Siku gani ulichacha hutaisahau?

Siku gani ulichacha hutaisahau?

Mwaka jana kuna siku nimeamka asubuhi sina kitu ,wife anaumwa ,mtoto anatakiwa kula ,ndani kuna unga,maharage Ila sina hela ya mkaa. Jirani muuza mkaa ananidai buku 7 ma siwezi kwenda kukopa tena. Nilidata kabisa,sina vocha kwenye sim na hata ningekua nayo bado sikua na mtu ambaye angeniazima hata buku.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ikawaje sasa?
 
Shida hazifanani lakini 2015 aisee siwezi kuisahau until God sent his angel in human form kuokoa jahazi...yaani kila mtu anakukosoa wakati we una hali ngumu...unashikwa na hasira kisha unasema unazificha hasira usije ukakosa na ugali wa shikamoo bure

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Kuna mifulio inakujaga na miujiza

Wangu mmoja sitausahau nilikuwa chuo nadaiwa semester mbili mfululizo ....na wakati huo sina hata msosi .......lahaula mtu mmoja akakosea kutuma milioni na laki 2 ikaingia kwangu ......

kama mnaniona nilivyohaha kuitoa ....niliitoa nikalipia karo ilikuwa jmosi na jtatu ilikuwa tunaanza mitihani ya mwisho

Mwenye nayo kashtuka kesho yake ......nilitupa na laini
Ilikuwa tarehe 30 mwezi wa 8. Mwaka 1999. Niliamka asbh sina hata 100. Na wakati huo mke wangu alikuwa amelazwa kwenye zahanati ya mtu binafsi tangu tarehe 28. Usiku akiwa na uchungu wa kujifungua mtoto. Siku hiyo ya tar. 30. Alfajir mama yangu akaja kwangu nikiwa ndo najiandaa kwenda pale dispensary. Mama(R.I.P)akanisalimia Kwa tabasamu na kunipa habari njema kuwa mke wangu kajifungua mtoto Salama mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 3 na gram 200.

Nilifurahi lkn mfukoni hakuna pesa na pale dispensary inatakiwa pesa ili mke wangu atoke. Nikatoka na baiskeli yangu,nikaenda kwa jamaa mmoja nikakopa elf 9,nikaacha baiskeli yangu bond. Nikaenda hospital,nikalipa deni lilikuwa elf 4,nikalipa cash. Nikaenda barabarani nikachukua taxi nikalipa elf 1. Ikawapeleka nyumbani.

Pesa iliyobaki nikaenda kununua poda,mafuta ya nazi,sabuni na vitu vingine vidogo vidogo. Mfukoni nikabaki na shilingi 400. Nikapeleka hivyo vitu nyumbani kisha nikarudi barabarani. Nikaenda sehemu moja huwa wanachezesha kamari ya ile korokoro ile ya kete 3 nikiwa na rafiki yangu(R.I.P). Tukaanza kucheza kidogokidogo,baadae akaja jamaa naye akawa anacheza pale..yule jamaa akawa anahamisha zile hela zetu ndogo yy anazipiga nyumba moja. Kumbe yule jamaa alikuwa mfanyabiashara wa mkaa. Pale kijijini kwetu alikuwa anasubiri gari ya kwenda porini akanunue mkaa.

Aisee yule mchezeshaji nilikuwa nafahamiana naye sana!(R.I.P) baada ya kugundua yule jamaa ana hela,akabadilishiwa kete,zikawekwa za kutoka upande mmoja tu jembe na karanga. Na jamaa,akanitonya,nikaanza kutakaka..namuwekea karanga na jembe yy anahamisha anaweka king au Nanga. Aisee Kwa nusu saa tu nilikuwa na zaidi ya laki na 30 mkononi..! Nilivyoona,hela zimejaa nikaondoka na yule rafiki yangu. Kwanza nilienda dukani kununua vitu vya mtoto vikali,na pamba za nguvu za mke wangu. Kisha nikaenda kuchukua baiskeli yangu..nikanunua kuku ndo nikarudi nyumbani. Hata mke wangu hakuamini maana alikuwa anajua hali yangu. Huyo mwanangu mwaka huu anatizimiza miaka 21. Hii kumbukumbu sitakuja kuisahau aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilichacha siwezi kuisahau maishani. Nilibakiwa na 10,000/- mfukoni. Sasa nilikuwa najisikia vibaya nikaenda kupima malaria nikawa ninayo. Nikawa njia panda, ninunue dawa au chakula maanake huwezi kunywa dawa bila kula ikabidi ninunue msosi tu nikala nikalala na malaria yangu. Kesho nikapiga mishe nikapata hela ya dawa na chakula
Bora yako wew iyo ili Baki ila mim Hali ya Leo sio nzur kwakwel Nina Mia mbili tu mfukon ya gome
 
Haya maisha ukiona mtu ana kitu ana ringa muache tu..
Kuna siku nimegombana na baba mtoto
Akasusa akaondoka kama wiki
Hapo ni mjamzito

Sasa akiba ikawa imeniishia sina unga sina chumvi wala sukari,
Nikamtafuta shoga yangu tuliyekuwa tuna mtindo wa kukopeshana akaniambia mpaka saa saba atakuwa ameshanitumia 10,000
Moyo ukatawanyika na tabasamu likarejea
Nilikaa kwenye saa mpaka saa 12 jioni
Nikapiga simu yake mpaka sasa mwaka wa tano huwa hapokei simu.

Kama unapita hapa rafiki yangu T nilishasamehe usiogope kupokea simu yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mifulio inakujaga na miujiza

Wangu mmoja sitausahau nilikuwa chuo nadaiwa semester mbili mfululizo ....na wakati huo sina hata msosi .......lahaula mtu mmoja akakosea kutuma milioni na laki 2 ikaingia kwangu ......

kama mnaniona nilivyohaha kuitoa ....niliitoa nikalipia karo ilikuwa jmosi na jtatu ilikuwa tunaanza mitihani ya mwisho

Mwenye nayo kashtuka kesho yake ......nilitupa na laini

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh unadhulumu bila kupenda, shida mbaya sana
 
Ilikuwa tarehe 30 mwezi wa 8. Mwaka 1999. Niliamka asbh sina hata 100. Na wakati huo mke wangu alikuwa amelazwa kwenye zahanati ya mtu binafsi tangu tarehe 28. Usiku akiwa na uchungu wa kujifungua mtoto. Siku hiyo ya tar. 30. Alfajir mama yangu akaja kwangu nikiwa ndo najiandaa kwenda pale dispensary. Mama(R.I.P)akanisalimia Kwa tabasamu na kunipa habari njema kuwa mke wangu kajifungua mtoto Salama mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 3 na gram 200.

Nilifurahi lkn mfukoni hakuna pesa na pale dispensary inatakiwa pesa ili mke wangu atoke. Nikatoka na baiskeli yangu,nikaenda kwa jamaa mmoja nikakopa elf 9,nikaacha baiskeli yangu bond. Nikaenda hospital,nikalipa deni lilikuwa elf 4,nikalipa cash. Nikaenda barabarani nikachukua taxi nikalipa elf 1. Ikawapeleka nyumbani.

Pesa iliyobaki nikaenda kununua poda,mafuta ya nazi,sabuni na vitu vingine vidogo vidogo. Mfukoni nikabaki na shilingi 400. Nikapeleka hivyo vitu nyumbani kisha nikarudi barabarani. Nikaenda sehemu moja huwa wanachezesha kamari ya ile korokoro ile ya kete 3 nikiwa na rafiki yangu(R.I.P). Tukaanza kucheza kidogokidogo,baadae akaja jamaa naye akawa anacheza pale..yule jamaa akawa anahamisha zile hela zetu ndogo yy anazipiga nyumba moja. Kumbe yule jamaa alikuwa mfanyabiashara wa mkaa. Pale kijijini kwetu alikuwa anasubiri gari ya kwenda porini akanunue mkaa.

Aisee yule mchezeshaji nilikuwa nafahamiana naye sana!(R.I.P) baada ya kugundua yule jamaa ana hela,akabadilishiwa kete,zikawekwa za kutoka upande mmoja tu jembe na karanga. Na jamaa,akanitonya,nikaanza kutakaka..namuwekea karanga na jembe yy anahamisha anaweka king au Nanga. Aisee Kwa nusu saa tu nilikuwa na zaidi ya laki na 30 mkononi..! Nilivyoona,hela zimejaa nikaondoka na yule rafiki yangu. Kwanza nilienda dukani kununua vitu vya mtoto vikali,na pamba za nguvu za mke wangu. Kisha nikaenda kuchukua baiskeli yangu..nikanunua kuku ndo nikarudi nyumbani. Hata mke wangu hakuamini maana alikuwa anajua hali yangu. Huyo mwanangu mwaka huu anatizimiza miaka 21. Hii kumbukumbu sitakuja kuisahau aisee...

Sent using Jamii Forums mobile app
Story inasisimua hii
 
Haya maisha ukiona mtu ana kitu ana ringa muache tu..
Kuna siku nimegombana na baba mtoto
Akasusa akaondoka kama wiki
Hapo ni mjamzito

Sasa akiba ikawa imeniishia sina unga sina chumvi wala sukari,
Nikamtafuta shoga yangu tuliyekuwa tuna mtindo wa kukopeshana akaniambia mpaka saa saba atakuwa ameshanitumia 10,000
Moyo ukatawanyika na tabasamu likarejea
Nilikaa kwenye saa mpaka saa 12 jioni
Nikapiga simu yake mpaka sasa mwaka wa tano huwa hapokei simu.

Kama unapita hapa rafiki yangu T nilishasamehe usiogope kupokea simu yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha haaa dah..Nimesoma hii comment nimecheka sana aisee..!!

Duh kizinga cha 10,000/- kimevunja urafiki
 
Mwaka 2009.ulikuwa Mwaka mbaya sana. Hata hela ya kula nilikuwa nakosa. Kulala na njaa siku tatu ilikuwa ni kawaida. Na kuomba nilikuwa siwezi. Njaa isikie kwa mwenzio. Nilipigika aswaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu hicho ni kipindi cha mkwere pesa nje nje sasa...babaake ukichacha hii awamu mpaka uibuke si leo!

I wish kipindi cha mkwere ningekuwa kwenye system mashule tupa kule[emoji134][emoji134]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom