Siku gani katika juma watu huamini ni siku yenye mikosi au nuksi?

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,621
Hapo vipi!

Nimeshakutana na watu wenye kuamini baadhi ya siku kwenye juma zina mikosi, hivyo hufunga hata kazi zao.

Je, hizi siku zipo na je kuna ukweli?
 
Nimesiki na nimeona kwa watu, Jumanne.

Tena wenye biashara na wana imani hiyo siku yao ya kupumzika uwa ni Jumanne.
We sio mtu wa kwanza kusema hvyo,hata boss wangu anaamini j4 Ni siku ya mikosi,hii hupelekea hata ukifanya kosa kubwa ofisini akikumbuka kosa umelitenda siku ya jumanne anakusamehe akiamini Ni siku ya mkosi
 
Jumanne, sababu kubwa ya siku hii kuwa mbaya ni kutawaliwa na nyota ya Mirihi ambayo ni moto. Ni siku inayotumika kufanya mambo mabaya hasa ya kishirikina na muda wake m'baya zaidi ni saa moja asubuhi na nane mchana.

walozi hutumia siku hii kutumia watu majini na uchawi kufarakanisha watu, kuwapa watu maradhi, kuwasababishia ajali, ufukara wa maisha nk.

Na bado jumamosi nayo pia hutumika kama siku mbadala kulingana na habari zake.

Yote haya yanabaki kuwa imani ya wenye kuamini kama ilivyo dunia kila mtu na yake.
 
Hapo vipi!

Nimeshakutana na watu wenye kuamini baadhi ya siku kwenye juma zina mikosi, hivyo hufunga hata kazi zao.

Je, hizi siku zipo na je kuna ukweli?
Ijumaa ni siku moja mbaya sana. We fika Kariakoo siku ya Ijumaa, utaona wafanyabiashara wengi wanafunga maduka na kutoa sadaka ya damu kwa misukule yao huku wakichoma udi na ubani kabla ya kwenda misikitini kushukuru.
 
Kuna siri kubwa sana katika siku..
 
Jumanne, sababu kubwa ya siku hii kuwa mbaya ni kutawaliwa na nyota ya Mirihi ambayo ni moto. Ni siku inayotumika kufanya mambo mabaya hasa ya kishirikina na muda wake m'baya zaidi ni saa moja asubuhi na nane mchana.

walozi hutumia siku hii kutumia watu majini na uchawi kufarakanisha watu, kuwapa watu maradhi, kuwasababishia ajali, ufukara wa maisha nk.

Na bado jumamosi nayo pia hutumika kama siku mbadala kulingana na habari zake.

Yote haya yanabaki kuwa imani ya wenye kuamini kama ilivyo dunia kila mtu na yake.

Ni Siku ya huyu jamaa [emoji889]
 
Tangu tunakua miaka ile tuliaminishwa siku ya jumanne ni siku ya mikosi na nuksi. Na kweli siku hiyo hatukuruhusiwa kusafiri.

Kwangu binafsi nikipitiaga matukio mabaya hasa ajali karibu zote nimewahi pata siku ya jumanne. Huwa naiangalia hii siku kwa umakini mno.
 
Back
Top Bottom