Siku gani ulichacha hutaisahau?

Ikawaje sasa?
 
Shida hazifanani lakini 2015 aisee siwezi kuisahau until God sent his angel in human form kuokoa jahazi...yaani kila mtu anakukosoa wakati we una hali ngumu...unashikwa na hasira kisha unasema unazificha hasira usije ukakosa na ugali wa shikamoo bure

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Kuna mifulio inakujaga na miujiza

Wangu mmoja sitausahau nilikuwa chuo nadaiwa semester mbili mfululizo ....na wakati huo sina hata msosi .......lahaula mtu mmoja akakosea kutuma milioni na laki 2 ikaingia kwangu ......

kama mnaniona nilivyohaha kuitoa ....niliitoa nikalipia karo ilikuwa jmosi na jtatu ilikuwa tunaanza mitihani ya mwisho

Mwenye nayo kashtuka kesho yake ......nilitupa na laini
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora yako wew iyo ili Baki ila mim Hali ya Leo sio nzur kwakwel Nina Mia mbili tu mfukon ya gome
 
Haya maisha ukiona mtu ana kitu ana ringa muache tu..
Kuna siku nimegombana na baba mtoto
Akasusa akaondoka kama wiki
Hapo ni mjamzito

Sasa akiba ikawa imeniishia sina unga sina chumvi wala sukari,
Nikamtafuta shoga yangu tuliyekuwa tuna mtindo wa kukopeshana akaniambia mpaka saa saba atakuwa ameshanitumia 10,000
Moyo ukatawanyika na tabasamu likarejea
Nilikaa kwenye saa mpaka saa 12 jioni
Nikapiga simu yake mpaka sasa mwaka wa tano huwa hapokei simu.

Kama unapita hapa rafiki yangu T nilishasamehe usiogope kupokea simu yangu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh unadhulumu bila kupenda, shida mbaya sana
 
Story inasisimua hii
 
Ha haaa dah..Nimesoma hii comment nimecheka sana aisee..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh kizinga cha 10,000/- kimevunja urafiki
 
Mwaka 2009.ulikuwa Mwaka mbaya sana. Hata hela ya kula nilikuwa nakosa. Kulala na njaa siku tatu ilikuwa ni kawaida. Na kuomba nilikuwa siwezi. Njaa isikie kwa mwenzio. Nilipigika aswaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu hicho ni kipindi cha mkwere pesa nje nje sasa...babaake ukichacha hii awamu mpaka uibuke si leo!

I wish kipindi cha mkwere ningekuwa kwenye system mashule tupa kule[emoji134][emoji134]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…