Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Mara tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi hii, Rais Magufuli alivipiga marufuku vyama vya upinzani nchini kutofanya mikutano ya kisiasa hadi mwaka 2020, kwa madai kuwa uchaguzi umekwisha, kwa hiyo huo ni wakati wa kufanya kazi na siyo wakati wa kampeni.
Wakati akitangaza hivyo Rais Magufuli, alijua wazi kuwa anaisigina Katiba ya Jamhuri wa Muungano ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) ambayo inatamka wazi kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakuwa nchi ya kidemokrasia na yenye kufuata mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu.
Jambo la ajabu ni kuwa Jeshi la Polisi nchini liliichukulia tamko hilo kuwa ni sheria na kuanza kuwakamata viongozi wote waliokuwa wameamua kukiuka kauli hiyo ya Rais, na kuwafungulia mashitaka ya kuleta uchochezi, ambayo ilikuwa ni uvunjaji wa dhahiri wa Katiba yetu ya nchi, kwani Jeshi hilo linajua wazi kuwa vyama hivyo vipo kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kufanya mikutano ya kisiasa ni moja ya wajibu wao mkuu.
Wakati hayo yakifanyika kwa vyama vya upinzani wenyewe CCM, akiwemo yeye mwenyewe Rais, Katibu Mkuu wa Chama hicho. Dkt Bashiru Ally na Katibu Mwenezi wa Chama hicho, Humphrey Polepole, walizunguka nchi nzima wakifanya mikutano ya hadhara na ya ndani, wakifanya kampeni, bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.
Hata hivyo kama nilivyoeleza kwenye kichwa changu cha habari, kuwa mwaka 2020 ndiyo ushafika, kwa hiyo ni wito wangu kwa vyama vya upinzani kutumia fursa hii adimu, kwa kufanya mikutano ya kisiasa, ambayo itaratibiwa kisayansi zaidi, ili hatimaye ifikapo mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2020, wananchi tukafanye maamuzi kwenye sanduku la kura kwa kuking'oa chama hiki cha CCM ambacho kimedumu kukaa madarakani tokea tupate Uhuru wetu, kwa "mbeleko" ya vyombo vya dola vya Jeshi la Polisi na TISS, badala ya vyombo hivyo vya dola kuwa "neutral" kama vinavyotakiwa kuwa kwa mujibu wa Katiba, badala yake vimekuwa mstari wa mbele kuwalinda watawala wetu na kujigeuza kuwa vitengo vya CCM ili watawala hao wasing'olewe madarakani.