Siku gani katika juma watu huamini ni siku yenye mikosi au nuksi?

Siku gani katika juma watu huamini ni siku yenye mikosi au nuksi?

Jumanne, sababu kubwa ya siku hii kuwa mbaya ni kutawaliwa na nyota ya Mirihi ambayo ni moto. Ni siku inayotumika kufanya mambo mabaya hasa ya kishirikina na muda wake m'baya zaidi ni saa moja asubuhi na nane mchana.

walozi hutumia siku hii kutumia watu majini na uchawi kufarakanisha watu, kuwapa watu maradhi, kuwasababishia ajali, ufukara wa maisha nk.

Na bado jumamosi nayo pia hutumika kama siku mbadala kulingana na habari zake.

Yote haya yanabaki kuwa imani ya wenye kuamini kama ilivyo dunia kila mtu na yake.
na vipi kiongozi kwa mtu ambaye mwenye nyota ya punda (hamal) ambao kawakib (sayari) yao ni hiyo mirikh na siku yao huwa jumanne ,je na wao siku hii huwa na mkosi kwao?
 
Jumanne ni siku ya ovyo mno niliigundua tangu nipo shule
 
na vipi kiongozi kwa mtu ambaye mwenye nyota ya punda (hamal) ambao kawakib (sayari) yao ni hiyo mirikh na siku yao huwa jumanne ,je na wao siku hii huwa na mkosi kwao?
Hapana, hawa ndiyo siku yao kubwa hivyo ukiwaroga kwa siku hiyo nguvu yao ya utawala inawasaidia.
 
Sasa kuna wengne tulizaliwa siku ya jumanne. Au ndo mana mikosi haituishi. Kuna kitu mnataka mniaminishe hapo🤔🤔
 
Siku zote ni Allah hakuna mbaya ila mipango yako tu basi.
 
Ijumaa ni siku moja mbaya sana. We fika Kariakoo siku ya Ijumaa, utaona wafanyabiashara wengi wanafunga maduka na kutoa sadaka ya damu kwa misukule yao huku wakichoma udi na ubani kabla ya kwenda misikitini kushukuru.
Wewe, lengo nimelijua ila kazana utalipwa ujira wako.
 
Asiyetaka kufuata njia ya M/Mungu basi atafata ya Ibliis 'alayhi la'na!

Na moto unawasubiri!
 
Jumanne aisee

Mabalaa mengi unikuta siku hyo


Na nimezaliwa siku hyo
 
Tangu tunakua miaka ile tuliaminishwa siku ya jumanne ni siku ya mikosi na nuksi. Na kweli siku hiyo hatukuruhusiwa kusafiri.

Kwangu binafsi nikipitiaga matukio mabaya hasa ajali karibu zote nimewahi pata siku ya jumanne. Huwa naiangalia hii siku kwa umakini mno.
Ungesema yangu unakuwa, wengine hatuzijui siku Mbaya Wala nzuri. All day are equal and good

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom