Siku hizi Ligi za Ulaya hazina watazamaji wengi huku kwenye vibanda umiza

Kwa nini AFCON hatufanyi vizuri?
Kwa nini hatuchukui ubingwa CAF?
Ukipata jibu kikosi cha Argentina kilikuwa na wachezaji wangapi wanaocheza ligi ya Argentina utapata jibu pia kuhusu AFCON.

Kwanini hatuchukui CAF? Jibu jepesi tu miaka kadhaa nyuma tulikuwa hatujawekeza ila kwa sasa tupo kwenye njia sahihi kabisa.

Napata ujasiri wa kusema ndani ya miaka mitano kati ya Simba au Yanga ataleta ubingwa wa CAF Tanzania.
 
Hoja hapo ni kuwa ligi nyingi za ulaya unaweza kutazama kupitia simu yako tena free bila sijui vifurushi ni Mb zako tu chanel nyingi zinaonesha ligi hizi kuliko hiyo ligi yako unayojisifu nayo
 
Ni wewe na mazingira uliyopo, mtaani kwangu hawaambii kitu kuhusu EPL.
 
Kuna ukweli kweny hili. Mitaani mechi za kibongo hasa za simba na yanga zinajaza sana zaidi hata ya Arsenal vs Man u au Man City! Kinachotokea ni kilekile kilichotokea kwenye mziki wa Marekani hapa nchini.
Hapo umenena mkuu. Bongo tunajitahidi sana kwenye upande wa burudani

Ukiachana na mpira kuna kipindi nilikuwa siwezi sikiliza kabia Bongo Flava ila siku hizi najikuta siku nzima ni Bongo tu.
 
Mpira wa ulaya umekua wa ki sayansi zaidi kuliko sanaa kama ilivokua miaka ya nyuma.

Ligi ya Tanzania inakuzwa na utani wa Simba & Yanga, papatu papatu za kupata points 3 kwa njia za kuhonga marefa, wachezaji kupewa majina ya utani mfano "Disconector", utani wa wasemaji wa Simba na Yanga.

Ligi ya Tanzania itaanza kupoteza radha siku wakileta VAR na Viwanja vyote vya Ligi vikiwa na hadhi ya "lupaso".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…