Zamani nilipenda sana kula maharage. Harage zito lililoungwa na vitunguu vingii na hoho, nazi au maziwa. Nilikuwa nikijaza maharage kwenye sahani wali unakuwa tepetepe, basi nilikuwa napenda kweli.
Hata enzi zile sekondari nilikuwa nakula tu naweka vitunguu, sukari na blueband na pilipili
Sijui nini kimetokea yamenikataa kabisa jamani nikila tumbo linaparanganyika kama vita humo ndani. Itanifanya hivyo hata wiki nzima au mbili jamani mpaka nimeyaogop. Sasa nayamiss leo naona yamepikwa hapa nimeona nilee kidogo nikanywa na maziwa nilipomaliza kula.
Je, kuna wengine mmeyashindwa kama mimi? Vidonda vya tumbo nimepima sina.
Nini itakuwa tatizo wajameni?