Mkwawa alikuwa na "shamba lake la pembe za ndovu" ambazo aliwauzia Waarabu,eneo hilo la "shamba" ndio mbuga ya Ruaha National Park ya sasa(Utakumbuka ndio mbuga yenye tembo wengi kuliko zote)
Walichoinga wahehe kwa Waarabu ni vazi,lkn Muhehe hakutaka liwe kama kanzu,yeye aliita "mgolole" na kichwani alijivika kiremba huku chini akivaa "lubega" nyeupa,hili ndio vazi rasmi la Wahehe mpaka leo
Kumbukumbu za Maandishi ya Kiarabu ya Makumbusho ya Mkwawa,ni yale aliokuwa nayo Sapi wakati akiwa Liwali kule Kilwa,akiwasiliana na wafanyabiashara wa kirabu kwa niaba ya Wajerumani,na Adam ndio aliyejengea kaburi la baba yake Sapi kwa mtindo wa kiislam baada ya kurudi toka Makerere na kukabidhiwa Uchief
Wahehe waliupokea Ukristo Ukatoliki toka kwa Wamisionari,na hasa Wamisionari wa Consolata toka Italia mwaka 1896 eneo la Tosamaganga,baadae Wamisionari hao wakasambaa eneo la Madibira bonde la Ihefu,Rujewa eneo la Usangu,Nyabula,Ilole na Pawaga.Toka mwaka 1896 Vatican ilituma Padre Francesco Caligliero(Mwenye jina la shule ya Cagliero iliyopo Ipogoro Iringa) kueneza Ukristo na kuifanya Iringa kama sehemu ya Metroponia ya Nyanda za Juu za Tanganyika,baadae ilipokomaa ndipo Papa akateua Askofu toka Italy kuja kuwa askofu wa Iringa,huyu Mzungu aliitwa Attilio Betlamino na alifia Tosamaganga na kuzikwa ndani ya kanisa hilo.
Cc
barafu UncleBen Ngongo Nyani Ngabu Mimi Mwanakijiji
Tangawizi Yericko Nyerere naiman64